Majibu ya Serikali (Wizara ya Nishati na Madini) kuhusu ripoti ya PAC juu ya Tegeta Escrow Account

jKwani PAC walifanya walifanya uchunguzi PAC wamefanya summary ya uchunguzi wa PCCB na wa CAG

Na ndiyo hapo issue ilipo. Tatizo ni nani wa kuaminiwa? PCCB na CAG au Muhongo? Je ni TRA ana TANESCO waliosema sehemu ya hela ya escrow ilikuwa na VAT au Muhongo?
 
You have no idea on what you are talking about. TRA hukusanya kodi kupitia mawakala. Wizara ya Nishati na Madini ni wakala wa kukusanya kodi ama la? Unaelewa dhana ya "withholding tax at source"? That an agent e.g. MEM is required by the law to withhold tax before making payments to other persons. Yaani Wizara inalipa fedha kwa kampuni na inasema si kazi yake kujua kama kampuni iliyolipwa italipa kodi au la? Kwa hiyo, Waziri Muhongo hajali kama serikali inapoteza mapato kwa kuwa ni kazi ya TRA kukusanya mapato? Hii ina maana kuwa Wizara ya Nishati inavyoingia mikataba na wawekezaji hawajihusishi kabisa kuhakikisha kuwa kodi stahili inalipwa? They just let it go kwa kuwa ni kazi ya TRA kukusanya mapato? No wonder hatunufaiki na uwekezaji unaofanyika. Mwajiri wako huwa anakulipa mshahara wote bila kukata kodi kwa kuwa si kazi yake kukusanya kodi? Kwamba ni kazi ya TRA kukusanya kodi? Hoja hii msingi wake ni fikra kwamba kuna "duality" kati ya TRA na taasisi nyingine za serikali. Why invoke dualism concept (which is a misconception) now?

Umeshawauliza tanesco kama hawajafanya withholding? Kumbuka kuna billion zaidi ya 100 wamezizuia Tanesco na au Serikali.
 
Hawezi ondoka hakuna anayeweza kujibu maswali bungeni kama yeye wote waoga so believe me ataendelea hadi uchaguzi atakapomteua waziri wake mkuu
 
LOL!!! Mpwa Elli hata MACCM kuna wakati yanakuwa upande wa wapenda haki na maslahi ya nchi yetu. Ilibidi nimsome jamaa mara mbili mbili ili kuhakikisha alichoandika, ndiyo nikakutanana hili bandiko lako LOL!!!!

Huyu unaemtukana ni ccm mwenzio ujue
 
Last edited by a moderator:
Kosa la Pinda tuliloambiwa jana ni kusema pesa iliyoibwa si ya umma. Sasa kama hivyo ndiyo alivyoelezwa na washauri wake kina Werema yeye angesemaje? Sioni sababu ya Pinda kung'atuka unless you know something we don't know. Wa kung'atuka is the trio from Mara.
Hakuna wa kung'atuka ndugu Gagnija. Ripoti ya PAC ilijaa uzushi mwingi na wakasahau kujibu masuala ya msingi ambayo yangewatia hatiani wahusika wakuu wa IPTL.
 
Huo ulikwisha tatuliwa na ndiyo maana wamelipwa. Na Jaji Utamwa alithibitisha kuwa mgogoro umekwisha kwa kupatiwa mkataba wa IPTL na TANESCO kuwa wameshafikia makubaliano nje ya mahakama kuhusu capacity charges.
Ulikuwa husikilizi?

Mgogoro uliishaje wakati bado IPTL wanaidai Tanesco ?
 
siasa zenu chafu zitaifanya Tanzania kukosa viongozi wenye vision kama Prof. na nakuambia ukweli hiyo mbinu yenu na wafanya biashara baada ya kudhibitiwa mkimtoa Prof kwenye wizara hiyo mtakuja kumbukumbuka katu tegemea umaskini kwa namna wafanyabiashara wanavyoitolea mate gesi, tanzanite wameimaliza na sasa wanataka gesi tu.

Mengi kakomaa anataka Vitalu vya Gesi huku mwenzake Mkono ana Uchungu wa kuzikosa Tenda za Tanesco Hawa wote Usiku na mchana wanataka Mhongo ang'oke wapaze kupiga Dili zao si kweli kuwa wana Uchungu na Nchi hii Bali wana jali masilahi Yao Tu.
 
Huo ulikwisha tatuliwa na ndiyo maana wamelipwa. Na Jaji Utamwa alithibitisha kuwa mgogoro umekwisha kwa kupatiwa mkataba wa IPTL na TANESCO kuwa wameshafikia makubaliano nje ya mahakama kuhusu capacity charges.

Ulikuwa husikilizi?

Tatizo ni nani wa kuaminiwa? PCCB na CAG au Muhongo? Je ni TRA ana TANESCO waliosema sehemu ya hela ya escrow ilikuwa na VAT au Muhongo?
 
That is exactly what I keep on saying. Porojo zote hizi bungeni mwisho wake ni Serikali inatakiwa ijibu hoja ya msingi kutokana na facts za CAG na PCCB. Wahisani wanayo copy ya ripoti ya CAG. Hii ndiyo repercussion ya kutegemea misaada. And it looks like tax payers in Tanzania are so stupid to let the government spend their taxes kwenye rushwa na upuuzi mwingine na wao wapo tu wanashabikia mabonanza. We will never develop. Tutaendelea kuwa maskini mpaka the end of time tusipobadilika.
 
Ugumu gani? Ebu jiulize; hujui kwamba wabunge wengi ni ccm; pili wanakula kupitia chama chao. Ugumu upo sana tu; waoige kura alafu wakale wapi? Katiba ya chama nitakilinda na kukitetea chama change kwa kila khali
 
Jamani Watanzania kusoma hatujui hata picha hatuoni .huyu jamaa anatamka waziwazi kuwa leo ameagiza Tanesco kuwa wahakikishe umeme haukatwikatwi sababu yeye anatoa utetezi wake..hili tu ni tosha huyu jamaa ni muhujumu uchumi hata platform ya kujitete alitakiwa asipewe kabisa ,yaani swala la umeme kukatwa siyo hitilafu ni hujuma za makusudi kabisa .its only in Tanzania
na watakata umeme saa kumi trust me!
 
Na ndiyo hapo issue ilipo. Tatizo ni nani wa kuaminiwa? PCCB na CAG au Muhongo? Je ni TRA ana TANESCO waliosema sehemu ya hela ya escrow ilikuwa na VAT au Muhongo?

PCCB na CAG hawajaonesha wizi wala rushwa kwenye ripoti zao kwa waziri yeyote yule. Kama unayo unaweza kuweka hapa, labda hatukuiona.

TRA, IPTL na au TANESCO wanapaswa wakae na watatue hilo. Hilo si jambo kubwa sana kwani IPTL wameshasema watalipa madeni yote an TANESCO na Serikali bado wamezuwia zaidi ya 100 b ambazo zinaweza kulipiwa 30 B aliyosema Zitto na bado wakawa wanadaiwa zaidi ya 70 b.

Mhongo kaelezea vizuri sana na kwenye hili nnaamini Serikali ipo sahihi.
 
Kwa nn serkali ilitumia nguvu nyingi sana kujaribu kuizuia report ya pac isiwasilishwe kama utetezi wa muhongo ni wa kweli?

Je report ya cag aliyoi-quote sana muhongo ni ile ilyochakachuliwa?
 
Kamati ya Bunge ya PAC haikuwa na ujuzi wala umakini wa kuchunguza suala la Escrow. Na mbaya zaidi walifanya conclusion kwa baadhi ya mambo mazito bila kujiridhisha kuwa mahitimisho waliyofanya ni ya kweli au la. Mbaya zaidi wamechukua taarifa za mitaani na kuziweka kwenye ripoti bila ya kuzifuatilia kama zina ukweli au la. Hii imemfanya Prof. Muhongo kuwa na kazi rahisi kabisa ya kujibu hoja zao nyepesi ambazo hawakuzifanyika kazi sawasawa. Imefika wakati wabunge wakubali kuwa kazi za uchunguzi na ukaguzi ni za kitaalamu na wanahitaji kushirikisha wataalamu kwenye kamati zao wakati wakifanya uchunguzi.

Uchunguzi ulifanywa na CAG na PCCB ambao ni wataalamu.
 
Umeshawauliza tanesco kama hawajafanya withholding? Kumbuka kuna billion zaidi ya 100 wamezizuia Tanesco na au Serikali.

Unatetea mpaka unajikuta unapingana na unayemtetea.Muhongo kasema kama kuna kodi TRA wafuatilie PAP sio mambo ya wizara kujua kama kodi imelipwa au la...
Hili pekee linatosha kumtoa ofisini.
 
Na kama huoni umuhimu wa kufuatilia mauziano ya hisa kati ya watu binafsi, nini kinaipa serikali uhakika wa new owner kiasi cha kuidhinisha ownership transfer hadi kubariki malip ya mabilioni ya fedha?

Anasemaje huu ya procedure inayomdai kujiridhisha pasipo shaka kabla haja efffect changes kwamba ununuzi umefanyika na si magumashi?

Mhongo anatutania.

Na kama PAP anamiliki IPTL kimagumashi,wakija Starn Chart wenyewe na hisa zao,hiyo indemnity iliyotolewa na PAP wataitambua?
 
Tatizo ni nani wa kuaminiwa? PCCB na CAG au Muhongo? Je ni TRA ana TANESCO waliosema sehemu ya hela ya escrow ilikuwa na VAT au Muhongo?
Hayo ndio maswali ambayo Zitto na kamati yao ya PAC walitakiwa watusaidie sisi wananchi kwa kuyapatia majibu kwa ufasaha bila kupepesa macho.Na wangeweza kufanya hivyo iwapo tu wangefanya kazi yao kwa umahiri unaotakiwa. Ila wao walijielekeza kwenye kushughulikia watu kisiasa bila kukamilisha kazi waliyopewa kwanza.
 
Back
Top Bottom