Majibu ya Sitta kwa Dr Slaa: Asema Dr Slaa Mnafiki, Dikteta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya Sitta kwa Dr Slaa: Asema Dr Slaa Mnafiki, Dikteta

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mpotevu, Sep 3, 2012.

 1. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Yafuatayo ni majibu ya Waziri Sitta kuhusu kauli ya Dr Slaa aliyoitoa Majuzi mkoani Iringa

  Nimesikitishwa na kauli za jazba na mwangwi wa kiwewe za Mhe Dr W Slaa alipokuwa Iringa juzi hadi kuniita mnafiki, mwongo, mtu wa hatari n.k

  Hali hii inatia mashaka juu ya uwezo wa kiongozi huyo wa kisiasa kuhimili kukosolewa ambayo ni sifa muhimu ya maisha ya mwanasiasa yeyote hususani anapojinadi kuwa anaweza kuchukua madaraka ya kuiongoza nchi.

  Kauli zisizo na staha alizozitoa Dr Slaa dhidi yangu kama vile sifai hata uongozi wa kata zinadhihirisha mambo mawili:

  Dr Slaa ni dicteta. Hana uvumilivu. Ana hulka ya kujiskia kwamba mawazo yake hayapingwi.
  Ni mzushi asiyeogopa kusema na kupindisha mantiki ya jambo ili tu kushinda hoja. Iweje mtu aliyenibembeleza nigombee uraisi kupitia chama chake mwaka juzi leo aseme sifai kuongoza hata kata kwasababu tu nimetamka ukweli juu ya udhaifu wa chama chake cha siasa?

  Niliyoyasema pale Karagwe majuzi katika uchambuzi wangu wa vyama vya siasa nchini ni kwamba CHADEMA wamekuwa hodari wa kukosoa na kuishambulia CCM na serikali zake lakini wanasau kuwa ili wawe mbadala kwa kuiongoza nchi hawana budi kurutubisha safu yao ya uongozi nawe na watu wakutosha kuweza kushika madaraka ya ngazi mbalimbali za uongozi wa Taifa. Kuukataa ukweli kwamba safu ya uongozi wa CHADEMA ni nyembamba ni kujidanganya tu.Kupita mikoani kutangaza kwamba matatizo yote ya wananchi yanatokana na CCM ni kazi rahisi na ina mvuto wake kisiasa lakini mwanasiasa makini hana budi kwenda mbele zaidi ya hapo.

  Hana budi kutuambia wapiga kura mipango ya chama chake inayoeleweka na inayotekelezeka na iliyo makini kukabiliana na changamoto mbalimbali za maendeleo ya nchi. Ahadi za alinacha za tiba bure, elimu bure bila kuonyesha vyanzo halisi vya mapato ni porojo tu. Kusema kwamba raslimali za nchi kama vile gesi asilia, madini, makaa ya mawe, utalii zinatosha kuondoa umaskini ni nadharia tupu ambayo uhalisia wake hauna budi kubainishwa kwa mikakati dhahiri na thabiti ya kiutawala (uendeshaji) inayoweza kuchuma utajiri huo kwa ufanisi, kwa uendelevu na kwa faida ya wengi1. Kuhusu mwenyekiti Mh Mbowe – MB

  Katika hotuba yangu sikukejeli uzoefu wa Mhe Mbowe, wala sijasema Mhe Mbowe ni mcheza disko. Niliuchambua wasifu wa viongozi wa CHADEMA na kutamka uzoefu wa Mhe Mbowe katika vitega uchumi vya burudani hii siyo kudharau bali ni kutamka ukweli tu.Huwezi kuuelezea wasifu wa Mhe Mbowe bila kuelezea mchango wake mkubwa katika tasnia ya burudani.Mmoja wa maraisi maarufu wa marekani (USA)alikuwa ni mcheza sinema Ronald Reagan.Na hapa Tanzania tulikuwa na mzee R. Kawawa ambaye alianzia katika tasnia ya uigizaji, kwa hiyo Mhe Mbowe au Dr.W. Slaa anaweza akawa Rais wetu kwa maana ya kupigiwa kura za uchaguzi wa demokrasia.Kumudu au kutoyamudu madaraka hayo ni suala tofauti. Tathmini yangu ilihusu safu nzima ya uongozi wa CHADEMA kwa ujumla wao.Ni safu nyembamba mno.

  2. Kujiunga na CHADEMA

  Kama alivyosema Dr. Slaa Chadema walifanya jitihada ya kunishawishi niingie CHADEMA 2010 na niwe mgombea wao wa Urais. Jambo hili nililitafakari na kutafuta ushauri kwa watu wangu wa karibu na nikabaini kwamba:-

  CHADEMA wana migawanyiko yao ya uongozi tena ni ya hatari kwasababu ni ya kikanda za nchi – yaani nani anatoka wapi.

