TUJITEGEMEE
JF-Expert Member
- Nov 6, 2010
- 23,914
- 23,079
Yaani kutakata kote huko ni 40 bilion za wizi!! Haki itendeke. Ndiyo maana nilikuwa nahimiza kauli ya hapa kazi tu iboreshwena kuwa HAPA KAZI NA HAKI TU.
Unaongea wakat huo akiwa waziri wa nishati wakat wa JK saiv ni tamisemi
Katika utetezi wake ndani ya gazeti la Mwananchi la leo, uamuzi wake wa kutofuata sheria ya Mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji(EWURA) ya kushindanisha zabuni ya uingizaji mafuta nchini na hatimaye kufanya serikali kutumia bil 40 zaidi ya zile ambazo ingelitumia kama sheria ingefuatwa jambo lililosababisha bei ya mafuta isishuke nchini wakati ilikuwa chini soko la dunia, Waziri huyo wa Nishati na madini wa serikali iliyopita( ambaye kwa sasa ni waziri wa Nchi ofisi ya Rais,Tamisemi) anadai ni kwa sababu za wasiwasi juu ya hali ya usalama kipindi cha uchaguzi
Mimi sio mjuzi wa masuala ya uchumi na kiusalama lakini naamini tathmini ya hali ya kiusalama na madhara yake hufanywa na vyombo husika vya usalama, hasa shirika letu la ujasusi TISS ambao nadhani wanakitengo kinachohusiana na mambo ya uchumi. Sasa maswali yanakuja
1.Waziri alifanya tathmini akiwa kama nani? Alishirikisha mamlaka zipi?
2.Kwa nini hakufuata ushauri EWURA ambao walimshauri kuwa mafutwa yasiingizwe bila mzabuni ili bei isiwe juu
Waziri inasemekana ana uhusiano mkubwa sana na viongozi wa kampuni iliyopewa tenda hiyo, na pia ana ndugu yake anayefanya kazi kwenye hiyo kampuni. Pia baadhi ya watendaji wa kampuni hiyo alishauri au kuagiza wapatiwe ajira hapo( kinachoonekana maandalizi ya upigaji fedha huo)
Kuna shaka waziri atakuwa anahusika katika faida hiyo ya bil 40. Huu ni ufisadi, Hili jipu Rais Magufuli alitumbue
Waziri Simbachawene anatoa majibu ambayo hayaeleweki kabisa. Washauri, kama walivyo EWURA, wanaajiliwa ili watoe ushauri na ushauri yapaswa yazingatiwe kwani wao ni wataalamu na wanategemewa sana serikali. Iweje mtu kama waziri anayehimiza uadilifu atoe maamuzi yanahusisha Sh.40 billioni bila kufuata ushauri na taratibu na kanuni zilizowekwa?????
Kuna NAMNA, ni vema kufanyike uchunguzi zaidi, hili ni JIPU KUBWA. Huyu na yule aliyetuma sms kwa Mama CHUWA, hawanatofauti. Fuatilia
Inaonekana kazipiga yeye binafsi
Huyu Simbachawene ilitakiwa hapa tunavyojadili hii habari awe tayari yuko Segerea. Kapiga dili la bilioni 42 kwa mgongo wa sisi walalahoi tunaotaabika sasa na kununua mafuta bei kubwa
Mkuu hata mimi nashangazwa na ukimya huo, ila naamini wanayafanyia kazi.majibu yake ni mepesi sana.
kama taratibu na sheria za manunuzi zimekiukwa wahusika inabidi wachunguzwe na pamoja na kufunguliwa mashtaka.
inasikitisha kuona mamlaka kama PPRA na PCCB wakishindwa kuchunguza suala hili na kujua ni halali au batili.
Anatakiwa awe mfano kwa mawaziri wengine
Magazeti ya The Citizen na Mwananchi ndiyo yaliandika, baada ya kama wiki hivi nikamsikia Mnyika akilizungumzia hili, sio mshabiki wa Chadema lakini nilifurahishwa na hilo, alisema wataliwasha bungeni hilo likifunguliwa. Hivi ndivyo jinsi ya kumuunga mkono Magufuli katika kuhakikisha taifa linasonga mbele na sio poroji, kejeli, maandamano n.kKatika vitu vinampa shida sana muda rais Magu ni mawaziri Wa jk waliochaguliwa tena awamu hii wengi WAo walizoeya rushwa tena grand corruption ukianzia huyo simbachawene kina makamba name wengneo SAS ili kuwatumbua HAWA jamaa na kumpunguziaa mzigo raisi hii ni opportunities kwa upinzani kutumia hizi gaps kumsaidia rais kutumbua majipu mana nao wapinzani wapo kimya hawafichui uvundo aina hii pak magazeti ndo wana mchango mkubwa kuweka wazii ufisadi mbalimbali.#TupazeniSautiUfisadiiTuumalizee
mngony;
Labda husomagi post za wengine ila tumeshasema saana tu kwa habari ya kuwajibika. CCM hainaga msamiati huo wa kuwajibika.
Hata mpige kelele Tz nzima, haifiki Magogoni au Mnazimmoja. CCM wanafarijiana kuwa; Huo ni upepo tuu unapita, utulivu unafuata punde.
Hatoki mtu hapo. Tena Simba cha wenyewe. Mmekoseaaaaaa
KWA kijiti cha yule mama ama??mt zilizimwa wapige kaziKuna mtu mwenye takwimu zinazoeleza jumpa ya lita au tonnes za mafuta zilizoagizwa ktk kipindi hicho cha Simbachawene ili tukokotoe jumla ya cha juu kilicholiwa?