Majibu ya Dr Slaa kwa Sitta ni haya hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Majibu ya Dr Slaa kwa Sitta ni haya hapa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Karikenye, Aug 31, 2012.

 1. Karikenye

  Karikenye JF-Expert Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [FONT=&amp]SIKU moja baada ya waziri wa Afrika Mashariki na mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki Samwel Sitta kumrushia kombora mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe kuwa ,katibu mkuu wa Chadema Dkt Willbroad Slaa aibua tuhuma nzito dhidi ya waziri Sitta amwita msaliti .[/FONT]

  [FONT=&amp]Dkt Slaa amedai kuwa waziri Sitta ndie alikuwa katika makubaliano ya kuja kugombea uspika kupitia Chadema ila alisaliti pamoja na kukubaliana vizuri kuwa angekihama chama chake CCM.[/FONT]

  [FONT=&amp]Dkt Slaa alitoa tuhuma hizo leo mjini Iringa alipozungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya M.R alisema ilikuwa Mei mwaka 2010, Sitta ambaye hivi sasa ni Waziri wa Afrika Mashariki alipokutana na viongozi wa Chadema na kuonesha dhamira ya kujitoa CCM na kujiunga na chama chao ila alionyesha usaliti wa hali ya juu.[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema kuwa katika mazungumzo hayo yaliyoendelea kufanywa katika kipindi chote cha bunge la bajeti lililokuwa la mwisho kabla ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, Dk Slaa alisema katika masharti yake ya kujiunga na Chadema, Sitta ambaye kwa wakati huo alikuwa Spika, alitaka apewe nafasi ya kuwania urais kupitia chama hicho na vikao vilikuwa vikifanyika ofisini kwake Dodoma.[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema ameamua kutoa siri hiyo baada ya kiongozi huyo (Sitta) kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari juzi akidai kwamba Dk Slaa ni mtu pekee ndani ya Chadema ambaye ni tishio kwa urais katika uchaguzi ujao, huku akimponda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kwamba ni mchezesha disco.[/FONT]

  [FONT=&amp]Hata hivyo alisdai kushangazwa na waziri Sitta kuanza kuzungumzia mambo ya watu badala ya kujibu hoja na kuwa Chadema haipendi kuzungumza habari za watu, inazunguma maendeleo. Kwa muda mrefu tumemuhifadhi Sitta lakini baada ya kupeleka mashambulizi sehemu isiyohusika sasa tunampiga ngumi za tumbo na uso[/FONT]

  [FONT=&amp]Dkt Slaa alisema kuwa wakati akitaka aandaliwe mazingira ya kujiunga na Chadema na kupewa nafasi ya kuwania urais, Sitta alidai ana kundi la wabunge zaidi ya 55 waadilifu kutoka katika chama hicho ambao angetoka nao pamoja CCM na kuhamia Chadema kabla ya bunge kuvunjwa.[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema kwa kuwa Chadema haina ubinafsi, ilihadi kuyafanyia kazi maombi yake ya kuwania urais kwa uzito mkubwa hata hivyo katika mazingira ya kushangaza aliwatelekeza.[/FONT]

  [FONT=&amp]Dk Slaa alisema Sitta ambaye uzoefu wake katika siasa na umakini wake katika kushughulikia maendeleo ya nchi umeanza kuwatia shaka watanzania, alisahau jinsi alivyowatelekeza kabla ya Uchaguzi Mkuu na baada ya uchaguzi huo akaja na hoja mpya kitaka Chadema wampe nafasi ya kuwania uspika kwa kile alichodai kuwepo kwa mizengwe ndani ya CCM.[/FONT]

