Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
NImesoma kwenye gazeti la Mwananchi na kushitushwa sana na majibu ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, DR Leonard Akwilapo, kwa mwandishi wa habari wa Mwananchi pale alipoomba apewe ufafanuzi kuhusu matumizi ya wimbo na bendera ya Taifa. Angalia hapa chini taarifa kutoka Mwananchi;
Sasa hebu niambieni wana JF na jamii kwa ujumla, hivi haya ni majibu ya mtu anayetakiwa kuwa na busara kwa kiwango cha PhD na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu? Je tunahitaji kumwelimisha Dr. Akwilapo kazi ya vyombo vya habari hapa nchini ni nini, kwamba ni pamoja na kusaidia kufikisha ujumbe wa serikali kwa wananchi? Sasa kama mwandishi wa habari anaomba ufafanuzi ili asaidie kufikisha ujumbe kw wananchi, kwa nini Katibu Mkuu ajbu kwa kiburi namna hii?
Nadhani Dr. Akwilapo anahitaji kukumbushwa kwamba yupo katika nafasi kwa kusudi la kuhudumia wananchi, na wananchi hao ni pamoja na waandishi wa habari.