mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,219
- 6,650
Bado ukweli utabaki kuwa hata kukiwa na hiyo inayodaiwa ni Tume Huru, watumishi wake ni binadamu wenye mapungufu yao. Ila kama mgombea ana sifa za kukidhi matarajio ya wapiga kura atapata kura zao na kuchaguliwa.Kwa macho yangu niliona kwenye chaguzi za marudio, mawakala wa upinzani wakipigwa kama wezi na jeshi la polisi ili kusaini fomu fake za matokeo. Kinachoendelea kwenye vituo vya kura kiko wazi, na sisi wananchi tumekuwa tukiona. Uzuri ukweli hauhitaji nguvu kubwa kuutetea, maana ukweli huwa unajibeba wenyewe. Kinachoendelea kwenye box la kura toka awamu hii ya tano imeingia, sio uchaguzi bali ni maonyesho ya ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura.