Maji ya mto yabomoa barabara kata ya Mazimbu, Morogoro Mjini

Oct 8, 2023
37
17
MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini,Dkt. Abdulaziz Abood amefanya ziara ya kushutukiza kwenye Kata ya Mazimbu kwa lengo la kujionea athari ya mvua katika miundombinu ya barabara zilizopo katika Kata hiyo.

Mhe. Mbunge ameshuhudia namna miundombinu ya barabara hizo zilivyoathiriwa hasa kipande cha kuanzia eneo la Barakuda hadi Kampasi ya Solomon Mahlangu (Mazimbu Ndani).

Hali hiyo imesababishwa na maji yanayopita mto ngerengere kuacha mkondo wake na kukatisha kwenye barabara hiyo jambo ambalo linasababisha adha kwa watumiaji barabara hiyo wakiwemo madereva wa malori ya mchanga na kuhatarisha usalama kwa wananchi.

Kutokana na hali hiyo, Mh. Mbunge ameahidi kuongea na Mamlaka zinazohusika wakiwemo Wakala wa Barabara za mijini na Vijijini TARURA Manispaa ya Morogoro ili kufanya haraka kurekebisha barabara hiyo.

IMG_20240118_113617_3.jpg
 
View attachment 2875553
Mtajuana wenyewe huko Moro. Uzuri mmepewa na gari la kuzikana
 
Back
Top Bottom