Adharusi
JF-Expert Member
- Jan 22, 2012
- 14,402
- 7,310
Comrade Mwigulu Nchemba tumekuelewa wenye akili.. Na kupongeza sana kila mara unakuja kutotoa ufafanuzi..
Ila wewe ni kichwa period.
Habari yeye ungempelekea aliyekuteua Uwaziri,basi.Ungekuwa umemaliza mchezo lakini kwa kuuleta hapa jamvini na niliyoyaona ndani yake,you are inviting more questions!!Salama comrades?
Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.
Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.
Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.
Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.
Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.
Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.
Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.
Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira
Mwigulu,
Kwema mkuu Shumbi?
Kwanza nikupongoze kwa ujasiri wa kujitokeza hadharani na kujibu tuhuma hizi. Hakika huo ni ukomavu na uungwana uliotukuka.
Nimefurahi pia kujua maana ya neno Mwigulu na Madelu leo. Asante sana. Ila mzee, hapa tutakutwanga tu maswali kwa heshima na taadhima. Usitukimbie tafadhali..
Sasa mie swali langu ni moja tu hapo kwenye kuamua kuchukua majina ya huyo nesi/daktari.
Ninachouliza, yeye hakuwahi kusoma? Na kama alisoma alitumia majina gani? Huoni kwamba utakuwa umechanganya kuchukua jina lililowahi tumika kutahiniwa? Nadhani hapo ndio msingi wa maswali haya kuibuka...
Iliwezekanaje kutumia majina ya daktari kwenye taaluma ilihali na yeye aliyatumia pia?
Salama comrades?
Nimeiona thread hii: Mwigulu, Kigwangalla, Makonda jibuni tuhuma hizi nzito, aliyeandika naona hajui historia yangu.
Ni vema kuweka rekodi sawa:
Kwanza anasema nilikuwa nanaitwa Lameck Madelu Mkumbo, sasa moja Lameck sio jina la kinyiramba, na Madelu sio jina halisi la baba bali ni utani kuwa ana ndevu nyingi, yaani ni mandevu, ndio maana hata kwenye ubunge nililiongeza tu kama a.k.a ili watu hasa wazee wanifahamu hili haliko kwenye vyeti.
Hili la Lameck siyo jina la kinyiramba ni jina la daktari aliyenipokea zahanati ya Iliyopo kijiji cha Mukulu, daktari tunaita hivyo lakini ni Nesi ndiye aliyekuwa anaitwa Mwigulu na jina la kizungu Lameck. Mimi nilipelekwa hosipital nikiitwa Mugulo na jina la ukoo kwa watoto wote wakiume ni Shumbi ambalo hata hivyo wanatumia wazee tu wanaojua kinyiramba hilo ndio jina la kinyiramba. Mama akaulizwa jina akanitaja Nesi yule akamwambia mama unamwitaje jina hilo hakuna lingine mama akamwambia hakuna labda mtaje wewe, basi jamaa akajitaja. Hili lilikuwa jambo la kawaida sana kijijini kwani familia inakuwa na watoto wengi mpaka majina inakuwa sio jambo la kujali sana. Hata pale kijijini kuna wengine waliotajwa majina ya waganga wa kienyeji wazee walikopewa dawa, majina ya manesi/matabibu kama mimi, majina ya walimu nk.
Kuhusu Elimu:
Mimi niliacha shule kwa mara ya kwanza 1984 baada ya kuanza na kaka yangu aitwaye Jugulu, mzee akasema tupeane zamu, nikaacha. Nikaanza 1985, nikaachia darasa la tano nikaenda kuchunga miaka kama miwili. Nikarudi tena baada ya mifugo kuanza kufa sana, mzee akashauri awekeze kwenye elimu. Walimu walikuwa wanashinda nyumbani kumsihi anirudishe shule, ndio nikarudi na nikachukua majina ya daktari. Mtu asichanganye kuona ni udanganyifu, mimi sijachukua vyeti vya mtu. Nimefanya mitihani tena kwa kupiga na picha za passport ili mtu asitumie haki ya mtu mwingine aliyefaulu, na mpaka sasa naona ni struggle za mfano kuwa nilisoma kwa mazingira ya kutoka kuchunga na kurudishwa shule na kufaulu mwenyewe.
Kwa anayetaka kuthibitisha haya anaweza kuwauliza niliosoma nao shule ya msingi.
Comrades, kwa mawazo yangu kosa ni mtu kuchukua nafasi ya mtu aliyefaulu na kwenda yeye, hapo ni kuiba haki ya mtu. Najua hii ilikuwa ikitokea baadhi ya maeneo, mtu anafaulu ila anakuwa hataki kwenda shule au amefariki then anakwenda mwingine. Mimi sijawahi chukua nafasi ya mtu. Halafu watu wanasema jina la mtu, labda kama wanamaanisha tofauti na wizi wa jina kwani kila mmoja hapo alipo ana jina la mtu, yaani atakuwa John wa biblia, Mohamed wa quran, litakuwa la babu, la bibi, la mganga, la daktari, la rafiki, la kiongozi, la tukio nk.
Nijuavyo, jina unakula kiapo tu kama sio la kwako kisheria na unatumia, na hata sasa nikitamani jina jipya nakula kiapo na kutangaza gazeti la serikali na lisipopingwa ndio linakuwa jina langu jipya.
Hoja ni kama mtu kapora cheti cha mtu, kapora nafasi ya mtu mwingine aliyefaulu akaenda kuisomea yeye. But, things do change pia kutokana na nyakati na mazingira
Mwigulu,
Tunampongeza kwa kuonyesha ungwaana wa kuja kujibu tuhuma hizi ingawa majibu bado hayaridhishi.safi kabisa Bavicha wote chaliiiii kifo cha mende.
kama ulikuwa na siku saba kwanini uje tena kuchukua jina ulipoacha darasa la tano?Yaani daktari hakuwa shule, hakuwa umri wangu, alijitaja nilipopelekwa nikiwa na siku saba, kama hivi mtoto akizaliwa siku ya mwenge kule simiyu wapo wataitwa Mwenge, hivyo alinitaja, na kuna mtoto wa rafiki yake baba tulizaliwa wiki hiyo naye aliitwa jina la huyo nesi, sikuchukua jina kwa kuomba wala hatukuwa tunaongea mimi nilikuwa mchanga bhana
Ila wewe ni kichwa period.
Na mwenye kusoma PhD kwa miaka 3 badala ya 5 aje nae hapa ajibu tuhuma zake tena yeye akiwa ndio kiongozi mkubwa.Natamani na MBOWE ajitokeze kujibu tuhuma zake.
Na siku Mbowe akijitokeza basi nijitoa kabisa kushabikia siasa.