Majina ya miji/maeneo na maana zake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majina ya miji/maeneo na maana zake

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Ambassador, Aug 11, 2010.

 1. Ambassador

  Ambassador JF-Expert Member

  #1
  Aug 11, 2010
  Joined: Jun 2, 2008
  Messages: 932
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Jana tulikuwa na boss mzungu mahala tunakula stori mara akaanza kutuuliza maana ya majina ya maeneo mfano Mwananyamala, wasahikaji wakawahi mtoto nyamaza na kumtafsiria kwa kingereza. Alipouliza Kijitonyama mmoja akasema kijito is a stream and nyama is meat. Tulibaki hoi kwa vicheko.

  Nasikia baadhi ya majina ya maeneo yanatokana na historia ya mahali hapo au tukio muhimu lililotokea wakati mengine yanahusishwa na watu maarufu walioishi mahali hapo, wakati majina mengine hayana maana.

  Hebu tuchangie majina ya miji/maeneo tunayoyafahamu na maana yake, tukianza na hilo la Kijitonyama.
   
Loading...