raster kipara
JF-Expert Member
- Jun 15, 2014
- 218
- 43
Air ukawa
Ndugu zangu wananchi, nimepigwa mishale ming sana, hata watoto amabo nimewasaidia kupata ubunge leo wanakuja kunitukana , wanasema kuwa ninagawa kura za wapinzani, hivi mtu waliyemwona hafai ana ana nguvu gani ya kugawa za kura za wapinzani?
sisi ACT wazalendo tumekubali kuungana (kwenye ukawa) wao hawataki hapa nani mbaya? Ngombe anaweza kutikisa mkia lakini mkia hauwezi kumtikisa ngombe
ACT wazalendo kukataliwa kwenye ukawa, hakitatetereka na juhudi za kusamabaza uzalendo kwa watanzania. Na sambamba na kujipanga na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi octobet mwaka huu.
Source Raia mwema
Mtu aliyeonekana hafai anaweza vipi kugawa kura za upinzani?? Mkia hauwezi kumtikisa ngombe ila ngombe anaweza kutikisa mkia hahahahaha., mkuu panic iko wapi hapo?
Watanzania hatuna chuki binafsi na Zito bali tuna chuki kubwa kwa yale aliyotufanyia. Mengi yamesemwa juu yake lakini hajawahi kuyajibu kwa vielelezo. Hajawahi kueleza kwa ukamilifu hela aliyokuwa akiipokea toka CCM (kwa kupitia maofisa wa TISS) ilikuwa ya nini? Hajawaeleza Watanzania ukaribu wake mkubwa na mawasiliano yake na maofisa wa juu wa TISS yamekuwa yanahusu nini hasa. Mawasiliano na maofisa wa TISS yalioneshwa kwa vilelezo, na hasa yalikuwa wakati wa kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi.
Leo anapotaka kushirikiana na UKAWA, Watanzania watakuwa na uhakika gani kuwa nia yake kubwa siyo kutaka kujua mipango na mbinu za UKAWA kwa manufaa ya wale ambao amekuwa akiwatumikia siku zote, CCM?
Zito kabwe ni uchuro namtakia safari fupi afie mbali kisiasa
Lakini mkuu, kwanini zzk ndio adui yenu number 1 badala ya ccm?? Au na ninyi ni mapandikizi tu kuhadaa watz?? Back to the point,cuf wanamkubali kinoma na wako tayari kushirikiana sasa ninyi mna nini nae?? Au mlitaka akalime?mtu alliyeonekana hafai na kufukuzwa kwenye chama kwa usaliti atakaribiswa vipi tena kwenye umoja wa wanamageuzi wa ukweli??
Zitto amepanic
Mkuu itakuwaje kama NCCR, NLD na CUF watataka kushirikiana na ACT? Tatizo mnaifanya UKAWA kama CDM na CDM kama UKAWA. Hapo ndipo penye shida kubwa.