Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)!

Mimi nadhani wewe hujui wajibu wako hivi nikuuliza priotize maslahi ya nchi na wananchi harafu chama utapangaje?
 
" ....Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM...." By Dr. Hamisi Kigwangalla.

Kwa hiyo hata kama ni kula rushwa ambayo huko CCM imetawala utaendelea kufanya hivyo hivyo simply kwa sababu uko CCM na ndiyo jambo linalokubaliwa? Dhamira yako iko wapi kwa yale ambayo yanaenda kinyume na maadili ya uongozi? Hutayasemea kwa sababu kuyasemea hakukubaliwi ndani ya CCM? sidhani kama huo ni uongozi badi ni umbumbumbu! Huko ni kuwa DODOKI kama Hayati Mwl. Nyerere alivyowahi kusema na watu wa namna hiyo ni wakuogopa kama UKOMA! Hawatufai na hawafi kuwa viongozi popote pale katika dunia hii!!
 
Hii ndio tabu ya wanacdm, akili yenu ni kutoa matusi,mtu amekuja na heshima zote halafu anakutana na wahuni, ndio maana wenye heshima zao wala hawana mpango wa kuja kujieleza humu. Mbona wana CCM wanaheshimu wabunge wenu? Jaribuni kujifunza kidogo
 
mkuu kwanza nikupongeze kwa kuja kuleta majawabu sawia!

Ingawa siwezi kuthubutu kukuita mnafiki kutokana na ukubwa wa neno hili kwa muumba, ila naona kama kuna sehemu sijakufahamu vyema kauli yako kwamba

"leo hii mimi niko chama kimoja tu, ccm, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya ccm",

wasiwasi wangu katika hili ni je ikiwa mambo hayo ambayo kimsingi yanakubaliwa na ccm yatakuwa yanaenda kinyume na matakwa ya wananchi itakuwaje hapo? Mfano tunajua kuwa uongozi ni dhamana na ubadhirifu ni kukosa unaminifu na ni dalili ya unafiki kwa kutenda kinyume na dhamana hapo inakuwaje kaka yangu hebu nijibu tafadhari?


" tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni mbunge kutokea ccm na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya ccm kwa hoja inayoletwa na mbunge wa kambi ya upinzani! Mbunge wa chama tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic "


lakini pia katika dhana hiyo hiyo ya kuungana na yatokanayo na chama chetu "ccm" na kutokubali hoja iliyotoka upande wa pili, napo ninaomba unipe ufafanuzi mzuri, naamini kabisa pamoja na sababu chafu na agenda zingine za vyama vyetu vya upinzani lakini bado kuna masuala yalio sahihi na yanayogusa maslah ya umma,

huenda hoja iliyoanzishwa kwa upande mmoja ikapelekea kuwapa ushindi wa kisiasa wapinzani lakini swali langu kwako mh. Ni upi msimamo wako pale hoja inapoletwa na wapinzani ikawa ina maslah makubwa kwa taifa lakini itakipunguzia nguvu chama chetu ccm, utaunga mkono hoja au kupinga? na kama ni lazima uitetee serikali yako huoni kama kwa hilo huwatendei haki wananchi?

Best
tume ya katiba

mkuu tatizo lako huwa unaona kama tunawaonea sana wabunge wenu tukisema ukweli hebu angalia akili kama hizi halafu huyu eeti ni dr.
Wengi niwanachama waccm ila ni aibu kubwa na tumechoka sana na chama hiki!
 
Ndugu zangu wanabodi,

Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Siyo kwamba nimekimbia JF, la hasha. Siwezi kukimbia na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Ni kwamba gadget yangu ninayotumia kwa mawasiliano ilipata mushkeri na nikawa nalazimika kutumia kompyuta na bahati mbaya sana kwa jinsi nilivyokuwa bize na ujenzi wa Taifa nilijikuta nakosa muda wa kukaa kuanza ku-surf. Nisamehewe kwa hilo.

Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.

Kuna uwezekano wa kuwa na tafsiri tofauti kutokana na pre-conceptions zetu vichwani, siwezi kulizuia hilo hata kidogo. Kwa kuwa ninakalia kiti cha uwakilishi, nina-feel ninawajibika kwenu kutoa maelezo ya msimamo wangu kwenye hili, na wala sintomumunya maneno.

Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo. Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa. Mhe. Zitto Kabwe (MB) alipokuwa akijumuisha hoja yake, alitaka serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa Wizara na Mashirika ya umma, na akasema kama serikali haikufanya hivyo kufikia J3 iliyofuata basi sisi (Bunge) tuna uwezo na WM na kwamba atapitisha karatasi ya kukusanyia saini 70 ili kukidhi matakwa ya kikanuni ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na WM; kwa tafsiri yangu ni kwamba Mhe. Mbunge alilenga kuweka presha kwa serikali, kuitaka iwajibike kwa kuwawajibisha mawaziri hao (watano) kama alivyowataja yeye. Kwanza mwanzoni nilielewa hivyo. Baadaye jinsi ilivyopokelewa na wadau mbalimbali nikaona kama hoja inahama sasa na kwamba si mawaziri hao watano wenye tuhuma mbalimbali, ni PM na kwa maana hiyo ni serikali yote Bungeni! Hili mimi siliungi mkono na silikubali. Nasema wazi hivyo kwa sababu, mimi nina imani na WM, nina imani na Rais - aliyemchagua WM, na nina imani na Mawaziri wengine wengi wazuri tu kwenye serikali hii, na msimamo wangu huu uko wazi sana tu.

Mbili, sioni sababu ya kuiingiza nchi kwenye wasiwasi wa kiutawala kiasi hiki. Na kwa kuwa wabunge wa CCM kwenye party caucus tulikuwa tayari tumeishaambiwa kwamba kuna mawaziri wameamua kujiuzulu wenyewe (tena siyo wale watano, ni wanane kabisa) kutokana na tuhuma hizo na presha kutoka kwa wabunge wa CCM na wengine, sikuona sababu ya mimi kusaini hoja ya Zitto (ambayo kikanuni ilikuwa imekosewa - kitendo kilichonidhihirishia wazi kwamba hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa WM bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita - na hii itaturudisha kule kule kwenye nilichokisema kule twitter kwamba hoja hii ni ......politically right but technically flawed!

Jamani, hoja ya kumuondoa WM madarakani siyo kitu kidogo, siyo kitu cha mchezo, ni lazima ujipange. Ukweli ni kwamba rafiki yangu Mhe. Zitto hakujipanga kuifanikisha (bila shaka yeye mwenyewe analielewa hili vizuri - he is smarter than this, I know him!)

Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.

Wakatabahu,
HK.

mh. mbunge umuhimu wa waziri mkuu ni uwajibikaji kwa wananchi, lakini kama anaona macho tuu kama mtazamaji hatufai hata kidogo pamoja na raisi wake. tulifikiri wabunge vijana kama wewe damu changa ungechukua maamuzi magumu kama mh. mbunge filikujombe wa ccm mwenzako. kumbe huna maamuzi, ujue mtaji wa sasa ni wananchi nasio chama. kumbatia tu chama hicho na matokeo utayaona. waziri mkuu gani hana maamuzi wala maagizo kama wenzake waliopita. na unasema serikali haijashindwa huku michango mingi kwa wananchi huku mawaziri wenu wanatesa pamoja nawe.
 
Umekuwa na majibu ya kudhani sana utetezi hauna Nguvu.
Pia sikuelewi unapochukua jukumu la kulinda masilahi ya Serikali yako wakati waliokuchagua waibiwa na unayemlinda asidhibiwe.
Je bora wananchi wafe kwa kukosa huduma wakati wewe undelea kuwalinda waharifu wa serikali yako?
Je unajua kwamba upo bungeni kuisimamia serikali?
Je kwa huo ujumbe uliotupata ndiyo muono wa serikali unayoitumikia?
Sina imani na uwakilishi wako kwa watu wa Nzega.wewe ni kati ya wachache munaotumikia kundi dogo la walafi Tanzania
Bora ungeomba radhi kuliko nadhani ulizo jaza kwenye utetezi wako
Naamini hautapona na dhoruba maana umejichafua mapema
 
Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo!
kwa hiyo wewe unaona ni bora uwaangushe wananchi waliokuchagua kuliko kuiangusha serikali fisadi? Yaani mwananchi amabaye ulipita ukimpa ahadi na matumaini makubwa leo unamgeuka na kumwambia eti chama kwanza? Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa! Haya- wananchi wa Kigwangalla mmesoma hivyo anayowatendea - chama ni bora kuliko nyinyi. Tusubiri uchaguzi ujao


Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority.
Kwa hiyo kwako wewe hata kama serikali imeamua kuwafisadi wananchi wake bado utaendelea kuitetea! Yaani huo mfumo wa westminster unakulazimisha utetee uovu na ufisadi wa serikali? Mbona huko Uingereza mfumo huo ulikoanzia ufisadi haulindwi? Acha kutudanganya bwana!

kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao.
Huko mnasema tu halafu hakuna hatua zinazochukuliwa, Kwa nini mnasemea gizani, mnahongana nini huko? Hata vitabu vitakatifu vinasema wazi kuwa matendo maovu hufanyika mafichoni!

Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.
Nakushukuru kwa kujiweka wazi, tumekuelewa sasa, tumeelewa nini unachokisimamia!
Wakatabahu,
HK.
Maoni yangu kwa kila comment ya 'dr.' nimewayeka kwenye red.
 
hi mada imeniharibia siku yangu kabisa.
bora jimbo angepewa selelii
kumbe hata ww chama kwanza wananchi baadae yawezekana
hata hospital unatanguliza hela kweza matibabu baadae
nafurahi kuwa wana Nzega wameshakuelewa na wameamka.
 
Duh.. hebu niangalie hoja zako..
Unasema hoja huikubali.. Kwa kuwa Serikali haijashindwa kazi.. Hapo hapo unasema unakerwa na baadhi ya watendaji wanaowaangusha watanzania.. ambao wanalindwa na Serikali hiyo ambayo wewe unadai haijashindwa kazi..! Kwani hizi kauli za kutaka kuwajibishwa kwa baadhi ya mawaziri zimeanza leo Mkuu..? Imefikia hapa ilipofikia kwa kuwa Serikali ambayo wewe unadai haijashindwa kazi, imeamua kwa makusudi kuwakumbatia hawa.. Na wenyewe wamesema kabisa hawako tayari kuachia madaraka..

Then unasema unaunga mkono hatua ya kuwatoa hawa.. Hii Mkuu wanaiita ni contradiction..! Japo unadai hukubaliani na njia inayotumika ku-pressurize uwajibikaji kwa kuwa inahusisha kupiga kura ya kutokuwa na imani na PM.. lakini unaelewa hii ndio njia pekee iliobakia kwa wabunge kuilazimisha Serikali ambayo sio sikivu kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa.. Na unajua anaewindwa wala sio PM..

Hili la Nchi kuingia katika wasiwasi mh.. Mkuu hapa umechemka.. Alipojiuzulu Lowassa Nchi iliingia kwenye hali kama hiyo ulioisema..? unadai Mawaziri walikubali kuachia ngazi.. mpaka leo ni mawaziri wangapi walioachia ngazi..? Na imeshapita wiki wakati PM aliahidi Jumatatu iliopita angetoa tamko..!

Ingekuwa vizuri ungeendelea kukaa kimya kuliko kuja na utetezi wenye upungufu mkubwa.. Sote tunaelewa mwisho wa siku kwenu CCM ndio kwanza na Taifa baadae.. Huna uzalendo wa kweli zaidi ya kuangalia maslahi yako binafci kwa manufaa yako na familia yako..

Ila ni vizuri ukianza kusoma alama za nyakati Mkuu..



 
Hivi kweli wewe una fikra huru??

Wewe inamaana hata ukiona nchi imetafunwa na nyie mchwa utakaa kimya kwa sababu Serikali ni ya chama chako??

Vipi kuhusu vile vimisemo vyenu vya 'Taifa mbele, Chama baadaye'??

Unaelewa maana ya concept ya 'Tanzania ilikuwepo kabla ya CCM'??

Nadhani ndio maana ulibebwa kwenye kura za maoni, hufai kuwa hata balozi wa nyumba kumi!!

Well said, Mkuu!!

Mnafiki sana huyu!! Anaaibisha wasomi, hasa sisi madaktari!!!

Kweli ndiyo maana alibebwa kwenye kura za maoni, walimjua kuwa boot-licker!!! Big shame on him!!!
 
Kwanini Hukujibu kule kwenye thread yenyewe?

Dr. Kupeng'e, unajua mtu yeyote mwenye akili timamu lazima atahoji swali kama hili lako. Lakini wenye timamu zao kichwani tulipoona tu ile thread nyingine namna ilivyoandikwa, tukajua mtu mzima ama kwa jina jingine au kw akumtuma mtu mwingine, ameamua kutafuta forum ya kuweka hoja zake ili naye aonekane kuwa yupo. Lakini kubwa zaidi akitaka kupeleka ujumbe kwa wakubwa zake kuwa yuko upande wao, wajue kuwa ni kijana wao na katika mabadiliko asisahaulike. Period. No more. Ujanja ujanja tu, kama walivyozoea wakubwa wao au watangulizi wao.
 
Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo.
huyu jamaa kumbe ni boya hivi..wewe mitembo na kobe wamesafirishwa watu wamejinunulia mijumba ya dola zaidi ya laki tano na bado wapo madarakani lakini wewe unakuaj kuongea upepo hapa.usiweke tumbo mbele ila kwa vile umeshasema kuwa hutaki tena kugombea ubunge sina shida na wewe kwani you have nothing to loose
 
Kama Kumuangusha Waziri Mkuu na serikali yote Bungeni na kukimaliza kisiasa CCM si kuyapokea mabadiliko, basi nimeshindwa. wamekosea mawaziri watano (or rather wanane) wewe utake kuiangusha serikali yote, lini tutafanya mambo ya maendeleo? Mimi sikubaliani na huo mtazamo, na kwa kuwa nimeuweka wazi sina unafiki ndani yake, so just take it or leave it!

