Majeshi ya Senegal yaingia Gambia

Majeshi ya Senegal yaingia Gambia

Vikosi vya majeshi kutoka nchini Senegal vimethibitisha kuingia katika ardhi ya Gambia katika muda ambao rais mpya Adama Barroe anaapishwa.
Msemaji wa jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndiaye ameiambia BBC kwamba vikosi hivyo vimevuka mpaka na kupiga hatua kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo,Banjul.

Na kusema kwamba vikosi hivyo mpaka sasa havijakabiliana na ukinzani wa aina yoyote ingawa viliweka bayana kwamba vilikuwa vimejizatiti kwa mapigano ikibidi.

Mapema baraza la usalama la Umoja wa mataifa inasemekana kwa siri limekuwa likiunga mkono juhudi za vikosi vya ECOWAS, kuhakikisha kwamba rais Barrow anachukua madaraka kutoka kwa rais aliyemaliza muda wake Yahya Jammeh.

Rais huyo wa zamani wa Gambia,awali aligoma kuachilia madaraka.
Rais wa sasa Adama Barrow ameapishwa leo katika nchini jirani kwenye ubalozi wa Gambia ulioko mjini Dakar nchini Senegal na kufuatiwa na shamra shamra ubalozini hapo.

Mpaka sasa haijafahamika wazi lini lini rais mpya wa Gambia ataweza kurejea nchini mwake na kuchukua hatamu za uongozi kwa mara ya kwanza akiwa rais
 
Huyo jamaa.bado.hajakamatwa tuu??

Alicheza.karata zake vibaya sana naisi atakuwa amekimbia bila.shaka..

Ila wabongo bhana kuna.hapo juu unasema anatamani Ecowas waje hata huku??

Waje kufanya nn?? Hata hivyo hakuna mgombea ambayo tume imetangaza kashindwa alafu yeye kakatalia madarakani

Mjue tofaut hiyoo,mkuruzinza na mseven sanduka la kura walishinda

Tatizo la tz ni tume ya uchaguzi


Sasa mnao laam jesh,nakusema mkuu wa majesh wa gambia ni mfano nasio wa huku kwan kuna nchi EAST imekumbwa na balsa kama gambia??


Huyo rais wa gambia alibugi
Kama angejua toka awali angecheza kiccm zaid kuweka sawa tume ya uchaguzi upande nk

Kujiamin kupita kiasi ndio kumemponza
Wewe ni mpuuzi sana kilichotokea Zanzibar na Gambia tofauti ni IPI?
 
Wameingia kwa ajili ya ku mantain peace maana huwezi jua pengine jameh ameenda kujipanga ili arudi.
 
Siasa za bongo zimewaharibu watu uwezo wa kufikiri,yani mtu anatamani hadi vita et kisa tu ccm.
 
Siasa za bongo zimewaharibu watu uwezo wa kufikiri,yani mtu anatamani hadi vita et kisa tu ccm.
Kichekesho zaidi ni aina viongozi tunaotaka wawe mbadala, yaani utoe serikali ya Magufuli uweke serikali ya Lowasa,Mbowe, Kingunge na Sumaye eti ndio wawe mbadala.
 
Kichekesho zaidi ni aina viongozi tunaotaka wawe mbadala, yaani utoe serikali ya Magufuli uweke serikali ya Lowasa,Mbowe, Kingunge na Sumaye eti ndio wawe mbadala.
Ah we achana tu mkuu,ndiyo maana wengine tumekaa pembeni tunaangalia tu.
 
Ni raha sana pale demokrasia inapotetewa, the people has spoken, respect their decision looser. Sijui kwanini wanajeshi wa huku kwetu nchi za maziwa makuu hawako hivi
 
Kwa nini jeshi la Gambia halikumlazimisha Jammey aachie madaraka kwa sababu lengo lao halikuwa vita, na hawamuungi mkono dikiteta Jammey
 
Kwan unaona hiyo ni sawa na kinachotokea GAMBIA??

Helewa kuwa rais wa gambia kagoma matokea na tatizo la tz ni tume

Nyambafu mwenyewe..maana hujui wanaweza peleka majeshi na wakasema kulinda amani kwasababu za msingi hata km.sio kweli hata ecowas wasinge vamia kisa zanzibar

Ndio mana faizafox anasema

Huko shule mlienda kusoma ujinga

Balaa la gambia ni tofaut na zenji jiongeze
Utafauti wa znz na gambia ni upi
 
Siasa za bongo zimewaharibu watu uwezo wa kufikiri,yani mtu anatamani hadi vita et kisa tu ccm.
Haki inapo dhulumiwa dawa yake ni mwenye nguvu kumshinda muonezi wizi wa kura udanganyifu katika jumla ya matokeo jecha type ingefaa kupigwa ccm ni balaa huku eac unafiki mwingi.
 
Utafauti wa znz na gambia ni upi
Ngoja nijibu tofaut nyingine sasa

Rais wa Tanzania alishinda tayar na Zanzibar sio nchii so waingilie kwann??

Gambia tume ilitangaza mshindi,zamzibar tume haikutangaza mshindi


Hivi napenda hao ecowas huwa wanaingilia na ushindan wa wabunge kweli??
 
Back
Top Bottom