Majina ya mawaziri wanaopaswa kujiuzuru yatua mezani kwa JK

Status
Not open for further replies.
Hii nchi ya ajabu sana upande huu unakutana na Waziri magufuri ana uwezo mkubwa lakini hasikiki akichukizwa na ufisadi, upande mwingine unakutana na waziri Mkulo uwezo mdogo na ni mtafunaji mkuu wa pesa za umma, upande mwingine unamkuta Mlugo uwezo wake mdogo sana hafai kuongoza wizara hata kuiibia hawezi.:ranger:
 
Huyu jamaa akili yake anaijua mwenyewe!!!

b5.jpg
 
Mkuu nakukumbusha kuwa kuna mmoja kati ya Mawaziri wanaotakiwa kujiuzuru, kupisha nchi ielekee kwenye neema. Naye ni Proffesor Jumanne maghembe. kuhusu issue ya stimulate package kwa wafanya biashara wa pamba ambayo hata mzee mzima Wassira na kimada wake alikwapua mabillioni ya walipa kodi, pamoja na issue ya wakulima wa korosho.
 
Nchi hii inavyoendeshwa na kutafunwa left, right and centre huku wananchi wakiteseka, natamani niingie porini nijiripue nifilie mbali.
 
nchi yaa kusadikika wanaishi kwa kutegemea mamlaka ya Rais kweli hatuna uwezo wakuwadabisha hao wanaokwapua mali zetu?
 
Tanzania inajengwa na wenye moyo na inaliwa na wenye meno. Mrema alisema
 
Unajua serikali ya CCM ukifuatilia yanayo jiri kila siku,unaweza ukashikwa na uwendawazimu.
Waliniacha hoi juzi usiku wakati mbunge wa nkasi kupitia CCM akigomba na serikali ya chama chake utadhani yeye yuko upinzani.
Kweli CCM haijui kula na vipofu,sasa walewale wanao jua mianya ya kulia hela CCM ndo hao hao wanao waumbua.
Tutasikia mengi.
Kikwete unakazi Baba.
Hawa jamaa wanakuchezea akili.
Wanakula wenyewe alafu wana anza kupiga kelele.
Yaani ni kama ma tumbili yaliyokutana kwenye shamba la Bibi nakuanza kula mahindi,alafu baadae matumbili mengine yanaanza kupiga kelele ati wanaiba mahindi Bibi njoo.
Fulish kabisa.
 
HATMA ya mawaziri watano wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa mali ya umma sasa iko mikononi mwa Rais Jakaya Kikwete, kufuatia hatua ya wabunge wa Chama cha Mapinduzi kutaka watendaji hao wajiuzulu. Habari za kuaminika kutoka ndani ya kikao cha wabunge wa CCM kilichofanyika jana mchana mjini hapa zimesema kuwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, ameamua kulifikisha suala hilo mikononi mwa Rais Kikwete kwa uamuzi zaidi.


Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho, kimewataja wabunge wanaotakiwa kujiuzulu kuwa ni pamoja na waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami, na Naibu wake, Lazaro Nyalandu, Waziri Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),George Mkuchika, Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

CHANZO: TANZANIA DAIMA



Wana Jf,
Mawaziri tajwa hapo juu wakijiuzuru ntaaanza kuamini CCm kwa kiasi furani wame anza kukomaaa kizalendo


 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom