Majibu kwa Nape, Ridhiwan Kikwete na wengine kuhusu elimu yangu na niliposoma

Unaelewa maana ya tuhuma au huelewi?! Mie nimesema amedanganya au nimesema anatuhumiwa kudanganya?! By the way, kwenye maelezo yake mwenye si amesema amesoma chuo kikuu miaka mitatu!!! We unafikiri maana yake hapo ni nini kama sio kuwadanganya waiofahamu? We unafikiri mtu aliyeishia elimu ya chini akaja kumsikia Mnyika anasema amesoma chuo kikuu miaka 3, unatarajia ataelewa nini?
Mia ya Nape na Ridhiwani ni kututoa kwenye matatizo yaliyosababishwa na utawala mbovu wa baba yake maisha bora kwa kila mtanzania imekuwa ni ndoto
ameingiza nchi kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe
Ametumia pato la taifa kwenda kubembea jamaica
ameruhusu rafiki zake waarabu na Katibu wake mkuu kuvuna wanyama wetu kwa aslimia 60
Ameefirisi misitu kwa silimia 80 mpaka misitu kama sao hill imebaki historia
Anavuna madini ameruhusu mpaka uranium ivunwe wakati nchi haina uwezo kujikinga na madhara yake
asilimia 94.5 wanafunzi wa sekondari wamefeli
ameshindwa kutatua janga la njaa wananchi wanakufa vijijini
ameruhusu mauaji ya wana dini wote waislamu kwa wakristo
sasa elimu ya Mnyika itajibu haya au munatutoa kwenye mjadala wa kitaifa na siku zote munafanya hivyo tunawajua nyie
 
Aache kutumia hadaa za kisiasa! Aseme tu ana elimu ya kidato cha sita, ataeleweka! Sasa stori ndeeeeeeefu lakini unaishia kusema "nimesoma chuo kikuu miaka mitatu, ambapo kwa baadhi ya vyuo vikuu duniani wanatoa Associate Degree!" Kama sio hadaa ni nini hii?!
Kwani uongo mfumo wa kimarekani wana associate degree tena mtu anakuwa college yaani wewe kwa akili yako Mnyika kwa pass alizopata toka darasa la saba unataka aone aibu ndio maana tunasema vichwa vyenu vimejaa sisimizi kwa sababu munataka kutulazimisha tuamini kwamba kuna mahala alijikwenza kwa crendentials asizokuwa nazo
 
Kamanda Mnyika ww ni mkali, endelea na moyo huo, mimi ninakubali sana ujengaji wako hoja, maana hauropoki kama hao akina Nape na mwenzake Riz last.
 
Mnyika ametumia porojo kukimbia kutoa taarifa zifuatazo kwa makusudi:
1. Matokeo yake ya A level hajayataja. Ya o level ametaja m¨paka idadi ya As alizopata, alipofika A level ameweka porojo. Ukweli ni kwamba A level alipata div 3.

2. Chuo hajamaliza. Kuhudhuria chuo si kuwa msomi wa chuo. Kusoma chuo ni kukamilisha mahitaji ya mitihani ya kozi yako ili uthibitishe umepata taaluma iliyokusudiwa. He is a collage drop out.

3. Hakuwa na sifa za kuchaguliwa kwenye program ya full time, hivyo akaingia program ya wazee ya jioni. Hili hajalisema kwa makusudi.

4. Baada ya kushindwa Ubunge mwaka 2005 alikuwa na miaka mitano mpaka 2010. Muda wote huu ameshindwa kumalizia kozi ya BBA!!!

5. Tangu aliposhindwa shule mpaka sasa ni miaka nane (8), bado ameshindwa kumalizia shule.

6. Sasa hivi ameenroll kwenye chuo fulani, ambacho katika majibu yake haya hajakizungumzia. Sababu ya kutokukizungumzia anajua yeye. Hata hivyo tangu ameenroll mpaka sasa hata module moja hajaweza kumaliza!!!

Jiulize kama mtoto wako akiamua kuacha shule na elimu ya form six ili ajikite kwenye siasa utamruhusu?
Ina maana gani kuacha shule kwa sababu ya siasa halafu unachoishia kufanya ni kulalamika kuwa CCM imeshindwa kutekeleza ahadi uloizotoa wewe kwa watu wako? as if CCM ilikwambia ukatoe hizo ahadi.
 
Thomas A.Edson had only three months of formal education during his entire life. Yet he did not lack education, nor did he die poor. Henry Ford had less than a sixth grade schooling, but he managed to do pretty well by himself financially.