  [FONT=&amp]Katika mazingira ya kushangaza badala ya kufikia uamuzi wake wa kuhamia Chadema kama dhamira yake ilivyomtuma, Sitta aliwatelekeza tena akidai kwamba atajiunga na chama hicho mpaka pale atakapokwenda jimboni kwake Urambo na kutangaza rasmi kujiondoa CCM.[/FONT]
  [FONT=&amp]Alisema kiongozi huyo aliyekuwa akitaka msaada wa viongozi wa Chadema ili afanikiwe kujiunga na chama hicho na hatimaye kupewa nafasi ya kuwania nyadhifa alizokuwa akitaka ameanza kuwatusi hadharani viongozi hao akiwemo Menyekiti wake Mbowe.[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema kauli inayotolewa na Sitta kwamba Mbowe ni mchezesha disco inadhihirisha jinsi asivyo makini jambo linalowafanya waanze kuitilia shaka elimu na uzoefu alionao katika kuendesha shughuli za serikali.[/FONT]

  [FONT=&amp]"Sita anataka kutuambia kwamba watu wanaocheza disco wakiwemo mawaziri wengi tu wanaokutwa kwenye kumbi za burudani wanatenda dhambi na ni uhalifu kufanya hivyo?," alisema.[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema kama biashara hiyo ya Mbowe inafanywa kinyume na sheria za nchi, serikali inasubiri nini kufuta leseni yake.[/FONT]
  [FONT=&amp]Kuhusu uongozi na namna ya kupata viongozi ndani ya chama hicho, Dk Slaa alisema sio kazi ya Sitta akuwapangia utaratibu.[/FONT]
  [FONT=&amp]"Sitta hajui kwamba duniani hakuna chuo cha kusomea uwaziri, ukatibu mkuu, na hajui kwamba Mwalimu Julius Nyerere hakuwa na uzoefu wakati akipewa madaraka ya kuongoza taifa hili na kwamba hata wasaidizi wake nao walipata uzoefu baada ya kupata madaraka," alisema.[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema Sitta ni kiongozi mnafiki na atakumbukwa zaidi alipokuwa Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwasababu kuna hoja mbalimbali zilizowasilishwa na wabunge wa upinzani kuhusu ufisadi alizizima.[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema kuzimwa kwa hoja hizo ikiwemo ya Mkataba uliogubikwa na utata wa Buzwagi, unadhihirisha jinsi naye alivyotumia madaraka yake vibaya kwa kujenga ofisi ndogo ya Spika ambayo yeye aliita ya mbunge jimbo kwake Urambo.[/FONT]

  [FONT=&amp]Alisema wakati serikali imeridhia ofisi za wabunge zijengwe kwa kiasi cha fedha kisichozidi Sh Milioni 40 kwa kuzingatia upatikanaji wa fedha, ofisi hiyo ya Urambo ilijengwa kwa Sh Milioni 350.[/FONT]

  [FONT=&amp]"Kauli zinazotolewa na Sitta kuhusu chama chetu zinadhihirisha jinsi alivyomnafiki na asivyofaa jambo lililosababisha hata CCM wamemnyime nafasi ya kuwania kugombea kwa mara nyingone tena nafasi ya Uspika," alisema.[/FONT]

  [FONT=&amp]Dk Slaa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wako mkoani hapa, wakisubiri waanza mikutano yao ya vugugugu la mabadiliko walilolipa jina la M4C baada ya kuzuiwa na jeshi la Polisi kufanya mikutano yao katika kipindi chote cha sensa.[/FONT]

  [FONT=&amp] Wakati huo huo Dkt Slaa ameshindwa kutolea ufafanuzi juu ya kiasi cha fedha walizotenga kwa ajili ya mikutano yao ya M4C inayoendelea hapa nchi huku akiishia kudai kuwa fedha zinazotumika ni fedha zinazotokana na ruzuku ya serikali na michango ya wananchi bila kutaja kiasi hicho cha fedha.[/FONT]
   
 2. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Habari imejitahidi kuwa 'objective' japo sio 'analytical'
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  SITA ni mnafiki fulani,kwani mambo yake huzungumzia makanisani tuu!
   