  Kutokana na yaliomo katika ilani yao ya uchaguzi 2010 – 2015 nilibaini mambo ya kiitikadi ambayo siyakubali kama vile sera ya majimbo. Sera ya majimbo inawezekana katika nchi ambazo ni tajiri na pia isiyo na tofauti kubwa ya hali ya maisha baina ya kanda mbalimbali za nchi kama vile Marekani (USA). Kuleta majimbo Tanzania ambako kuna tofauti kubwa za kimaendeleo baina ya Kaskazini, Mashariki, kati, Kusini na Magharibi ni kusababisha nchi ichanike vipande vipande.

  Huduma bure za elimu kuanzia chekechea hadi chuo kikuu na huduma bure za afya kwa wote ni ndoto na ni ghilba kwa wananchi. Isitoshe siamini kwamba kazi ya Serikali yoyote Duniani ni kuwalea Wananchi kwa umaskini huku ukiwaahidi huduma za bure badala ya kuwaendeleza wajitume na waongeze kipato ili wamudu gharama za maisha. Kwa hiyo nisingeweza kuwa mgombea Uraisi ndani ya chama ambacho itikadi zake za msingi sikubaliani nazo.

  Baada ya hapo nisingeweza eti baada ya uchaguzi Mkuu niombe kugombea Uspika kupitia chama cha CHADEMA.

  3. Kuhusu CCJ

  Kama ilivyo kawaida kwa vyama vya siasa kutafuta wagombea bora, CCJ ni miongoni mwa vyama vilivyonifuata mimi na baadhi ya wanasiasa wakati wa maandilizi ya uchaguzi mkuu. jambo hili si la siri wala la ajabu na Nimelizungumza hili mara nyingi. Isitokee katika mfumo wa vyama vingi vya siasa mtu kutoka chama kumoja cha siasa na kujiunga na chama kingine haiwezi kusemwa kuwa ni uhaini. Na kama Ningeridhika na mambo yao ningejiunga na CCJ mwaka 2010 lakini sikufanya hivyo. Pia ni uzushi usio na msingi kunihusisha na uanzishaji wa chama hicho. Waanzilishi wa chama hicho cha siasa wanajulikana na wapo hai, ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania kuanzisha au kujiunga Binafsi na chama chochote cha siasa.

  4. Madai mengine

  Eti nilitamka kwamba ningehamia chadema na Wabunge wa CCM 55 ni porojo za Dr. Slaa kama ulivyo usemi ningeihama CCM siku chache kabla ya kuvunjwa Bunge la 9.

  Inashangaza kwa Dr Slaa kukejeli uendeshaji wa bunge la 9 ambalo ndilo lililowapa fursa watu kama yeye kujulikana na kujipatia umaarufu.

  Haya madai ya mimi nikiwa Spika kukwamisha uchunguzi wa Meremeta na Richmond ni kutokana na hisia tu za chuki. Taratibu za Kibunge hazimwezeshi Spika kuwa Dikteta anayeamua nini kijadiliwe na nini kisijadiliwe. Yote yapo katika kanunu za Bunge. Maamuzi ya Bunge si lazima yawe ni ya Spika.

  Kuhusu ofisi ya Mbunge jimboni Urambo mahasimu wangu ndani ya CCM na nje yake wameng'ang'ania kwa makusudi maalum kuiita ofisi ile kuwa ni ya Spika. Michoro yake na gharama zake hata ukijumuisha samani haifikii tarakimu za ajabu wanazotaja mahasimu wangu kujenga hoja istoshe ofisi hiyo haina maslahi yeyote binafsi kwangu Aidha viongozi wengine waliofikia hadhi za juu mathlani ya uwaziri mkuu nao wamejengewa majimboni ofisi zinazolingana na hiyo

  Porojo nyingine binafsi kama vile kumuhusisha mke wangu kumpigia simu Dr Slaa kumsihi anisaidie kisiasa ni upuuzi wa aina yake unaodhihirisha umahiri wa Dr.Slaa katika siasa za kiwango cha chini.

  5. HITIMISHO

  Mimi nikiwa mwanasiasa mzoefu na mkongwe nimetoa ushauri na nitaendelea kutoa ushauri kwa makundi mbalimbali nchini.Kuniambia naingilia mambo ya CHADEMA ni kichekesho.Wakiwa wao ni chama cha siasa kinachoendesha harakati za kuwania kuchukua madaraka ya kuongoza nchi ambayo mimi ni raia wasitazamie kuwa sisi wapiga kura tutaacha kuwachambua.Wanalo tatizo kubwa la safu nyembamba mno ya uongozi, Kulingana na majukumu ya kuendesha nchi.