Unavyozidi kujibu utumbo humu ndani unazidi kujidhalilisha
Bora kukaa kimya kuliko kuanika unafiki wako hapa
Huna lolote na bora umejipambanua mapema kuwa wewe ni wale wale ambao wako tayari kulamba viatu vya wakubwa ili upate kula yako
Na uko tayari hata kuuza utu wako na taaluma yako ili upate kula
 
Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! HUYU JAMAA NAMJUA ALIVYOO NA MOST OF HIS FAMILY MEMBERS NI WANAMA.T.A.T.IZO YA AKILI HATA YEYE SIMSHANGAI!!UKIMSIKILIZA BUNGENII FULL KUJICHANGAYA KTK HOJA ZAKE!! ONA HZO SENTES ZA KE ALIZOTOA!!! HAKUNA LOLOTE NI M.P. UMBA.V.U FURANI!! BLV ME OR NOT MAELEZO ALIYOTOA NI COMENTS ALIZOTOA MNAFIKI MWENZIO January!! ktk fcbk!! tunakusubiri nzega mwana hi .zaya mkbwa we !!UMEBEBWAA HUWEZ ONGEA LLOTE!! KURA ZA MAONI 1000!!! TUNAJUA UMEMUOGOPA HAWA GHAS!ALIVYOKUBEMENDA WAKATI WAMGOMO WA MA Dr hadi leo mkimya wote umerudi tumboni!! kukutoa shaka Tangaza kabsa kaam bibi KIDUDE kutogombea ubunge :frusty: :frusty:
 
Nadhanimimi nakuona bado hujaiva kisaisa na kwa sababu umeamua kufuata unazi wa ccm aukufuata mkumbo wa kichama pasipokutaika kuielewa hoja ya Zitto hilolimenisikitisha. Kwanza hoja hii ya kumtoa WM ilianzishwa na mbunge wa chademaTundu na si wabunge wa ccm. Wabunge wa ccm walikuwa wanalaumu zaidi na kuwaombamawaziri wajiuzulu. Lakini zitto kwa nafasi yake ya uenyekiti wa kamati akaamuakuiingiza hoja hiyo na kuisimamia. Hata hivyo alisema wazi kabisa kuwa wabungehawana uwezo wa kuwawajibisha mawaziri. Kwa maana hiyo hata kama wabungewangelipiga kelele kiasi gani isingesaidia bali ingebakia hadithi ya kelele zachura hazimzuii ng'ombe kunywa maji. Kwa hiyo kwa mamlaka ya kikatiba na kanuniza bunge, wabunge wanaweza kumwajibisha WM tu kwa kumpigia kura ya kutokuwa naimani naye, ili akijiuzuru na baraza la mawaziri lazima livunjwe na huo ndiomwanya wa Rais kuteua watu safi, kama anania ya kuwaondoa mawaziriwaliotuhumiwa kwa ufisadi. Huu ndio usahihi wa hoja ya Zitto nilivyomwelewa.
Pili nimeona umetaja kuwa mnafuata mfumo wa Westminster, mimi sielewi kamaunapata hata muda wa kusikiliza bunge la uingereza lilivyo (House of commons).Bunge la hapa halina kulindana kama ilivyo kwa wabunge wa CCM wanaopiga kelelepasipo kuchukua hatua. Hebu angalia historia ya wabunge na mawaziri wa serikaliya uingereza walivyojiuzuru na wengine kufungwa sababu ya udanganyifu wamasurufu (expenses), je kwetu licha ya ripoti za CAG kuonyesha ubadhirifu wakutisha kwenye halmashauri na wizara nani amewajibishwa. Hebu niambie wewembunge hii scandal ya wanyama zaidi ya 100 kuchukuliwa kupitia KIA kwa ndege yakijeshi/mfalme na kupelekwa uarabuni bila eti serikali kujua nanikawajibishwa!!!? Waziri wa utalii hadi leo anapeta na tena anadai anaundiwazengwe- hivi hakuna waliohusika kuwakamata wanyama hao? Hivi hao wanyamahawakupita kwenye mageti ya hifadhi na barabarani kwa askari polisi wabarabarani? Hivi hapo KIA hakuna mageti na waliingizwaje kwenye ndege? Eti nandege serikali haikuwa na taarifa nayo? Hao usalama wa taifa wako wapi? Afisamaliasiri wa uwanjani alikuwa wapi? Huu ndio ufisadi mnaoshindwa kuuchukuliahatua na kuendelea kuukumbatia ndani ya serikali ya ccm. Kweli ni Chama ChaMafisadi (CCM).
 
I hate ccm, especially hujalala wasomi waliomo wakisaliti elimu zao, shame on you
 
Back
Top Bottom