Majeshi yasigeuzwe chaka la kuficha mafisadi

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Hakuna jambo linaloanza kuniogopesha kama hii mbinu chafu inayoanza kutumiwa na baadhi ya viongozi wetu wapumbavu kutaka kuyatumia majeshi yetu kama chaka la kufichia wizi na vitendo vyao vya hujuma na ufisadi dhidi ya maslahi ya taifa.

Tusidanganyane, katika masuala ya wizi, hujuma na ufisadi hakuna popote duniani unapoweza kuacha kushughulikiwa kwa kisingizio kwamba ni mambo nyeti yanayohusu usalama wa taifa, huo ni uongo.

Katika miaka ya karibuni tumeshuhudia masuala ya ufisadi ndani ya majeshi kama ya Afrika kusini ya kashfa ya ununuzi wa ndege za kijeshi, kashfa ya ununuzi wa rada na silaha huko Saudia n.k vikiandikwa na kutangazwa na vyombo vya habari vya dunia kwani vilihatarisha usalama gani kwao?

Huku kwetu tumebaki kuficha mambo na kudanganyana, ebu watanzania tujiulize, hivi Lugumi aliyesaini mkataba na jeshi la polisi kulifungia mashine za kuchukulia alama za vidole kwenye vituo vyake lina unyeti gani, na huyo Lugumi aliyesaini mkataba na kujua kila kilichomo kwenye mkataba na hao mafundi wake waliotumika kuvifunga vifaa hivyo waliaminiwa vipi lakini wabunge wetu wasiaminiwe kuuona na kuhoji? Tunaomba watawala wasipende kucheza na akili za watanzania.

Namwomba mheshimiwa Rais asikubaliane na upumbavu huu wa viongozi kuvichafua vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na kuvifanya chaka la kufichia madhambi yao.

Naomba kuwasilisha.
 
Well said
Ila huu mfupa.mgumu sana kwa mkuu... kati ya ile mifupa tunayoijua
 
Hii kuficha mikataba imelipatia hasara sana nchi tukianzia ile ya Tanesco, Bandari ya bagamoyo, police, majeshini, gas and mingine ambayo imefichwa chini ya uvungu. Ni wakati sasa JMP ukaweka system ambayo itatoa ruhusa kwa hii mikataba kupitiwa na wataalam binafsi ambao hawana masilahi yao binafsi.
 
Back
Top Bottom