  Kujilinganisha na safu ya uongozi ya Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere ni mzaha wako wapi akina R.M Kawawa, Pauli Bomani, George Kahama, Amir Jamal, Solomoni Eliufoo, Tewa Saidi, Tewa Abdallah, Fundikira wa CHADEMA? Kutembea nchi nzima kuhamasisha chuki dhidi ya serikali iliopo madarakani ni jambo jepesi lakini Watanzania walio makini wanahitaji maelezo ya mipango mbadala ya uchumi kuinua hali za maisha yao na kuiona safu ya uongozi itakayowezesha kwa dhati kubuni na kusimamia mikakati endelevu ya kuondoa umaskini kujenga uchumi imara na kuimarisha umoja wa watanzania
   
 2. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #2
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Napata mashaka makubwa kwa huyu mzee Six, juzi kamsifia Dr Slaa, leo anamuita mnafiki, sasa hapo nani mnafiki wa kweli? Sita au Slaa?
   
 3. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Namheshimu sana Mzee wangu Sitta lakini hoja yake kuhusu wembamba wa safu ya uongozi wa Chadema, hasa kama hoja yake ya msingi kwanini Chadema hawapo tayari kutawala ni hoja nyembamba sana; isitoshe hao viongozi kama Kawawa, alikuja kuwa KAWAWA baada ya TANU kukamata uongozi; Fundikira alikuja kuwa FUNDIKIRA baada ya TANU kukamata uongozi; same applies kwa orodha ya viongozi wote including Mwalimu; vinginevyo kabla ya hapo, wote walikuwa wanaharakati waliojiunga TANU 1954, na kuja kutwaa madaraka ya nchi miaka saba tu baadae (1954 - 1961); Kinachohitajika na chama cha siasa ni LEADERSHIP, it could be one charismatic leader ambae anazaa followers who later proceed to become LEADERS as well; Mwalimu was the only LEADER wa TANU, and it is because of his influence, he attracted others who later became leaders, ingawa none kwa kiwango chake;

  YESU na MTUME wote hawa walikuwa viongozi, and we all know how they influenced people from different walks of life who later became followers...then leaders..., both BELIEVERS AND NONE BELIEVERS; It has to begin from somewhere;

  Ninaandaa makala kumjibu Mzee Sitta, kama mwanachama mwenzake wa CCM ninayeamini katika dhana ndani ya chama chetu kwamba kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi. Kwanini nataka fanya hivi? Kwa sababu nina amini kwamba BILA CHADEMA MADHUBUTI, CCM MAKINI HAIWEZEKANI!
   
 4. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  ​Lione, linafiki lingine linakuja hapa kujaribu kujikosha ili lionekane siyo fisadi. Wewe Sitta mnafiki mkubwa, utakufa kwa kihoro cha kuwasaliti watanzania kwa manufaa ya mafidi ndani ya chama chenu cha wauaji.
   
 5. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2012
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Utetezi wako unazua maswali zaidi kuliko majibu.

  1. Ofisi ya Urambo haikugharimu milioni 300? Ila iligharimu milioni mia ngapi?
  2. Dr. Slaa amesema hukutangaza tenda. Mbona hujalisemea hilo?
  3. Ni kweli kampuni ya Blandina Nyoni ilipata tenda ya kuleta vifaa vya ofisini?
  4.Kwa nini ulikataa nyumba ya Uwaziri uliyopewa na kung'ang'ania nyumba yenye bwawa la kuogelea inayotugharimu walipa kodi dola 10000 kwa mwezi?
  5. Ni kweli ulikua unataka Uwaziri Mkuu ndiyo maana ukaruhusu hoja ya Richmond ijadiliwe na kuzipuuzia hoja za EPA, KAGODA,BOT na Meremeta? Lowassa na Slaa wanapingana kama mbingu na nchi, lakini kwa hili wanaungana, mbona hujalisemea hili?
   
 6. ugolo wa bibi

  ugolo wa bibi JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 1,231
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  We saba! aaah sita,hebu zeeka salama ni juzi tu, umemsifu dr.slaa leo hii eti oooh kuku kapanda baiskeli acha unafiki ndio maana mara nyingi ukiwa unaongea jasho jingi linakutoka sababu ya kutumia nguvu nyingi kwenye mambo madogo!wewe na wenzio mkaendelee kutafuta umaarufu kupitia makanisa inatosha!
   
 7. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #7
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  very very good analysis
   
 8. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Jamani, huyu mzee nilikuwa namheshimu tena sana lakini kwa hoja hii kwamba CHADEMA haina safu ya uongozi ya kutosha ni upotoshaji wa hali ya juu. Unajua, tatizo la CCM tena lipo kwa wazee sana wa aina ya akina Six ni moja. Wao wamelishwa sumu na chama hiki mfu kiasi cha kudhani kwamba nchi lazima iongozwe na baraza la mawaziri lenye mawaziri na manaibu waziri 60, makatibu wakuu na manaibu makatibu wa kuu wa wizara zaidi ya 60, n.k. Wanasahau kwamba idadi ya viongozi wa serikali ni matokeo ya mfumo wa chama katika kuongoza nchi.

