Majibu kwa lara 1

Majibu kwa lara 1

ng`wana ong`wa kulwa

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
2,420
Reaction score
1,754
Jana lara 1 alianzisha mada inayosema, wanawake above 30 hata 40 marriage is a hypocritical institution. Kilichonishitua ni kuita ndoa ni hypocritical institution tafsiri isiyo rasmi ni taasisi ya kinafiki/unafiki.

Mimi nimeoa na nina mtoto mmoja sikubaliani kabisa na mtazamo huu wa lara 1

Lara 1 ni binti ambaye hajawahi kuwa kwenye ndoa hivyo kujifanya anayajua mambo ya ndoa kwa undani ni uongo,ni sawa na mtu aliyeishia kidato cha sita na kujifanya anajua sana matatizo ya chuo kikuu ili hali hajatia mguu pale.

Anatahadharisha wale ambao ndoa zao zinaonekana ziko vizuri kwa sasa kwamba na wao ndoa zao zaweza geuka kuwa kilio,anasema kwamba kwani ndoa zao zina uspecial upi.

Ukweli ni kuwa ndoa haziwezi kufanana hata siku moja kama anavyotaka yeye ziwe. Si lazima ndoa zote ziwe na migogoro hata kidogo,kuna ndoa zinaanza vizuri zinaishia vizuri.

Zingine zinaanza vizuri zinaishia vibaya,zingine zinaanza vibaya zinaishia vizuri,zingine zinaanza vibaya na kuisha vibaya,kutegemea na wanandoa wenyewe wanavyoendesha ndoa yao.

Anashangaa wana ndoa wa jf hawatoi ushuhuda wa ndoa zao au kuomba ushauri wakati mambo yanapoharibika.kwa vile binti huyu hajawahi kuwa kwenye ndoa sishangai kuona akiuliza kitu kama hiki ndoa ina maadili yake mojawapo ni kutotoa siri nje ya ndoa.

Hii haimaanishi kwamba wafe na tai shingoni kuna taratibu zake akiingia kwenye ndoa ataambiwa ndiyo maana wapo na wasimamizi wa ndoa kuwaelekeza nini cha kufanya.

Lakini hata wale mambo yao yako salama kabisa wanaogopa kutoa ushuhuda wao kuogopa kejeli,dharau kutoka kwa watu wenye mtazamo kama wa huyo dada. Lakini ajue pia walioko kwenye ndoa hasa wanawake wana majukumu mengi ya kifamilia tofauti na walio single.

Anadai kuwa wanawake walioko kwenye ndoa ni wanafiki kwa sababu waume zao wanazini nje ya ndoa na wengine wana watoto nje ya ndoa,wengine hawatoi matumizi nyumbani lakini hawawakatazi,hvyi anauhakika gani hawawakanyi waume zao?

Yeye mwenyewe wapo watu walishamshauri aache tabia yake ya kuchuna wanaume lakini hajaacha lakini si kwamba hajashauriwa.

Anaelekea kuhitimisha kwa kusema ndoa ni safari hivyo wanaofurahi sasa wajiandae kwa lolote mbeleni yaani kufiwa na mwenza,kupata ajali,mwenzi kulogwa.

Hapa amenishangaza zaidi ina maana walio single hawafiwi hata na wazazi,ama rafiki kufiwa ni mpaka awe mme au mke.

Basi nachelea kusema sikumwelewa Lara1, mie niliona mantiki ya sred ile ilikuwa ni kwamba, wanawake kati ya 30-40, walio wanaopata pressure katika jamii kuolewa, wawe makini, wasikubali kuwa bullied. Sababu kubwa ikiwa ni kuwa si kila ndoa ina furaha(japo wengi hawasemi), na maisha yote yana changamoto.
 
Inawezeakana uko sawa kilicho nifanya niazishe uzi ni kuita ndoa ni hypocritical instution hilo tu
 
Ile thread ilikuwa ya kuwapa moyo wanawake wa 30s na 40s....Na si thread ya kukandia ndoa...

Ni kweli ilikuwa inawapa moyo kwa upande mmoja kwa upande mwingine kuna kitu aliongelea ndoa zenyewe hebu kairudie tena maana mimi nimejibu kwa mtazamo wangu kulingana na hoja alizojenga kwenye post yake.
 
Basi nachelea kusema sikumwelewa Lara1, mie niliona mantiki ya sred ile ilikuwa ni kwamba, wanawake kati ya 30-40, walio wanaopata pressure katika jamii kuolewa, wawe makini, wasikubali kuwa bullied. Sababu kubwa ikiwa ni kuwa si kila ndoa ina furaha(japo wengi hawasemi), na maisha yote yana changamoto.