As knowledge is acquired, it must be organized and put into use, for a definite purpose, through practical plans. Knowledge has no value except that which can be gained from its application toward some worthy end. This is one reason why a college degree in itself is not valued more highly. It often represents nothing but miscellaneous knowledge. Those who usually make the mistake of believing that the "knowledge-acquiring" period ends when one finishes school. The truth is that formal education does but little more than to put one in the way of learning how to acquire practical knowledge (Napoleon Hill- Think & Grow Rich!) pg 79. Hebu Nape na Riz acha hizo, matumizi ya elimu Nape ni kupiga poroja zisizoliletea taifa tija.
 
Mnyika ametumia porojo kukimbia kutoa taarifa zifuatazo kwa makusudi:
1. Matokeo yake ya A level hajayataja. Ya o level ametaja m¨paka idadi ya As alizopata, alipofika A level ameweka porojo. Ukweli ni kwamba A level alipata div 3.

2. Chuo hajamaliza. Kuhudhuria chuo si kuwa msomi wa chuo. Kusoma chuo ni kukamilisha mahitaji ya mitihani ya kozi yako ili uthibitishe umepata taaluma iliyokusudiwa. He is a collage drop out.

3. Hakuwa na sifa za kuchaguliwa kwenye program ya full time, hivyo akaingia program ya wazee ya jioni. Hili hajalisema kwa makusudi.

4. Baada ya kushindwa Ubunge mwaka 2005 alikuwa na miaka mitano mpaka 2010. Muda wote huu ameshindwa kumalizia kozi ya BBA!!!

5. Tangu aliposhindwa shule mpaka sasa ni miaka nane (8), bado ameshindwa kumalizia shule.

6. Sasa hivi ameenroll kwenye chuo fulani, ambacho katika majibu yake haya hajakizungumzia. Sababu ya kutokukizungumzia anajua yeye. Hata hivyo tangu ameenroll mpaka sasa hata module moja hajaweza kumaliza!!!

Jiulize kama mtoto wako akiamua kuacha shule na elimu ya form six ili ajikite kwenye siasa utamruhusu?
Ina maana gani kuacha shule kwa sababu ya siasa halafu unachoishia kufanya ni kulalamika kuwa CCM imeshindwa kutekeleza ahadi uloizotoa wewe kwa watu wako? as if CCM ilikwambia ukatoe hizo ahadi.

Mnyika you are so smart brother wewe huwezi kujibizana na vilaza kama Nape na Ridhiwan mdogo wake kapata Mwanaasha kapata ziro juzi tu au amesahau? piga kazi akili yako ni kubwa mno na elimu sio vyeti elimu ni yale unayoyaonesha pale bungeni mpaka vilaza wote wa ccm wanachanganyikiwa.
 
Hizi kauli za kusema elimu sio vyeti halafu mnashangaa kwanini wanafunzi hawafaulu. Its simple, kwa sababu jamii haiheshimu elimu, inaheshimu longolongo na porojo zinazopigwa bungeni. Kwanini mwanafunzi akeshe akisoma wakati anajua kuwa akipiga domo tu inatosha???
 
hadaiwi hata senti na serikali hii ya CCM amesoma kwa jasho lake na wazazi wake. swali pale TAMBAZA ulikuwa ukilipa ada tsh ngapi?
 
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.

Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

Kwa mara nyingine tena zinafanyika jitihada za kuhamisha wananchi kwenye mjadala kwa kumshambulia mtoa hoja badala ya hoja, sasa ili turejee kwenye mijadala ya msingi ni muhimu niweke kumbukumbu sawa kuhusu masuala kadhaa kama yalivyoombwa.

Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam).

Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne; nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa.

Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tambaza kwa sababu nilitaka kusoma huku nikiendelea na harakati ambazo nilizianza kabla.

Hapa ndio ilikuwa chanzo cha mimi kuingia kwenye kazi ya kuhamasisha mabadiliko kwenye mimbari nje ya utumishi wa madhabahuni. Tukio lililobadili mwelekeo wa maisha yangu, mwaka 1998 nikiwa kidato cha nne; nimesoma na tumeanza mitihani tukatangaziwa kwamba mitahani yote imefutwa baada ya kuvujishwa.Tukarudishwa nyumbani kipindi hicho nikaenda kwenye mafungo kujitafakari kwenye mkoa mmoja nikarejea Dar es Salaam nikakutana na wanaharakati kadhaa wa asasi zisizo za kiserikali; maelezo kuhusu ufisadi yalinifanya nione nina wajibu kwa nchi yangu, nikarejea Seminarini kufanya mitihani nikiwa na fikra tofauti.

Matokeo yakatoka nimefanya vizuri, kwa mifumo yetu mibovu ya wakati huo kwa mara ya pili tena Serikali hii inayoongozwa na CCM haikutambua vipaji na nikapaswa niendelee kujilipia ada mwenyewe kama ilivyokuwa kwa ngazi nyingine za elimu zilizotangulia; hapa nikakata shauri kwamba nitatumia uwezo na uadilifu wote ambao Mwenyezi Mungu amenijalia kuwezesha mabadiliko katika taifa letu.

Nikaamua kuacha kwenda kwenye shule za bweni mikoani na kubaki Dar es salaam nisome Tambaza huku nikiendelea na kazi za harakati; wakati huo nikihamasisha masuala ya ukombozi wa vijana nchini. Pamoja na kusoma kutwa huku nikifanya kazi nilipata daraja la pili katika kidato cha sita.

Taasisi nilizoanzisha au nilizoongoza katika kipindi hicho na kazi nilizofanya sio siri na zinapaswa kujieleza zenyewe kwa matendo badala ya maneno.
Katika kipindi hicho, wakati huo kukiwa hakuna Mfuko wa Elimu wala Bodi ya Mikopo nikashiriki katika ushawishi wa mabadiliko ya kimfumo; nilikwenda Dodoma, tukakutana na wabunge na mawaziri nikawasilisha mada “Towards a more functional education in Tanzania”, wakati huo nikiwa mwanafunzi wa Sekondari.

Kati ya wabunge waliosikiliza mada niliyoiwaisilisha wakati huo sasa ni Rais Jakaya Kikwete ( Ridhwan ukiwa nyumbani unaweza kumwuliza maoni yake aliyotoa siku hiyo kuhusu ugharamiaji wa elimu na suala la mauaji ya mwanafunzi wa Iyunga Michael Sikupya). Nilipotoka kwenye mkutano ule Dodoma mwishoni wa miaka ya tisini, nilikata shauri kwamba mwaka 2005 nitagombea Ubunge hii ni baada ya kushudia aina ya wabunge waliokuwepo.

Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam kusomea “Bachelor in Business Administration (BBA) kwenye programu ya jioni; nilifanya hivyo kwa kuamua kwa kuwa nilitaka nisome huku nikiendelea na kazi. Mkuu wa Programu hiyo wakati huo alishangaa sana kwa umri wangu (wakati huo shahada hiyo walikuwa wakisoma wazee watu wazima wafanyakazi) na matokeo yangu (kwa kuwa yaliniruhusu kwenda kuingia kusoma katika mfumo wa kawaida). Nikamweleza akanielewa kwamba sitaki kusoma kama wanachuo wengine wa kawaida, uamuzi wangu huo ulikuwa na gharama kwa kuwatafsiri yake ni kuwa nilipaswa kujisomesha binafsi.

Kwa hiyo mimi ni kati ya wale ambao hatudaiwi na nchi hii kwa maana ya kwamba sijawahi kuchukua ruzuku wala kusomeshwa na Serikali hii inayoongozwa na CCM; nimesoma kwa jasho la wazazi wangu na langu binafsi. Kwa hiyo, nijibu tu kuhusu elimu yangu ya juu kwamba nimesoma miaka mitatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (mtu aliyosoma kwa kiwango hicho kwenye baadhi ya vyuo duniani hupewa associate degree).

Mwaka 2004 ikaanza misukosuko mbalimbali, mwaka huo ulikuwa ndio unatungwa muswada wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, haya matatizo yanayotokea leo niliyatabiri wakati huo.
Niliwasilisha mada kwa wanachuo kwenye ukumbi wa Nkurumah kuchambua udhaifu wa muswada huo na kupata maoni ya wanafunzi kuhusu marekebisho yanayohitajika; wanachuo wakapitisha azimio la kwamba muswada huo upingwe.

Kesho yake nikiwa Morogoro kikazi kukafanyika mgomo hatimaye wanafunzi wakapigwa na kukamatwa.Nakumbuka nilikatiza kazi niliyokuwa nafanya nikarejea kwa kuwa Chuo kiliweka sharti kwamba lazima wanachuo waache mgomo ndio waliokamatwa waachiwe. Wakati huo Serikali ya wanafunzi ilikuwa haisikilizwi, mimi na wengine wachache tukajitolea kuzunguka kampasi na hosteli zote kushawishi wanafunzi kurejea masomoni na wakafanya hivyo.

