Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya Kigwangalla: Kwa Nini Sikusaini Hoja ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe (MB)!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by HKigwangalla, Apr 27, 2012.

 1. HKigwangalla

  HKigwangalla Verified User

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu wanabodi,

  Nimeamua kuja kujibu kama ambavyo mngependa nifanye. Siyo kwamba nimekimbia JF, la hasha. Siwezi kukimbia na wala sina sababu ya kufanya hivyo. Ni kwamba gadget yangu ninayotumia kwa mawasiliano ilipata mushkeri na nikawa nalazimika kutumia kompyuta na bahati mbaya sana kwa jinsi nilivyokuwa bize na ujenzi wa Taifa nilijikuta nakosa muda wa kukaa kuanza ku-surf. Nisamehewe kwa hilo.

  Mimi sijawahi kuwa mnafiki, at least kwa alama tatu za mnafiki kama tunavyofundishwa sisi waislamu. Kwa faida ya mjadala huu, niseme alama zenyewe. Moja ni kuwa akitoa ahadi hatekelezi. Mbili, ni akiaminiwa anahalifu na tatu, akizungumza husema uongo. Namshukuru Mungu sina hata moja ya alama hizi na hivyo kushindwa mtihani wa kuwa 'mnafiki'. Ungeniita mnafiki kama nisingekuwa tayari kutoa maelezo ya maamuzi yangu, ama kama ningewasaliti CCM na kupeleka siri za huku kule, ama kama ningeahidi kuunga mkono hoja hiyo kisha nikakimbia. Leo hii mimi niko chama kimoja tu, CCM, na nitafanya mambo yanayokubalika ndani ya CCM. Siku nikihamia CHADEMA/CUF/NCCR basi nitafanya ya huko bila kusaliti kule na kurudisha CCM ama kupeleka kokote kule kinyume na utaratibu. Huo ndiyo msimamo wa ukweli na siyo unafiki.

  Kuna uwezekano wa kuwa na tafsiri tofauti kutokana na pre-conceptions zetu vichwani, siwezi kulizuia hilo hata kidogo. Kwa kuwa ninakalia kiti cha uwakilishi, nina-feel ninawajibika kwenu kutoa maelezo ya msimamo wangu kwenye hili, na wala sintomumunya maneno.

  Kwanza, hoja yenyewe siikubali. Kwa sababu ninaamini serikali ya Chama Changu (CCM) haijashindwa kufanya kazi ya watanzania kiasi cha kung'olewa madarakani kwa namna hiyo. Pili, naamini na ninakubali, na kwa hakika ninakerwa na baadhi ya watu waliopewa dhamana za kuongoza baadhi ya ofisi nyeti za umma wametuangusha watanzania, na hivyo naunga mkono hoja ya kutaka kuwatoa hawa. Mhe. Zitto Kabwe (MB) alipokuwa akijumuisha hoja yake, alitaka serikali iwawajibishe baadhi ya mawaziri na watendaji wakuu wa Wizara na Mashirika ya umma, na akasema kama serikali haikufanya hivyo kufikia J3 iliyofuata basi sisi (Bunge) tuna uwezo na WM na kwamba atapitisha karatasi ya kukusanyia saini 70 ili kukidhi matakwa ya kikanuni ya kuwasilisha hoja ya kutokuwa na imani na WM; kwa tafsiri yangu ni kwamba Mhe. Mbunge alilenga kuweka presha kwa serikali, kuitaka iwajibike kwa kuwawajibisha mawaziri hao (watano) kama alivyowataja yeye. Kwanza mwanzoni nilielewa hivyo. Baadaye jinsi ilivyopokelewa na wadau mbalimbali nikaona kama hoja inahama sasa na kwamba si mawaziri hao watano wenye tuhuma mbalimbali, ni PM na kwa maana hiyo ni serikali yote Bungeni! Hili mimi siliungi mkono na silikubali. Nasema wazi hivyo kwa sababu, mimi nina imani na WM, nina imani na Rais - aliyemchagua WM, na nina imani na Mawaziri wengine wengi wazuri tu kwenye serikali hii, na msimamo wangu huu uko wazi sana tu.

  Mbili, sioni sababu ya kuiingiza nchi kwenye wasiwasi wa kiutawala kiasi hiki. Na kwa kuwa wabunge wa CCM kwenye party caucus tulikuwa tayari tumeishaambiwa kwamba kuna mawaziri wameamua kujiuzulu wenyewe (tena siyo wale watano, ni wanane kabisa) kutokana na tuhuma hizo na presha kutoka kwa wabunge wa CCM na wengine, sikuona sababu ya mimi kusaini hoja ya Zitto (ambayo kikanuni ilikuwa imekosewa - kitendo kilichonidhihirishia wazi kwamba hakuwa na u-seriousness wa kutaka kweli kumuondoa WM bali ni baadhi ya mawaziri, sema alichomeka tu hiyo kauli ili kutia presha zaidi!). Zaidi ya hapo, ninaamini hoja hiyo ni nzito na kimsingi, kwa sasa, imegeuka kuwa ni mchezo wa kisiasa na media na haitofika popote! Kama Mhe. Mbunge Zitto alikuwa na nia ya dhati ya kumuondoa WM asingekurupuka kiasi kile, angewashirikisha watu wengi zaidi, hususani wabunge wa CCM, na kimkakati zaidi angewapa wabunge wa CCM walioibua hoja hizo za kuwataka mawaziri wang'olewe na hapo angefanikisha malengo ya kumuondoa WM na serikali yake Bungeni. Kwa namna ilivyo hawezi kupata support ya wabunge wa CCM na kwa kuwa sisi ndiyo majority, hoja hiyo haitopita - na hii itaturudisha kule kule kwenye nilichokisema kule twitter kwamba hoja hii ni ......politically right but technically flawed!

  Jamani, hoja ya kumuondoa WM madarakani siyo kitu kidogo, siyo kitu cha mchezo, ni lazima ujipange. Ukweli ni kwamba rafiki yangu Mhe. Zitto hakujipanga kuifanikisha (bila shaka yeye mwenyewe analielewa hili vizuri - he is smarter than this, I know him!)

  Tatu, msisahau kitu kimoja cha muhimu kabisa. Kwamba, mimi ni Mbunge kutokea CCM na kama walivyo wengi wenzangu hatukusaini kwa sababu hatuwezi kuiangusha serikali ya CCM kwa hoja inayoletwa na Mbunge wa Kambi ya Upinzani! Mbunge wa Chama Tawala kuamua kuiangusha serikali ya chama chako ni sawa na kuamua kukata tawi la mti uliokalia, kwa vyovyote vile utaanguka nalo! Simple logic! Mfumo wa Bunge letu ni wa Westminster, na hivyo kuna kambi ya Upinzani (yenye interest ya kutaka kuiangusha serikali inayotawala) na Kambi ya Serikali (ambayo ina interest ya kutaka kuilinda serikali yake). Kwa maana hiyo sisi wabunge wa CCM tuna jukumu la kuilinda Serikali inayopatikana kutokana na sisi kuwa majority. Serikali ni lazima i-enjoy majority status ndani ya Bunge ili nchi itawalike kwa amani na utulivu, japokuwa haimaanishi kuruhusu ubadhirifu na ndiyo maana kwenye Party Caucus wabunge wana nguvu na fursa ya kusema chochote dhidi ya serikali ya Chama Chao. Kuna wengine wanataka Bunge liwe Bunge huru (ama 'An Indipendent Power House') disregarding political opinions/inclinations/affiliations na serikali iwe serikali, hii haiwezekani kwa katiba tuliyonayo leo. Tubadilishieni kwanza katiba na mfumo wa kufanya kazi ndipo mtutake tufanye hayo mnayoyatamani.

  Nadhani nimejiweka wazi bila unafiki, sasa tujadili kwa hoja siyo kwa hisia na matusi kama hatukwenda shule vile.

  Wakatabahu,
  HK.
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kwanini Hukujibu kule kwenye thread yenyewe?
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Dr. Hamisi Kigwangalla, MD, MPH, MBA.Duh wasomi wa Tanzania hovyo.
   
 4. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Hivi kweli wewe una fikra huru??

  Wewe inamaana hata ukiona nchi imetafunwa na nyie mchwa utakaa kimya kwa sababu Serikali ni ya chama chako??

  Vipi kuhusu vile vimisemo vyenu vya 'Taifa mbele, Chama baadaye'??

  Unaelewa maana ya concept ya 'Tanzania ilikuwepo kabla ya CCM'??

  Nadhani ndio maana ulibebwa kwenye kura za maoni, hufai kuwa hata balozi wa nyumba kumi!!
   
