Majibizano ya wanasiasa baada ya Mtatiro kuhamia CCM

Ketoka

JF-Expert Member
Joined
Sep 23, 2015
Posts
1,121
Reaction score
1,983
Dar es Salaam. Wanasiasa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini wametoa maoni tofauti kuhusu uamuzi wa mwanasiasa Julius Mtatiro aliyetangaza kuhama CUF na kuonyesha nia ya kuhamia CCM.

Mtatiro ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa CUF, amewaambia wanahabari leo Agosti 11, 2018 jijini Dar es Salaam kwamba, amejiuzulu CUF na yuko tayari kujiunga na CCM kwa ajili ya kumuunga mkono Rais John Magufuli.

Saa chache baada ya kutangaza uamuzi huo, wanasiasa mbalimbali waliibuka na kuandika kwenye mitandao ya kijamii wengine wakimpongeza na wengine wakimkosoa.

Mbunge wa Kigoma Mjini, (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe ameandika kwenye ukurasa wake wa Twita ameandika akisema:

“Huko wanakokutegea kukufukuza kila usemapo ukweli? Ninaamini kwenye maendeleo ndani ya Demokrasia na siyo maendeleo ndani ya udikteta. Ninaamini katika uhuru wa fikra na siyo mawazo ya kiimla.Ninaamini nchi yetu inahitaaji chama kingine kuirudisha kwenye reli. Nafasi ya CCM ni Museum (makumbusho).

Mbunge wa Nzega, (CCM) Hussein Bashe ameujibu ujumbe wa Zitto akisema:

“Ni rahisi kuleta mabadiliko ya haki, demokrasia na maendeleo ndani ya CCM) kuliko kutafuta mabadiliko nje kwa sababu kuna mgogoro wa kimawazo, kimuundo na kimadili huko nje. Kuna wanajeshi wachache wa ukweli.”

Kwa upande wake, Nape Nnauye Mbunge wa Mtama (CCM) ameandika akisema:

“Tunachagua rangi ya Paka wakati shida yetu ni kukamata Panya.Nguvu tunayopoteza kuhoji rangi ya paka ingetumika kushughulika na panya tungekuwa mbali sana,”

Nape katika nukuu yake nyingine ameandika akisema:

“Kama msomi wa Sayansi ya Siasa, naona hii ni fursa muhimu ya kujengwa kwa aina mpya ya vyama na siasa za upinzani nchini. Kwa demokrasia, hamahama hii muhimu itumike kama fursa ya kujenga upya uimara wa CCM unaotegemea ubora wa upinzani(Simba/Yanga).

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole yeye ameandika:

“Huu unaitwa uhuru wa kisiasa kwa mujibu wa katiba yetu, halafu wale wa ‘siasa za bei nafuu mseme kanunuliwa;” Hongera kaka, ndugu, kamaradi. Historia na Mungu pekee atakupa tuzo ya dhamira yako njema. Na mimi nimeikuta mtandaoni.”

Baadae mh Zitto akamjibu Husen Bashe kwa kupitia twitter
Screenshot_20180811-154404.jpg
 
Sina chama cha siasa wala kadi ya chana chochote...
Lakini kwa jinsi nilivyokuwa namsoma huyu jamaa Mtatiro sikuwahi kuwaza kama anaweza kuhama..

Nawaomba wanasiasa wengine wa ccm na chadema kuanzia leo muwe mnaweka akiba ya maneno maana leo tukisema tuweke screenshot za matusi ya mtatiro kwa ccm yanaweza kufika hata page ya 20 hapa jf..
Lakini leo anaomba kwenda ccm..

Mwanasiasa niliyebaki nae kitoka upinzani na imani kidogo (2%) ni malisa na lissu.

Na hawa wakihama basi inabidi wanasiasa mtuachie dunia yetu nyie mkakae na viumbe wenzenu mnaowezana sayari nyingine
 
Mbona unakata tamaa ndungu?
 
Bora CCM wanajiuliza na kutafakari lakini upande wa pili jibu lao ni moja tu …..WAMENUNULIWA . Wanakiri kuwa wananunulika….ambao hawajapata soko wanawacheka waliopata soko …..ni swala la muda tu na busara Zaidi ni kukaa kimya kuliko kujifanya unanyooshea vidole wengine kumbe na wewe utajaa kwenye kumi na nane zao siku si nyingi. Mnyenyekevu angejiuliza nini kinawatokea hawa majabali? Tunakosea wapi na nini?
 