Serikali ya CCM ikatoa maelekezo kwamba kama tumeweza kuwafanya wanafunzi warudi, hata kama sikushiriki mgomo na sihusiki na masuala ya mikopo kwa kuwa ni mwanafunzi ninayejilipia mwenyewe lazima nisimamishwe; nikiwa mwanafunzi pekee wa BBA niliyesimamishwa wakati huo.

Nikarejea baada ya muda tayari kukiwa na mvutano kati yangu na utawala, mwaka 2005 nikaamua kugombea Ubunge wakati huo nikiwa mwanafunzi; mvutano ukaongezeka zaidi. Na utawala wa Chuo ukawa unapata mashinikizo mengi kutoka kwa Serikali na CCM; wengine wakipendekeza nifukuzwe, wengine nifelishwe na wengine nisiruhusiwe kuingia katika maeneo ya Chuo jioni masomoni kwa kuwa nitakuwa nafanya kampeni.

Nikawa katika mtanziko(dilemma) wa kuchagua ama kuendelea na masomo na kujitoa au kupunguza nguvu kwenye kampeni (mbinu nyingi zilitumika wakati huo, sio sehemu ya majibu yangu ya leo) au niendelee na kampeni. Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki.

Mwaka 2006 nikiwa Marekani nilitafakari sana na kufikia uamuzi wa kuendelea na kazi hii ya kusimamia mabadiliko na kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2010. Mwaka 2010 niligombea tena na kushinda wakati huo huo nikiongoza kazi za kitaifa za kampeni makao makuu pamoja na Profesa Baregu na wengine; hakuna mahali popote nilipowadanganya wananchi kuhusu elimu yangu, kama nilivyoeleza hapo juu.

Naamini wananchi wa Jimbo la Ubungo walinichagua kwa uwezo na uadilifu wangu, na walijua pia kwamba nilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mitatu.
Naamini elimu ni kitu muhimu sana kwa kiongozi, lakini wapo wenye elimu kubwa ya vyeti lakini hawajaelimika na wapo wenye elimu ndogo sana ya vyeti lakini wanaelewa mkubwa wa kutimiza majukumu yao ya uongozi.

Tangu mwaka 2012 na 2013, nimekuwa kwenye mtanziko mwingine na viongozi wangu ndani ya chama wanafahamu; niliomba kuachia majukumu mengine yote katika chama ili nibaki na ubunge peke yake niweze kuwatumikia wananchi wakati huo huo niendelee na masomo zaidi ya elimu ya juu katika fani inayoendana na kazi ninayoifanya ya sasa na matarajio yangu ya baadaye.

Hata hivyo, kwa mwelekeo huu wa Serikali na CCM leo nieleze tu kwamba nikifanya hivyo itakuwa faida zaidi kwa watawala tunapoelekea mwaka 2015; hivyo, nimeamua kama nilivyoamua mwaka 2005; kwamba nitarejea masomoni baada ya CCM kuondoka madarakani na Tanzania kupata Serikali mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho.

Wakili Ridhwan katika maandiko yake amefanya rejea ya suala Kihiyo wa CCM Temeke, nashauri arejee kwenye hukumu ya kesi ile na marekebisho ya sheria yaliyofanywa na Serikali yaCCM kuwalinda wabunge wake vihiyo baada ya hukumu.

Mifano hailingani kwa sababu mimi sijatoa maelezo ya uongo popote. Lakini hata kwa wabunge wa CCM wanaotoa maelezo ya uongo wa wapiga kura, marekebisho hayo yamewawekea wigo wa mianya yakutokea mahakamani.
Zamani fomu zakuogembea zilikuwa na mahali pa kujaza elimu ya mgombea, sasa kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo, suala la kughushi na kutoa taarifa za uongo haliko kama ilivyokuwa awali, isipokuwa kesi inaweza kufunguliwa ya ukiukwaji wa kawaida wataratibu za kampeni kwa kuwashawishi wapiga kura kwa taarifa za uongo (ndani ya ule muda wa kisheria wa kesi kufunguliwa ambao ulishapita).

Halafu ni jukumu la mlalamikaji sio tu kuthibitisha kwamba uongo ulitolewa bali uongo umeathiri vipi matokeo. Ndio maana leo kuna vihiyo wengi tu wa CCM ndani ya Bunge lakini ni vigumu kuwabana kwa mfumo wetu wa sasa.
Baada ya majibu hayo marefu, naamini sasa Nape unaweza sasa kurejea kwenye kujibu; Elimu ya Mnyika ina uhusiano gani na CCM kuahidi kwenye ilani yake na kushindwa kutekeleza kwamba ifikapo mwaka 2010 asilimia 90 ya wananchi wa mijini ikiwemo Dar essalaam watakuwa wanapata maji safi na salama? Ridhwan kwa kuwa umeweza kufanya rejea unaweza pia kueleza ni kwanini Rais Kikwete mwaka 2011 aliahidi kuwa tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa historia mwezi Februari 2013 lakini mwezi huo umefika na matatizo bado ni makubwa?