 5. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapo kwenye REd HUU ndo unafiki wenyewe

  Sisi tunasafisha chama na nyie mnaturudisha nyuma

  Shame on you
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Saidi Bagaile bwana unanifurahisha sana...yaani wewe
  1. vyeti umefoji
  2. ubunge ulishindwa ukapewa tu
  3. ukatishwa wakati wa mgomo wa madaktari ukanywea kama changudoa wa kona baa wamekamatwa na polisi
  4. bungeni ulikaa kimya huna la maana ulilochangia
  wewe kaa kimya huna unalolijua zaidi ya kuwa SHABIKI asiye na msimamo
   
 7. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  We jamaa ovyo kabisa
  Huu utetezi wako haujakaa sawa.
  Naomba hata rais asikuteue kuwa waziri umesha onyesha wazi wazi huwezi kazi na huwezi tetea wanyonge.
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  nimekuelewa mkuu unamaanisha ccm kwanza na nchi baadaye sawa kabisa dr na waziri mtarajiwa wa tanzania
   
 9. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Ngongo hli jamaa ni zero kabisa..

  Vijana kama hawa wapelekwe kwenye zile kambi za kulelea wazee...

  Kilaza mkuu..
   
 10. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,972
  Likes Received: 20,334
  Trophy Points: 280
  Hukuweza kusaini karatasi ya Zitto kwa sababu ni 'sawa na kukata mti uliokalia'. kwa hapa ndugu nimekuelewa. Hofu ni haki ya kila mmoja na hasa linapokuja suala la kuchagua. Ulikuwa na hofu na huoni maisha nje ya baraza hili na serikali hii na kwa maana hiyo hata kelele na misimamo yako ya kutetea wananchi wa Nzega kupata faida na utajiri unaowazunguka (rejea msimamamo wako kwenye Resolute co.) ilikuwa ni kuzuga tu!

  Kazi njema bwana HK, na ukweli ni kuwa pamoja na kuwa umeingia ndani, bado tunaona umekanyaga kapeti letu na viatu vyako vichafu'
   
 11. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Zitto umeambiwa ulikurupuka na mpotoshaji, tafadhali njoo kamanda
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kwa mara ya kwanza toka nimekufahamu umeongea point!
  PAMOJA SANA NDUGU!
   
 13. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nadhani mkuu ni kujipigia upatu wa kutaka kuteuliwa na rais kwenye baraza jipya la mawaziri hongera kwa unafiki wako na uroho wako wa kugombea nafasi.Shetani akutangulie.
   
 14. kanga

  kanga JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 1,011
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Eti huyo naye anapoteza muda kuandika nonsense namna hii.Dawa yako ni Hawa Ghasia tu
   
 15. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ebu tuondolee upu.pu hapa,wewe ni mnafiki namba moja,wizara zote zimeoza mawaziri wote ni wezi na wewe ni mchumia tumbo,dawa yako ni 2015 sidhani kama utarudi mjengoni kwa kuendekeza kukumbatia wala rushwa na mafisadi wananchi lazima wakuadhibu tena kipigo kitakatifu we subiri dawa yenu ni kwenye kura tu.
   
 16. T

  Tajiri Mtoto Senior Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: Feb 12, 2009
  Messages: 131
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Kuogopa kukata tawi mlilokalia ndicho kitakachowaponza..... Mark my words. TUNANG'OA MTI MZIMA!
   
 17. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #17
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,381
  Likes Received: 407
  Trophy Points: 180
  kama unakataa unafiki basi wewe umekosa uzalendo. Nini cha muhimu, chama ama taifa? Kwa mtazamo wako zitto na wengine wanafanya tu kuiangusha serikali ya ccm na sio kutetea maslahi ya nchi? Hapa umekengeuka. Na jambo jingine walio saini fomu ya zitto hawakuwa wanalenga kuiondoa ccm madarakani; la hasha, walikuwa wanawasaidia ccm wajipange upya kwa manufaa ya wananchi.

  Lugha kwamba suala hili linaenda kupelekwa kwa wananchi maana yake ni kuwa maslahi ya wananchi kwanza, vyama baadaye.

  Doctor endelea kulinda chama chako na historia itakutambua hivyo.
   
 18. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  hapo redi tu nimepata kiu ghafla
  shikamoo muheshimiwa
   
 19. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Dr. Kupeng'e
  Msidhani hapo mna mwanachama ni kama msukule tu...

  Watu wengine ndio wanafikiri badala yake...

  Ninahisi na kale kakampuni kake kalikula hela za stimulus package...

  He can't think out of the box..
   
 20. g

  geophysics JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  NA HII PIA......Dr. Hamisi Kigwangalla, MD, MPH, MBA
  Mabadiliko ya kweli yataletwa na sisi...!.......
  Mabadiliko ya kweli yataletwa na ninyi......ULAAANIWE TENA KAMA WEWE NI MBUNGE WA CCM USHINDWE.
   
Loading...