Kibanga Ampiga Mkoloni
JF-Expert Member
- Aug 9, 2007
- 19,077
- 9,240
This is a sad news; nawapa pole familia za marehemu wote, JWTZ na Watanzania wenzangu kwa pigo hili. Moyo wangu ulishtuka kwani nina dadangu ambaye yuko huko kwa kazi hii. Mungu azilaze pema roho za marehemu na kuwafariji familia.
Ni kweli mkuu,ngoja tuone kama watazisaidia familia zao.Maana that's what's important now.Inatia uchungu kweli kwa hawa ndugu zetu kupoteza maisha, kinachosikitisha ni pale fedha wanazotakiwa kulipwa wanejeshi hawa viongozi wa juu wanazifanyia ubadhirifu tukumbuke yule kiongozi wa juu wa jeshi mwenye tuhuma za kuhifadhi fedha uswiss na fedha zenyewe ni malipo kwa wanajeshi waliokuwa katika ulinzi wa amani kama hawa ambao leo wamepoteza maisha yao.hii inasikitisha tena saana.
Hivi mkuu wameifia Tanzania ama Sudan?Naomba kueleweshwa kwenye hili.Kuuliza si ujinga mkuu wangu.Kila nafsi itaonja mauti. Imeandikwa. Pumzikeni kwa amani, Makamanda. Mmeifia nchi. Tanzani. Kifo cha kishujaa. Mungu ibariki Tanzani.
Hivi mkuu wameifia Tanzania ama Sudan?Naomba kueleweshwa kwenye hili.Kuuliza si ujinga mkuu wangu.
Ni wanajeshi wa umoja wa mataifa waliotokea Tanzania?Tanzania ina wajibika kuona dunia ni mahali salama pa kuishi kwa nadharia na kwa vitendo. Ni wanajeshi wa TANZANIA. wameifia Tanzania
Ni wanajeshi wa umoja wa mataifa waliotokea Tanzania?
ndiyo. wametoka Tanzania, wameifia Tanzania.
Vifo hivi viwakumbushe wanajeshi wetu kwamba watanzania wote ni ndugu na kwamba sote ni mavumbi na mavumbini ni lazima tutarudi. Mateso wanayoyafanya wanajeshi kwa raia wa Mtwara ni ya kinyama!!! Si ya kiutu hata kidogo!!! Ni bahati mbaya kwamba jeshi letu linatumiwa vibaya na wanasiasa!!! Mungu aturehemu sote na roho za wanajeshi hawa zipumzike kwa amani!!