Ukiifuatilia ile thread vizuri ni kama lara 1 kuna muda alikuwa anaenda nje ya key, labda ilikuwa ni katika kuoanisha kwamba hata hizo ndoa zenyewe sio kitu kiviile (wadada wasizikimbilie) akaishia kubase sana kuziponda ndoa badala ya kuelezea faida za kusubiri kwanza kama kusoma, career growth, kujikusanyia mali etc.
 
Last edited by a moderator:
Nawahi nafasi! Nimerudi!

YES MARRIAGE IS A HYPOCRITICAL INSTITUTION SIFUTI KAULI!

Naomba kujibu hoja zako kama ifuatavyo!

Kwanza ile kama fasihi simulizi yoyote inapokelewa tofauti tofauti na hadhira! Naomba nijibu mapokeo yako ya ile fasihi andishi nilioiweka jana. Kama fanani ni wajibu wangu kujibu querry sijui spelling nimemapatia manake watu watu wa grammar mnanikalia mnoo kooni siku hizi kama ifwatavo!

1. Kweli sijaolewa, na wala siwezi kudanganya niliolewa ama vipi, hapanaaaa! Ila ile ni observation yangu kama LAY MAN au THIRD PARTY tu ambayo ni HAKI YANGU YA KIKATIBA UKIZINGATIA WE HAVW BEEN A FREE COUNTRY SINCE 9 DECEMBER 1961. Na neno langu sio sheria ama presidential decree ni mtazamo tu binafsi.

2. Kweli nimetahadharisha si wanandoa tu, bali BINADAMU KWA UJUMLA WETU kuwa maisha ni safari ndefuu sanaaa, ukicheka leo kesho huenda unune nanikaenda mbali sanaa kuwaomba bin adaam MUMUOMBE MUNGU AWAFANYIE WEPESI MIZIGO YENU na sio kuhukumu watu wengine na kuwasulubisha msalabani!

3. All in all sijaona ulipo dhibitisha PASIPO SHAKA YOYOTE kuwa MARRIAGE IS NOT A HYPOCRITICAL INSTITUTION! The hypocrisy inakuwa pale MNAPOJADILI HII TAASIS HAMUWEKI KARATA ZOTE MEZANI, MNAJADILI MAZURII TUUUUUU! Sio uugwana huo! Sawa wekeni mazuri na vibaya pia mseme?

4. Tabia ya kuchuna hahahahaaaaaa! COUNTING MY SINS DOES NOT MAKE YOU A SAINT!

Hitimisho!
TUWE TU WA WAZI UOLEWE, USIOLEWE, MAISHA YOTE NI CHANGAMOTO! Married people should be honest and stop window dressing of facts THAT THEY ARE THE HAPPIEST, LUCKIEST, AND BETTER THAN EVERYBOY HAVING A HEAVEN ON EARTH AND SINGLE OLD CARGOS LIKE ME SHOULD GO HUG A TRANSFOMER BECAUSE WE ARE PITYFULL! Hypocrisy at its highest!

IT ABOUT TIME WE PUT ALL THE CARDS ON THE TABLE!
 
Ile thread ilikuwa ya kuwapa moyo wanawake wa 30s na 40s....Na si thread ya kukandia ndoa...

Ni kweli lakini sehemu kubwa ya maelezo yalikuwa kukandia ndoa! As if anashauri wasiende kwa sababu ndoa siyo.
 
Sidhani kama kuna mdada anapenda kuishi bila ndoa maisha yake yote ila hutokea tu akajikuta umri umeenda na yupo kwenye hali hiyo. Alichokiandika yule mdada ni kuwa courage wasijione wao ni tofauti na maisha yaendelee sikudhani kama aliwakosea waliokua ndoani mpaka kupatiwa majibu.
 
Ukiifuatilia ile thread vizuri ni kama lara 1 kuna muda alikuwa anaenda nje ya key, labda ilikuwa ni katika kuoanisha kwamba hata hizo ndoa zenyewe sio kitu kiviile (wadada wasizikimbilie) akaishia kubase sana kuziponda ndoa badala ya kuelezea faida za kusubiri kwanza kama kusoma, career growth, kujikusanyia mali etc.

mkuu Raimundo ulivyoelewa wewe na mimi ndiyo niliona hivyo
 
Back
Top Bottom