 4. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Sitta ni kama wale dada zetu wa K'ndoni, hana choice, yeyote atakayekuja almradi tu amwakikishie nafasi fulani yeye twende! Kaanza CCJ na sasa CDM! Duh! Kweli Physically yupo CCM, Spiritually bado anatafuta pa kutua.
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 760
  Trophy Points: 280
  Slaa hoja hujibiwa kwa hoja sio wehu.
   
 6. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  na hapo kwenye gharama zinazotumika kwenye m4c zingewekwa wazi. naamini kuwa si jukumu la Dr. Slaa ila mhusika anapaswa aweke wazi. ni lazima kutenda differently rather than different
   
 7. Daniel Anderson

  Daniel Anderson JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 879
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ulichojibu wewe ndo wehu.
   
 8. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  JK kweli kiungo mchezeshaji, anawavuruga atakavyo leo wanatajana,walianza wale wa CCJ.
   
 9. s

  slufay JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,372
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pesa za cdm eti zinatoka kwa kamerun,italia,na ujerumani sijui n kweli toeni kiasi ili tujue
   
 10. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kweli siasa za ccm ni ngumu...hivi haiwezekani kutangaza utekelezaji wa ilani ya chama bila kuwataja CHADEMA? Ona sasa anavyowekwa mtupu. Huyu mzee anajulikana kwa UNAFIKI hata ndani ya chama na amechangia sana kupelekea utendaji dhaifu wa serikali ya J.K na asidhani hajulikani kwa hilo.

  Anajifanya anaijua sana nchi hii,kumbe ****** hakukosea kumwandama uspika...kama kungekuwa na tuzo ya busara ndani ya ccm bila shaka angeipata Prof. Mark Mwandosya pekee kwa angalau hakurupuki kama hawa wengine...Najua yatakupata maono haya Mzee Sitta...ukweli ni kwamba hufikiri kabla ya kunena na uachane na CHADEMA, endelea kuozea magambani...kwani hujui mabadiliko yanaletwa na wachache?...

  Ni wanasiasa gani waliokuwa maarufu sana zaidi ya Nyerere na kundi dogo kuliko CHADEMA then,wakafanikiwa kuweka msingi mzuri mnaobomoa ninyi?
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Dr.Slaa, acha uongo bana ulikuwa wapi kusema hayo yetu, wewe ni mgombea urais wa Chadema unataka kutuambia ungekubali Sitta awe juu yako.
   
 12. t

  thatha JF-Expert Member

  #12
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Slaa anazidi kudhihirisha kuwa anazeeka vibaya
   
 13. j

  j joni Member

  #13
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Dr. Slaa kamwe hajataka wala kuomba kugombea uraisi. aliombwa na Chama chake.
   
 14. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  Objective? Objectivity here?? I doubt!
   
 15. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 864
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Hope u gote the sms! Ndo CCM yenu hiyo. CCM ni tumbo kwanza, Waaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
 16. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 864
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Ulitaka alopoke kama mnavyolopoka nyinyi na akina Kova, Sitta, n.k! CCM ni tumbooo kwanza, Waaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!
   
 17. mapanga3

  mapanga3 JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 659
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 180
  Kazi kweli kweli
   
 18. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,695
  Likes Received: 428
  Trophy Points: 180
  Duh..kuanzia sasa naanza kumweka Sita kwenye Microscope yangu ya siasa..Ila naona kama amejaa unafiki sana..kwake yeye anataka madaraka zaidi na wala sio maendeleo ya nchi!!
   
 19. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #19
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Dr Slaa, kama Prof Lipumba ni wagombea urais wa kudumu.
   
 20. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #20
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Kama kuna watu wengine wana nia ya kuhamia chama chako mheshimiwa Dr. unawatia wasiwasi wa kuja kuwaanika mbele ya safari kama unavyofanya kwa Sitta.
  Huoni ya kuwa unaweza kupoteza sifa ya chama?
   
Loading...