Write your reply...kwa mtatiro kujiunga na ccm,naamini kuna kitu kipo ccm.japokuwa watu wanasema kuwa wanaoenda ccm wananunuliwa.
 
Sina chama cha siasa wala kadi ya chana chochote...
Lakini kwa jinsi nilivyokuwa namsoma huyu jamaa Mtatiro sikuwahi kuwaza kama anaweza kuhama..

Nawaomba wanasiasa wengine wa ccm na chadema kuanzia leo muwe mnaweka akiba ya maneno maana leo tukisema tuweke screenshot za matusi ya mtatiro kwa ccm yanaweza kufika hata page ya 20 hapa jf..
Lakini leo anaomba kwenda ccm..

Mwanasiasa niliyebaki nae kitoka upinzani na imani kidogo (2%) ni malisa na lissu.

Na hawa wakihama basi inabidi wanasiasa mtuachie dunia yetu nyie mkakae na viumbe wenzenu mnaowezana sayari nyingine
Wewe una moyo mgumu sana. Na si kweli kwamba huna itikadi ya chama flani. Endelea kuwaamini wanasiasa Wa Afrika
 
Sina chama cha siasa wala kadi ya chana chochote...
Lakini kwa jinsi nilivyokuwa namsoma huyu jamaa Mtatiro sikuwahi kuwaza kama anaweza kuhama..

Nawaomba wanasiasa wengine wa ccm na chadema kuanzia leo muwe mnaweka akiba ya maneno maana leo tukisema tuweke screenshot za matusi ya mtatiro kwa ccm yanaweza kufika hata page ya 20 hapa jf..
Lakini leo anaomba kwenda ccm..

Mwanasiasa niliyebaki nae kitoka upinzani na imani kidogo (2%) ni malisa na lissu.

Na hawa wakihama basi inabidi wanasiasa mtuachie dunia yetu nyie mkakae na viumbe wenzenu mnaowezana sayari nyingine
wanasiasa ni kama watoto wa miaka 2, sio wa kuwatilia maanani kwa kila kitu, akili zao wanazijua wao na Mungu wao.

sasa nazidi kuamini Tanzania hakuna wapinzani wa kisiasa.
 
Sina chama cha siasa wala kadi ya chana chochote...
Lakini kwa jinsi nilivyokuwa namsoma huyu jamaa Mtatiro sikuwahi kuwaza kama anaweza kuhama..

Nawaomba wanasiasa wengine wa ccm na chadema kuanzia leo muwe mnaweka akiba ya maneno maana leo tukisema tuweke screenshot za matusi ya mtatiro kwa ccm yanaweza kufika hata page ya 20 hapa jf..
Lakini leo anaomba kwenda ccm..

Mwanasiasa niliyebaki nae kitoka upinzani na imani kidogo (2%) ni malisa na lissu.

Na hawa wakihama basi inabidi wanasiasa mtuachie dunia yetu nyie mkakae na viumbe wenzenu mnaowezana sayari nyingine
Ulitegemea Mugabe kusaliti chama alichokianzisha na kusapoti upinzani, hawa waache tu kama walivo hakuna ajuaye kesho yake.
Screenshot_2018-07-30-18-49-18.jpg
 
Polepole katisha sana eti "wale wa siasa za bei nafuu...."
 
Hahahaha

Mtatiro Kama kanunuliwa ndio asinunuliwe Kubenea Au Joshua Nassari?

Mwanasiasa wa kuaminika Bado hajazaliwa Tanzania
 
Sina chama cha siasa wala kadi ya chana chochote...
Lakini kwa jinsi nilivyokuwa namsoma huyu jamaa Mtatiro sikuwahi kuwaza kama anaweza kuhama..

Nawaomba wanasiasa wengine wa ccm na chadema kuanzia leo muwe mnaweka akiba ya maneno maana leo tukisema tuweke screenshot za matusi ya mtatiro kwa ccm yanaweza kufika hata page ya 20 hapa jf..
Lakini leo anaomba kwenda ccm..

Mwanasiasa niliyebaki nae kitoka upinzani na imani kidogo (2%) ni malisa na lissu.

Na hawa wakihama basi inabidi wanasiasa mtuachie dunia yetu nyie mkakae na viumbe wenzenu mnaowezana sayari nyingine
Dah, imebidi niandike kidogo. Sikutegemea hili toka kwa Mtatiro, wanasiasa si watu. Mkuu umeandika vyema sana ila nimesikitika sana.
 
Zitto ameapa kutoa CCM madarakani?!!..sujui nicheke au nilie teh.
 
Back
Top Bottom