mokala1989
JF-Expert Member
- May 4, 2013
- 2,236
- 731
ni habari iliyonisikitisha sana...........maombi yangu ni kwa wanafamilia na wapendwa wote ambao msiba huu umewagusa kwa karibu sana kwamba mungu awape faraja yake na awafanyie wepesi katika kipindi hiki kigumu wanachopitia.
subiri nikuelimishe bwana mdogo.
(1) unapozungumzia swala la jeshi kwenda kulinda amani maana yake ni kwamba hili eneo au hapo mahali pana machafuko ya vita, kwa hiyo ni lazima jeshi lipelekwe kwenda kutuliza hayo machafuko ya kivita....
(2) pia, kutokana na mahali hapo kuwa na vita ndio maana wanajeshi wanatakiwa wabebe silaha, tena nzito za kivita kwa ajili ya kuakikisha hilo eneo linakua na amani...
(3) hizo silaha wanazobeba sio urembo, ni silaha wananzotakiwa kuzitumia pindi adui anapokua anataka kuleta za kuleta....
(4) kwa hilo, huko somalia ni vitani na wanajeshi wetu wapo vitani... Hilo unatakiwa ufahamu...
Sasa swali la kujiuliza, jeshi letu limeenda vitani kwa manufaa ya nani hasa, un?? Kwa taarifa yako hizo vita za namna hiyo zinaigharimu sana taifa letu, kuanzania human capital, financing, equipment etc...
Pia, inakupasa utambua hatuna sababu ya msingi ya kupigana vita sasa... Je, tumepakana na somalia? Wacha kila mtu atatue matatizo yake na sio kujifanya kimbelembele...
Hayo maneno uliyoandika hapo chini ni upumbavu na kukosa akili kuliko pitiliza.
Rest in peace askari wetu. Mmekufa kishujaa
Kuliko kuwa JW kwa Tanzania kwa sasa hata ukifia kazini familia yako inaambulia maneno matupu na watoto wako wanakuwa machokoraa bora kujiunga na walume M23 maana kule mkipiga fungu linakuwa la uhakika
Tanzania ina wajibika kuona dunia ni mahali salama pa kuishi kwa nadharia na kwa vitendo. Ni wanajeshi wa TANZANIA. wameifia Tanzania
Sad day kws TPDF, na RIP kwa hawa vijana wsliojitolea maisha yso kwa ajili ys amani.Majina ya askari saba wa Tanzania waliokufa kwenye shambulio la ghafla mjini Darfur yamepatikana.
Askari hao waliokufa ambao walikuwa kwenye vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa huko nchini Sudan ni :-
1. Sajenti Shaibu Othuman,
2. Koplo Oswald Chaula,
3. Koplo Mohamed Juma,
4. Koplo Mohamed Chikilizo,
5. Pte. Rodney Ndunguru,
6. Pte. Peter Werema,
7. Pte. Fortunatus Msofe.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye mtandao ni kwamba askari hao walikwenda kujaribu kumwokoa mwenzao (ambaye hakutajwa) ambaye alisemekana kutekwa na vikosi vya waasi nchini humo.
Wakati wakijiandaa, ghafla walizingirwa na askari hao waasi na kisha kushambuliwa kwa risasi hadi kufa.
Haikufahamika hali ya askari huyo ambaye alidaiwa kutekwa kama bado yu hai ama ni miongoni mwa waliokufa.
Mungu azilaze roho za askari wetu mahali pema peponi, Amina.