JJ
kwa kazi unazofanya wala hauna haja ya kurudi chuoni inachotakiwa ni kupewa PHd
 
Sijui nishaisoma hii makala ya Mnyika mara ngapi sasa, ila ninauhakika si chini ya mara 5, na sichoki! da inatia hamasa sana
 
Hizi kauli za kusema elimu sio vyeti halafu mnashangaa kwanini wanafunzi hawafaulu. Its simple, kwa sababu jamii haiheshimu elimu, inaheshimu longolongo na porojo zinazopigwa bungeni. Kwanini mwanafunzi akeshe akisoma wakati anajua kuwa akipiga domo tu inatosha???

acha ujinga wewe vyeti kama wewe unaweza kua navyo au Nape na Ridhiwani vimepoteza maana wewe akili yoko hiyo ni ya kukuongoza kuvuka barabara tu na kuendea chooni.
 
Zomba na wapuuzi wenzako wote pamoja na ualimu wako wote mmesha sikia kwamba kijana kamaliza six na hajafeli popote .Sasa imesha wasaidia kuwapatia watanzania maisha bora mliyo waahidi ? JJ ni kwamba hata yule ---- wenu wa class gani sijui hagusi kazi yake matusi tu naona sasa katulia .

Kwani hapa kuna hoja ya kufeli au kupasi? na nani aliosadikisha hayo ayasemayo?

Hoja ni kuwa hajamaliza chuo kikuu, asiseme uongo!
 
Kamanda ni vizuri kiwei a rekodi sawa! Nape na Riz njooni sasa tujadili...
 
dah aisee huo muandiko tu hatari,hivi ametumia font gani vile?..

Mnyika ni kichwa sana,Nape hawezi kurudi hapo.
 
acha ujinga wewe vyeti kama wewe unaweza kua navyo au Nape na Ridhiwani vimepoteza maana wewe akili yoko hiyo ni ya kukuongoza kuvuka barabara tu na kuendea chooni.

Mashabiki wa chadema matusi ni kawaida yenu. Tumeshawazoea.
 
Nilikuwa katikati ya kazi jimboni nikaambiwa kwamba kuna mwito humu wa Nape na Ridhwan kutaka nieleze elimu yangu. WanaCCM walianza suala hili kwa ari, nguvu na kasi mpya niliposema kwamba nchi imefika hapa ilipo kwa sababu ya udhaifu wa Rais Kikwete, uzembe wa Bunge na upuuzi wa CCM.

Nikapuuza, naona sasa limeibuka tena kwa ari, nguvu na kasi zaidi baada ya yaliyojiri bungeni kuhusu hoja binafsi niliyowasilisha bungeni kuhusu maji na mkutano wa hadhara wa tarehe 10 Februari 2013 na masuala ambayo niliipa Serikali wiki mbili kuyatolea majibu ama sivyo nitaongoza maandamano ya wananchi kwenda Wizara ya Maji kutaka uwajibikaji na hatua za haraka.

Kwa mara nyingine tena zinafanyika jitihada za kuhamisha wananchi kwenye mjadala kwa kumshambulia mtoa hoja badala ya hoja, sasa ili turejee kwenye mijadala ya msingi ni muhimu niweke kumbukumbu sawa kuhusu masuala kadhaa kama yalivyoombwa.

Elimu yangu sio siri, nimegombea ubunge mara mbili mwaka 2005 na 2010 na mara zote nimeeleza kuhusu suala hili; Nape na Ridhwan wangetumia tu elimu yao wangetafuta kwenye mitandao na kukuta majibu wanayoyatafuta. Nieleze kwa muktasari tu; nimesoma shule ya msingi Mbuyuni Dar Es Salaam (nilikuwa mwanafunzi wa kwanza kwa mkoa wa Dar es Salaam).

Nilichaguliwa kwenda Shule ya Sekondari ya Ilboru wakati huo ikiwa ya vipaji maalum, sikwenda; wito ulinituma kwenda Seminarini. Nilisoma Franciscan Seminary Maua (FRASEMA) mpaka kidato cha nne; nilipata daraja la kwanza; nikiwa na alama A katika masomo tisa.