  CCM inatumia vyeo kama zawadi kwa wanachama wake na siyo mkakati wa kujipanga kiuongozi na kujiletea maendeleo. Binafasi bado nina imani kwamba CHADEMA inaweza kujipanga vizuri na kukamata dola bila wasiwasi na dalili nzuri ni namna walivyojipanga bungeni na kubeba majukumu mazito pamoja na uchache wao. Watanzania wengi wasomi katika kila nyanja wamechoka na hiki chama cha CCM na bila shaka endapo CHADEMA itakamata dola watashirikiana vema nacho katika kujenga safu nzuri ya uongozi na kuwaletea maendeleo wananchi.

  USHAURI WANGU KWA DR. SLAA BAADA YA MAJIBU YA SIX:
  Dr. Slaa katika maelezo yako umeonyesha kuwa Mzee Six akikujibu utatoa data au uthibitisho zaidi wa kuonyesha jinsi mzee huyu alivyo mnafiki na asivyofaa kuwa kiongozi wa nchi hii. Tafadhali nakuomba ufanye hivyo kwani pasipo kufanya hivyo tutastukia mzee huyu yupo magogoni na hapo ndipo kitakuwa kilio na kusaga meno.
   
 9. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #9
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  ni kweli anapaswa kujibu haya kama anataka kujisafisha ingawa nahisi anaweza kuwa anajisafisha kwa tope
   
 10. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Nilisema haya katik thread nyingine kuwa kajiweka vibaya.hata anashutumiwa kwa kutoaminika.Sasa leo nathibitisha hilo.Sifa alizompa dr. slaa kwa umakini leo kaanza zikosoa zote.Mzee anajikata mkia wake mwenyewe.Kaingia katika selfe distruction mode.Sasa atakuwa kikimbizana na issue, akimaliza moja kabla hajapumzika CDM wanampa signment ingine.Mzee ata "dance" n akukimbia kivuli chake mwenyewe.Akimaliza dili na individual wa CDM wa CCM nao wana msubiri.Halafu kabla hajamaliza atajikuta mchuano wa ndani ya chama ndio umeiva,na wakati huo ajue kuwa atakuwa na vita na CDM kama chama n amatokeo yote yanategemeana.

  Mbaya katik vita ya ndani ya CCM itakuwa ngumu kwani CCM watapima upepo na kuona naye kachafuka sana na hawezi uzika mbele ya CDM kwa hiyo kumtosha.

  Sikumshauri tangu mapema aingie katik vita na CDM.sasa hapa bado hajamafikia hta katik vita yake na CDm kama chama,bado ankimbizana na individuals.Ndio atakapoona kuwa CDM ina watu wengi wa kujenga serikali, watampokezana sana kaba ya wao kumrudisha katik chama wajibu hoja kupitia rasimu za CDM.
   
 11. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #11
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Hapo kwenye ushauri panafaa sana kufanyiwa kazi
   
 12. KISHOKA_ZUMBU

  KISHOKA_ZUMBU Senior Member

  #12
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  enhe!? Napita tu
   
 13. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #13
  Sep 3, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,295
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Simama ukaguliwe
   
 14. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #14
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,185
  Likes Received: 1,903
  Trophy Points: 280
  Anzisha CHAMA CHAKO maana hata SHETANI hakukubaliana na Mambo ya Mungu akaanzisha Chama Chake... SITTA anataka Kuonekana Juu na hataki kuongozwa bali aongoze ni bora akaanzisha chama chake
   
 15. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sita wewe ni mnafiki kuliko shetani .hivi wale wamisri na watunisia walikuwa na viongozi walipo fanya mapinduzi? Mzee acha mawazo mgando .CDM inawatu ndio maana inakubalika .
   
 16. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Unafiki ni noma ulisema mbowe ni mchezesha disco leo unajifanya kumsifia eti hata Reagan na kawawa walikua waigizaji .mzee umefungulia muziki ambao kuucheza hutaweza.
   
 17. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Safu nyembamba ya uongozi sasa hapo ccm kuna safu gani nene ya uongozi? jitazame mzee sitta amka bado unalala wewe.
   
 18. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #18
  Sep 3, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,460
  Trophy Points: 280
  Tunataka safu ya uongozi nyembamba maana hiyo nene imetufilisi na kutunyonya sana..!!
   
 19. Nkandi

  Nkandi Member

  #19
  Sep 3, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Very logical questions
   
 20. m

  majebere JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Naona gwandaz wote humu hawataki kukubali ukweli. Nyie semeni mtakavyo lakini Sitta amefunga kesi. Slaa hamuwezi huyu mzee.
   
Loading...