Majengo yanayovutia kwa ubunifu bora zaidi duniani

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,446
The-Isokon-building-in-London-1933-designed-by-Wells-Coates.jpg

Jengo la Isokon, London (1933), limedizainiwa na Wells Coates.

PAMOJA na kwamba makazi au nyumba msingi wake mkubwa ni kumwezesha binadamu kupata mahali pa kuishi, bado ujenzi hubeba kitu kingine; sanaa ya kuvutia. Mmarekani Michael Webb msanifu wa majengo ambaye ameifanya kazi hiyo kwa miaka karibu 40 hadi akatoa kitabu chake kiitwacho “Building Community: New Apartment Architecture”.

Kitabu hicho kinazungumzia mahitaji ya kujenga nyumba nyingi zaidi kwa ajili ya makazi ya watu ili kuondokana na matatizo ya nyumba katika miji mbalimbali na kwa kuitumia ardhi vizuri zaidi kwa kujenga nyumba nyingi lakini katika maeneo madogo. Katika kusisitiza wito wake huo wa kujenga nyumba na kuongeza usanii, msanifu huyo alikusanya mifano mbalimbali ya ujenzi na usanifu wa nyumba zaidi ya 30 duniani.

Miongoni mwa hizo, zifuatazo ni nyumba tano zinazovutia kwa usanifu wake na zinatoa fursa kubwa ya kuchukua idadi kubwa ya watu katika ardhi au eneo dogo:


nn.jpg
CityLife, Milan, Zaha Hadid Architects (2004-14)

Hili ni eneo la makazi ya watu wenye kipato cha juu ambalo limepambwa na usanii wa hali ya juu likiwa jijini Milan, Italia, likichukua eneo la kilomita moja ya mraba. Usanifu wake ukiwa umefanywa na Zaha Hadid, Daniel Libeskind na Arata Isozaki. Eneo hilo linajumuisha fleti 1,930


buildings-ghorofa-5.jpg
The Interlace, Singapore, OMA/Ole Scheeren (2007-13)

Makazi haya, au jengo hili, kwa jumla ni moja ya vivutio vikubwa vya usanifu wa majengo duniani. Msanifu wake, Ole Scheerren, ni dhahiri alichoshwa na ujenzi wa maghorofa marefu zaidi kwenda juu na badala yake akaamua kuyatawanya katika eneo moja na kufupisha urefu wa kwenda juu. Matokeo yake, aliweza “kuyashusha” mafleti 1,040 ambayo yangekwenda juu angani, yakajikuta katika jengo la kawaida fupi katika eneo la hekta 20 tu.


buildings-ghorofa-1.jpg
25 Verde, Turin, Luciano Pia (2007-13)


Usanifu wa jengo hili unayafanya mazingira yake yavutie kiasi kwamba hata familia ya Uswiss iliyozoea mazingira ya miti na mimea, ingeweza kuhamia katika jiji la Turin, Italia, na kujikuta ikifurahia kama iko nyumbani. Jengo hilo limepambwa na miti 150 ambayo hutunzwa ili kuleta mvuto kwa jengo hili katika usanifu wa kujenga makazi na kujumuisha miti.

Usanifu huo kutoa vivuli vya burudani na faragha zinazoambatana na bustani. Jengo hilo lenye fleti 63 ni kivutio kikubwa hasa kwa watu wenye kipato cha kati.


buildings-ghorofa-9.jpg
Sugar Hill, New York, Adjaye Associates (2012-14)

Wasanii wa jengo hili lililopo jijini New York, Marekani, walilenga kuwasaidia maskini. Msanifu wake, David Adjaye, ndiye aliteuliwa na mamlaka za ujenzi wa nyumba na mashirika yasiyo ya kibiashara, kulijenga jengo hilo lenye ghorofa 13. Lina fleti 124 ambapo asilimia 70 ni kwa ajili ya watu wenye kipato kilicho chini ya nusu ya kipato rasmi, na asilimia 25 ni kwa ajili ya watu wasio na makazi. Pamoja na kwamba kila fleti lina chumba kimoja tu na dirisha la upande mmoja tu, bado usanifu wake ni wa kuvutia.


buildings-ghorofa-8.jpg
V_Itaim, Sao Paulo, Studio MK27 (2011-14)


Moja ya kero za watu wanaoishi katika mafleti ni kukosa faragha kutokana na macho ya nje ambapo majengo mengi huwa ni ya kuta za vioo zinazowezesha watu walio nje kuona kinachotokea ndani. Katika jengo hilo, na mengine, katika jiji la Sao Paolo, Brazil, wasanifu wa majengo wamekabiliana na kero hiyo kwa kuweka vipande vinavyovutia vya mbao ambavyo huchomekwa katika maeneo ya chini ya kuta za vioo ili kuzuia taswira ya ndani isionekane kutoka nje, hivyo kuwafanya wakazi wake kuzuia pia kelele na mwanga kutoka nje.

Pamoja na kuzuia kero hizo, mbao hizo maalum huwa ni moja ya mapambo tosha ya usanifu wa majengo hayo.


Kanungila Karim
 
Nchi Na Yote Viijazavyo Dunia Ni Mali Ya Bwana

Mungu Ni Mwema Wakati Wote
 
Zaha hadid - Beijing Airport
 

Attachments

  • CD53237A-BD51-4766-A498-706B0BB9AB06.jpeg
    CD53237A-BD51-4766-A498-706B0BB9AB06.jpeg
    60 KB · Views: 27
Back
Top Bottom