Ningeweza kwenda shule yoyote ya Serikali ya kidato cha tano na sita yenye mchepeo ambapo ningeutaka; lakini niliamua kubaki Dar es Salaam shule ya Tambaza kwa sababu nilitaka kusoma huku nikiendelea na harakati ambazo nilizianza kabla.

Hapa ndio ilikuwa chanzo cha mimi kuingia kwenye kazi ya kuhamasisha mabadiliko kwenye mimbari nje ya utumishi wa madhabahuni. Tukio lililobadili mwelekeo wa maisha yangu, mwaka 1998 nikiwa kidato cha nne; nimesoma na tumeanza mitihani tukatangaziwa kwamba mitahani yote imefutwa baada ya kuvujishwa.Tukarudishwa nyumbani kipindi hicho nikaenda kwenye mafungo kujitafakari kwenye mkoa mmoja nikarejea Dar es Salaam nikakutana na wanaharakati kadhaa wa asasi zisizo za kiserikali; maelezo kuhusu ufisadi yalinifanya nione nina wajibu kwa nchi yangu, nikarejea Seminarini kufanya mitihani nikiwa na fikra tofauti.

Matokeo yakatoka nimefanya vizuri, kwa mifumo yetu mibovu ya wakati huo kwa mara ya pili tena Serikali hii inayoongozwa na CCM haikutambua vipaji na nikapaswa niendelee kujilipia ada mwenyewe kama ilivyokuwa kwa ngazi nyingine za elimu zilizotangulia; hapa nikakata shauri kwamba nitatumia uwezo na uadilifu wote ambao Mwenyezi Mungu amenijalia kuwezesha mabadiliko katika taifa letu.

Nikaamua kuacha kwenda kwenye shule za bweni mikoani na kubaki Dar es salaam nisome Tambaza huku nikiendelea na kazi za harakati; wakati huo nikihamasisha masuala ya ukombozi wa vijana nchini. Pamoja na kusoma kutwa huku nikifanya kazi nilipata daraja la pili katika kidato cha sita.

Taasisi nilizoanzisha au nilizoongoza katika kipindi hicho na kazi nilizofanya sio siri na zinapaswa kujieleza zenyewe kwa matendo badala ya maneno.
Katika kipindi hicho, wakati huo kukiwa hakuna Mfuko wa Elimu wala Bodi ya Mikopo nikashiriki katika ushawishi wa mabadiliko ya kimfumo; nilikwenda Dodoma, tukakutana na wabunge na mawaziri nikawasilisha mada “Towards a more functional education in Tanzania”, wakati huo nikiwa mwanafunzi wa Sekondari.

Kati ya wabunge waliosikiliza mada niliyoiwaisilisha wakati huo sasa ni Rais Jakaya Kikwete ( Ridhwan ukiwa nyumbani unaweza kumwuliza maoni yake aliyotoa siku hiyo kuhusu ugharamiaji wa elimu na suala la mauaji ya mwanafunzi wa Iyunga Michael Sikupya). Nilipotoka kwenye mkutano ule Dodoma mwishoni wa miaka ya tisini, nilikata shauri kwamba mwaka 2005 nitagombea Ubunge hii ni baada ya kushudia aina ya wabunge waliokuwepo.

Mwaka 2002 nilijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Es Salaam kusomea “Bachelor in Business Administration (BBA) kwenye programu ya jioni; nilifanya hivyo kwa kuamua kwa kuwa nilitaka nisome huku nikiendelea na kazi. Mkuu wa Programu hiyo wakati huo alishangaa sana kwa umri wangu (wakati huo shahada hiyo walikuwa wakisoma wazee watu wazima wafanyakazi) na matokeo yangu (kwa kuwa yaliniruhusu kwenda kuingia kusoma katika mfumo wa kawaida). Nikamweleza akanielewa kwamba sitaki kusoma kama wanachuo wengine wa kawaida, uamuzi wangu huo ulikuwa na gharama kwa kuwatafsiri yake ni kuwa nilipaswa kujisomesha binafsi.

Kwa hiyo mimi ni kati ya wale ambao hatudaiwi na nchi hii kwa maana ya kwamba sijawahi kuchukua ruzuku wala kusomeshwa na Serikali hii inayoongozwa na CCM; nimesoma kwa jasho la wazazi wangu na langu binafsi. Kwa hiyo, nijibu tu kuhusu elimu yangu ya juu kwamba nimesoma miaka mitatu Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam (mtu aliyosoma kwa kiwango hicho kwenye baadhi ya vyuo duniani hupewa associate degree).

