Kachimbe kisima wewe mwenyewe ndugu yangu na unywe maji yako peke yako.
Usishiriki na mwingine,Ni hatari kubwa sana.
Hakika,maji ya kisima cha watu wengi yameingiliwa na mdudu,
ukiwa na kiu usiyaonje,Utaambukizwa.
Siku hizi kiu ya maji imeongezeka sana,watu wanayanjwa maji kila wakati,...
mengine yanauzwa kila kona ya barabara,..mengine hutolewa bure.
Nani atapona?
Kwa sababu maji yameingiliwa na mdudu,yanapatikana kiurahisi sana.
Ukipita kote utayaona,usiyanywe.
Yapo yaliyowekwa kwenye chupa kubwa na ndogo,wengi wanakimbilia yaliyo
kwenye chupa ndogo wakidhani ndio salama,wana jidanganya....
Hayo ndio machafu kupindukia.
Tafadhalini sana wapendwa,chimba kisima chako mwenyewe.
Chota maji vile utakavyo,chemsha mara kwa mara na usiyanywe na mtu mwingine
nawe utakuwa salama.
Kuweni na weekend njema.
na mie nina rig ya kuchimbia visima
naweza kujua sehemu ya kuchima kisima kwa matokeo mazuri zaidi
at a reasonable price
discount ipo.
Mchimba kisima...? Kaingia mwenyewe! Kaingia.
Tafadhalini sana wapendwa,chimba kisima chako mwenyewe.
Chota maji vile utakavyo,chemsha mara kwa mara na usiyanywe na mtu mwingine
nawe utakuwa salama.
Duh! umemwelewaje mleta mada yakhe? Una drill babukubwa ati? Au ndo mwenye kisima unataka tujikimu kwako? Una hakika na maji yako hayana virus?
Hii Jamii forums ni meli inayokusanya wengi kuanzia watoto wachanga hadi maajuza na vibabu. Hilo usishangae maana ndivyo alivyosoma mstari kwa mstari na kuuelewa wakati we unaangali ujumbe gani umebebwa katika mada hii.
Ujumbe wako umesikika mbali kupitiliza mipaka.
Mazoea ya kubadilisha kisima cha maji kila leo ndio hatari ya kutojua maji yapi yako safi kuyanywa.
Kisima chako mwenyewe utakitunza vizuri kila siku na kuhakikisha kimefunikwa virus hawaingii.
Wengi tuna kawaida ya kuchota maji na kuyanywa kwa domo toka kiganjani, hakuna hakika ya safi au la na hatuna fulsa ya kuyachemsha .
Wengine tamani ya kisima cha mbele au kisima kinachopatikana kwa urasihi hukimbilia kuchota maji kumbe ndio kipindupindu kimejaa.
Weekend tunapopumzika ndio kiu inatushika zaidi na mara nyingi hata maji ya kisima changu hayazimi kiu ila kisima cha jirani kina maji ya kuzima kiu.
Mimi kufa na kupona na kisima changu, maana visima vingine sina nafasi ya kuhakiki usalama wa maji yake.
Yes weekend njema na tujihadhari na maji ya visima mbalimbali hasa ya maji bei poa, na hasa visima vinayvozagaa ovyo mitaani, utakuja shtukia siku mtu unaharisha na kutapita kipindupindu kisicho na tiba huku mtu anachungulia na kuyaona mauti yanavyomchelewesha, maji haya ya visima balaa, maana wengine haturidhii kupata kikombe kimoja cha ndani, tunataka visima vya kulee vyenye kutoa vikombe zaidi vya kunywa, hapo mambo ni mkorogo wa kutojijua na mwendoo huu kipindupindu kitakaponishika sitajua ni kisima kipi ambacho hakikuwa na maji salama.
hivi kiumbe chaweza kweli kujichimbia kisima chake yenyewe na kunywa maji chenyewe bila ya kuingiliwa? Nijuavyo Muumba ndiye awezaye kukuwezesha ukaqfanikisha hayo....pekee yako huwezi................kwanza uwezo wa kukichimba hicho kisima hatuna. pili kisima nacho kinasikia kiu na chaweza kutafuta maji kutoka kwenye visima athirika na kukusogezea wewe vijirusi kutoka visima hatarishi...................................mambo siyo mepesi hivyo......................mtegemee Muumba kwa yote atakuongoza njia stahiki..........
Drink water from your own cistern, running water from your own well
Genesis 6-15
ukishachimba cha kwako mwenyewe utajuaje kama watu hawaji kukuibia ukitoka????labda ukifunike na ukitie kofuli