Majeshi ya Senegal yaingia Gambia

Baazigar

JF-Expert Member
Aug 30, 2015
1,129
1,101
Habari wakuu....nipo naangalia FRANCE 24 mda huu..! Wanadai majeshi ya Senegal yameingia Gambia,maneno hayo yamesemwa na msemaji wa jeshi...Mkuu wa majeshi wa Gambia yuko pamoja na wafuasi wa Barrow wakishangilia Street

Source :FRANCE 24

====

Vikosi vya majeshi kutoka nchini Senegal vimethibitisha kuingia katika ardhi ya Gambia katika muda ambao rais mpya Adama Barroe anaapishwa.
Msemaji wa jeshi la Senegal Kanali Abdou Ndiaye ameiambia BBC kwamba vikosi hivyo vimevuka mpaka na kupiga hatua kuelekea katika mji mkuu wa nchi hiyo,Banjul.

Na kusema kwamba vikosi hivyo mpaka sasa havijakabiliana na ukinzani wa aina yoyote ingawa viliweka bayana kwamba vilikuwa vimejizatiti kwa mapigano ikibidi.

Mapema baraza la usalama la Umoja wa mataifa inasemekana kwa siri limekuwa likiunga mkono juhudi za vikosi vya ECOWAS, kuhakikisha kwamba rais Barrow anachukua madaraka kutoka kwa rais aliyemaliza muda wake Yahya Jammeh.

Rais huyo wa zamani wa Gambia,awali aligoma kuachilia madaraka.
Rais wa sasa Adama Barrow ameapishwa leo katika nchini jirani kwenye ubalozi wa Gambia ulioko mjini Dakar nchini Senegal na kufuatiwa na shamra shamra ubalozini hapo.

Mpaka sasa haijafahamika wazi lini lini rais mpya wa Gambia ataweza kurejea nchini mwake na kuchukua hatamu za uongozi kwa mara ya kwanza akiwa rais
 
IMG_20170119_234143.jpg
 
Senegalese troops entered neigbouring Gambia on Thursday, an army spokesman said, as part of regional effort to support its new President Adama Barrow in a showdown with longtime ruler Yahya Jammeh, who has refused to step down.

"We have entered Gambia," Colonel Abdou Ndiaye wrote in a text message to Reuters.

Adama Barrow was inaugurated Thursday in a hastily arranged ceremony at Gambia's embassy in Senegal. The small embassy room held about 40 people, including Senegal's prime minister and the head of Gambia's electoral commission.
5cb850b63524421fb0c825acf911b8e3_18.jpg

Senegalese troops enter Gambia in support of new president - France 24
 
Nimependa sana msimamo wa mkuu wa majeshi wa gambia.
Nataman kungekua na wakuu kama hawa wa majeshi zile nchi ambazo zinaongozwa kidikteta kwamba viongozi mda wao unaisha lakini hawtok madarakani
Hivi mfano raia wakadhurika na hayo majeshi ya ecowas, na mkuu wa majeshi ya gambia kasema hatopigana, itakuwa ni sahihi? Maana hiyo ni kama vita, risasi hailali njaa vitani... Nauliza kitu nusichokijua ili nieleweshwe, ni sawa? Au maamuzi aliyochukua ndio sahihi? Msaada wakuu!!
 
Hivi mfano raia wakadhurika na hayo majeshi ya ecowas, na mkuu wa majeshi ya gambia kasema hatopigana, itakuwa ni sahihi? Maana hiyo ni kama vita, risasi hailali njaa vitani... Nauliza kitu nusichokijua ili nieleweshwe, ni sawa? Au maamuzi aliyochukua ndio sahihi? Msaada wakuu!!
Anaposema hatapigana anamaanisha kuepusha mapigano. majeshi wenyeji wasiporesist majeshi ya kigeni yatapigana na nani. Kifupi ana busara kwamba acha majeshi ya nje yaungane na ya ndani kulinda usalama na wakati huohuo kumkamata jammeh bila kudhuru RAIA.
 
Hivi mfano raia wakadhurika na hayo majeshi ya ecowas, na mkuu wa majeshi ya gambia kasema hatopigana, itakuwa ni sahihi? Maana hiyo ni kama vita, risasi hailali njaa vitani... Nauliza kitu nusichokijua ili nieleweshwe, ni sawa? Au maamuzi aliyochukua ndio sahihi? Msaada wakuu!!
Uamuzi.wa mkuu wa majesh ni sahihi
na raia watadhurikaje mana huyu yahaya anachotegemea ni hilo.hilo.jeshi la nchi yake limsaidie ..na mihimil yote imemkimbia,si mahakama,,si tume ya uchaguzi, kote huko alikimbilia kuwabembeleza, lakin wanamkimbia,.jeshi akiwemo mkuu wa majeshi sasa linamsikiliza rais barrow ambae ndo rais sasa kamil wa gambia, kwaio yahaya sidhan kama ana ujanja tena aondoke tu kwa hiari yake mana fedheha atakayoipata itakua kubwa
 
Back
Top Bottom