Mwaka 2004 ikaanza misukosuko mbalimbali, mwaka huo ulikuwa ndio unatungwa muswada wa Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, haya matatizo yanayotokea leo niliyatabiri wakati huo.
Niliwasilisha mada kwa wanachuo kwenye ukumbi wa Nkurumah kuchambua udhaifu wa muswada huo na kupata maoni ya wanafunzi kuhusu marekebisho yanayohitajika; wanachuo wakapitisha azimio la kwamba muswada huo upingwe.

Kesho yake nikiwa Morogoro kikazi kukafanyika mgomo hatimaye wanafunzi wakapigwa na kukamatwa.Nakumbuka nilikatiza kazi niliyokuwa nafanya nikarejea kwa kuwa Chuo kiliweka sharti kwamba lazima wanachuo waache mgomo ndio waliokamatwa waachiwe. Wakati huo Serikali ya wanafunzi ilikuwa haisikilizwi, mimi na wengine wachache tukajitolea kuzunguka kampasi na hosteli zote kushawishi wanafunzi kurejea masomoni na wakafanya hivyo.

Serikali ya CCM ikatoa maelekezo kwamba kama tumeweza kuwafanya wanafunzi warudi, hata kama sikushiriki mgomo na sihusiki na masuala ya mikopo kwa kuwa ni mwanafunzi ninayejilipia mwenyewe lazima nisimamishwe; nikiwa mwanafunzi pekee wa BBA niliyesimamishwa wakati huo.

Nikarejea baada ya muda tayari kukiwa na mvutano kati yangu na utawala, mwaka 2005 nikaamua kugombea Ubunge wakati huo nikiwa mwanafunzi; mvutano ukaongezeka zaidi. Na utawala wa Chuo ukawa unapata mashinikizo mengi kutoka kwa Serikali na CCM; wengine wakipendekeza nifukuzwe, wengine nifelishwe na wengine nisiruhusiwe kuingia katika maeneo ya Chuo jioni masomoni kwa kuwa nitakuwa nafanya kampeni.

Nikawa katika mtanziko(dilemma) wa kuchagua ama kuendelea na masomo na kujitoa au kupunguza nguvu kwenye kampeni (mbinu nyingi zilitumika wakati huo, sio sehemu ya majibu yangu ya leo) au niendelee na kampeni. Nafsi yangu ikanituma kuamua kuandika barua yakuahirisha masomo, baada ya matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2005 mazingira yalikuwa yamebadilika sana kuweza kurejea kumalizia mwaka au miezi michache iliyokuwa imebaki.

Mwaka 2006 nikiwa Marekani nilitafakari sana na kufikia uamuzi wa kuendelea na kazi hii ya kusimamia mabadiliko na kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2010. Mwaka 2010 niligombea tena na kushinda wakati huo huo nikiongoza kazi za kitaifa za kampeni makao makuu pamoja na Profesa Baregu na wengine; hakuna mahali popote nilipowadanganya wananchi kuhusu elimu yangu, kama nilivyoeleza hapo juu.

Naamini wananchi wa Jimbo la Ubungo walinichagua kwa uwezo na uadilifu wangu, na walijua pia kwamba nilikuwa Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa miaka mitatu.
Naamini elimu ni kitu muhimu sana kwa kiongozi, lakini wapo wenye elimu kubwa ya vyeti lakini hawajaelimika na wapo wenye elimu ndogo sana ya vyeti lakini wanaelewa mkubwa wa kutimiza majukumu yao ya uongozi.

Tangu mwaka 2012 na 2013, nimekuwa kwenye mtanziko mwingine na viongozi wangu ndani ya chama wanafahamu; niliomba kuachia majukumu mengine yote katika chama ili nibaki na ubunge peke yake niweze kuwatumikia wananchi wakati huo huo niendelee na masomo zaidi ya elimu ya juu katika fani inayoendana na kazi ninayoifanya ya sasa na matarajio yangu ya baadaye.

Hata hivyo, kwa mwelekeo huu wa Serikali na CCM leo nieleze tu kwamba nikifanya hivyo itakuwa faida zaidi kwa watawala tunapoelekea mwaka 2015; hivyo, nimeamua kama nilivyoamua mwaka 2005; kwamba nitarejea masomoni baada ya CCM kuondoka madarakani na Tanzania kupata Serikali mpya itakayoongozwa na CHADEMA. Kwa sasa nitaendelea kujisomea kila siku ninapopata wasaa kwa kuwa elimu haina mwisho.

