balibabambonahi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2015
- 15,370
- 13,767
Wakati anaibuka alionekana kiongozi mzuri lakini loo,alikuwa bado kuonekana rangi yake kamili.Yuko wapi nguli,Shaaban Robert,alipoongelea tofauti kati ya Karama na Majivuno?
Je,huyu alifikiri yeye ni Fumo Lyongo wa mji fulani uliopo pwani ya Azania? Kijana kaja na tongotongo zake ,akaleta mbwembwe utafikiri yeye yu msafi na makini au ungefikiri yeye ni Hunju bin Unuk wa kizazi hiki.
Ni mwendo wa kurupu kurupu hata akapigwa changa la macho na mtoto mmoja wa mjini hukooo,Gezaulole.
Kalikoroga kweli maana wengine wanasema ,Karma imemgeukia sasa maana,kuna mzee fulani hapa miaka kadhaa iliyopita inadaiwa alitendewa vibaya na kijana huyu.
Tatizo la kijana huyu mmmh,ngumu kumeza maana ana mawaa kila upande,waswahili wanasema muache alinywe maana mtaka nyingi nasaba hupata mingi misiba.
Hayo yana mwisho wake lakini nani ajuaye mwisho wake utakuwaje.tulianza na safari ya matumaini,baadaye safari ya mabadiliko kwa kazi tuu leo ya wapi?
Yule mzee hapo kabla alitwambia ari mpya ,kasi mpya na nguvu mpya lakini mwanazuoni mmoja akasema ni ANGUKA,watu hawakuelewa alichomaanisha lakini kichapo kilipoanza ndo tukajua alikuwa na maana gani.
Yangu mimi Pangu Pakavu tia mchuzi ni hayo ngoja tusubiri na kuona.Alamsiki.