Wadau habarini,
Miongoni mwa waliofanya makosa ya Kidemokrasia kwenye Uchaguzi Mkuu 2015 ni wapiga kura wa Jimbo ya Singida Mashariki.
Ukweli Jimbo hili hadi leo bado lipo chini sana Kiuchumi ukilinganisha na Majimbo mengine.
Jimbo hilo linakabiliwa na changamoto kadha zikiwemo ukosefu wa huduma muhimu za Jamii.
Changamoto hizi kiukweli zimeendelea kuwepo pamoja na ahadi nyingi walizopewa wakazi hao kwa nyakati mbalimbali.
Wakati umefika sasa kwa wakazi hao kuamka mapema kwa kujiandaa ili muda muafaka utakapofika mfanye maamuzi sahihi ya kidemokrasia na kufuta makosa mliyofanya hapo awali.
Mnaweza tu kuondokana na hali halisi mliyonayo kwa kufanya maamuzi sahihi kwa kuzingatia ubora wa chaguo lenu badala ya kuchagua kiushabiki.
Msikate tamaa ila msifanye makosa tena.
Aksanteni.