Wakili Ridhwan katika maandiko yake amefanya rejea ya suala Kihiyo wa CCM Temeke, nashauri arejee kwenye hukumu ya kesi ile na marekebisho ya sheria yaliyofanywa na Serikali yaCCM kuwalinda wabunge wake vihiyo baada ya hukumu.

Mifano hailingani kwa sababu mimi sijatoa maelezo ya uongo popote. Lakini hata kwa wabunge wa CCM wanaotoa maelezo ya uongo wa wapiga kura, marekebisho hayo yamewawekea wigo wa mianya yakutokea mahakamani.
Zamani fomu zakuogembea zilikuwa na mahali pa kujaza elimu ya mgombea, sasa kipengele hicho kimeondolewa. Hivyo, suala la kughushi na kutoa taarifa za uongo haliko kama ilivyokuwa awali, isipokuwa kesi inaweza kufunguliwa ya ukiukwaji wa kawaida wataratibu za kampeni kwa kuwashawishi wapiga kura kwa taarifa za uongo (ndani ya ule muda wa kisheria wa kesi kufunguliwa ambao ulishapita).

Halafu ni jukumu la mlalamikaji sio tu kuthibitisha kwamba uongo ulitolewa bali uongo umeathiri vipi matokeo. Ndio maana leo kuna vihiyo wengi tu wa CCM ndani ya Bunge lakini ni vigumu kuwabana kwa mfumo wetu wa sasa.
Baada ya majibu hayo marefu, naamini sasa Nape unaweza sasa kurejea kwenye kujibu; Elimu ya Mnyika ina uhusiano gani na CCM kuahidi kwenye ilani yake na kushindwa kutekeleza kwamba ifikapo mwaka 2010 asilimia 90 ya wananchi wa mijini ikiwemo Dar essalaam watakuwa wanapata maji safi na salama? Ridhwan kwa kuwa umeweza kufanya rejea unaweza pia kueleza ni kwanini Rais Kikwete mwaka 2011 aliahidi kuwa tatizo la maji Dar es Salaam litakuwa historia mwezi Februari 2013 lakini mwezi huo umefika na matatizo bado ni makubwa?

JJ

avatar205_5.gif

Nimemkumbuka sana yule gwiji mwanzilishi na mgunduzi wa Apple Macintosh aliyefariki karibu mwaka mmoja uliopita. Katika historia ya maisha yake anafanana na Mnyika. Hakuwahi kuhitimu chuo ingwa alikuwa Mwanachuo. Pamoja na kutohitimu chuo amekuwa kichwa cha ajabu katika kugundua computer ambayo ndiyo maarufu kwa wataalamu wa design hata software za computer nyingine nyingi zimetokana na Apple. Leo ulimwengu unatamba na simu zake katika kizazi cha leo. Hakuwa na vyetu ukutani.

Nani asiyejua Mnyika alivyo na uwezo wa kujenga hoja zenye kuakisi hali halisi ya maisha na manufaa kwa taifa? Tatizo la CCM wakishaishiwa nguvu ya hoja huanza mashambulizi kwa mtu binafsi maana yake hoja ya nguvu dhidi ya nguvu ya hoja.
 
Hizi kauli za kusema elimu sio vyeti halafu mnashangaa kwanini wanafunzi hawafaulu. Its simple, kwa sababu jamii haiheshimu elimu, inaheshimu longolongo na porojo zinazopigwa bungeni. Kwanini mwanafunzi akeshe akisoma wakati anajua kuwa akipiga domo tu inatosha???

Cheti unaweza kukipata kwa :
1.Kukariri bila kuelewa a(kumeza nakutapika kwenye mtihani)
2 kuwahonga au kuwainfluency wahadhili kwa manufaa ya mitihani yako kwa namna yeyote ile e.g cheo cha baba ,hela , ngono n.K
3kudesa kwa wezio au vyovyote vile

Lakini elimu lazima ujifunze kiukweli na uwe mzuri kichwani. Kujifunza sio lazima ukae Drsn
Wapo college drop out kama Bill gate ambao ukuzi na ueledi wao hauwezi kufananishwa na wengi humu mlio na digrii feki

Myika is intelligent , his IQ is great no ubishi

Kuna dalili zote kwamba Riz1 anatoka ukoo wa vilaza
 
Kwani hapa kuna hoja ya kufeli au kupasi? na nani aliosadikisha hayo ayasemayo?

Hoja ni kuwa hajamaliza chuo kikuu, asiseme uongo!
wewe uliyemaliza mbona hatuoni impact ya Elimu yako kwenye nchi hii zaidi ya kukesha JF kushabikia udini?
 
Back
Top Bottom