Majarida haya na watunzi wake:wako wapi?

Nakapanya

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2012
Posts
2,096
Reaction score
709
katika miaka ya tisini hadi 2000 kulikuwa na majarida mbalimbali yaliyokua yakituburudisha sana.Moja ya majarida hayo yalikua kama vile,BONGO,TABASAMU na SANI.Humo ndani kulikua na watunzi wazuri sana na wenye ubunifu wa hali ya juu sana,watunzi kama vile,DAUDI MASASI,FORTUNATUS NDILA(4T NDILA),na wengineo kibao.Hakika majarida haya yalikua yanatuburudisha sana na ilikua kila mwezi lazima upate kopi yako. Unakumbuka stori kama zifuatazao:- -Anga za wenyewe -Pablo Zungu -Bush Stars vs Born Town -Zena na Betina Kipepe na Mkasa wa masokwe unakumbuka watu wafuatao:- -Mapung'o -Njomba Nchumbari -Bob Mikwara Je wewe binafsi unazikumbuka stori hizo,watu hao na watunzi wake?hebu ongezea wengine bac na stori nyingine ili tukumbushane enzi.
 
Na Darasa la Mapenzi unalikumbuka? Na unajua kila aliyejiandikisha kwenye darasa hili alipelekwa wapi?
 
4T NDILA alikuwa mchoraji. Unaikumbuka "Mlinzi wa zamu".
Riwaya: Hata ukioga mjini huendi.
Mwinyi mpeku na wakeze,Mporipori.
 
hahaaaa mkuu umenikonga nyoyo sawasawa,hiyo riwaya nakumbuka kwenye Bongo,mzee utamu ule sijui kwann umepotea,
 
Darasa la Mapenzi ilikuwa hadithi inatoka kwenye Heko. Na mwandishi (au niseme Mwalimu wa hilo Darasa) alikuwa mmiliki wa gazeti mwenyewe, Ben R. Mtobwa. Katangalia mbele ya haki sasa; hayupo.

duuuh RIP Mtobwa,hivi un afikiri ubunifu ule unaweza kufanywa na vijana wa siku hizi au ndio mambo ya dunia kama kijiji?kuperuzi tu
 
Nakumbuka ndani ya SANI kulikuwa na mtunzi mahiri anaitwa Amri bawji,jamaa alikuwa ananikosha sana kwa hadithi zake kama Love story tanganyika na unguja,
Na mtunzi flani alikuwa gazeti la lete raha anaitwa Beka mfaume, namkubali aliachia hadithi miaka ya nyuma yaitwa mzee beka niliikubali, vipaji vipo sana bongo ila ndo hivyo
 
Vijana mnisamehe kwa uwazi huu. Akili za watoto tuliowazaa zina mambo mawili tu kwa sasa. Wanawaza ngono na viloba, basi. Ukitaka kujua we angalia tu humu JF. Angalia Forum za MMU kuna post ngapi, na Forum za Biashara kwa mfano, kuna post ngapi... Server zimejaa ushauri wa ngono wakati biashara hata robo ya post za MMU haifiki.

Unganisha dots hapo
 
ni kweli kabisa mkuu,lakini unafikiri ni nini kilichopelekea mpaka majarida yale yakapotea kabisa
 
Vijana mnisamehe kwa uwazi huu. Akili za watoto tuliowazaa zina mambo mawili tu kwa sasa. Wanawaza ngono na viloba, basi. Ukitaka kujua we angalia tu humu JF. Angalia Forum za MMU kuna post ngapi, na Forum za Biashara kwa mfano, kuna post ngapi... Server zimejaa ushauri wa ngono wakati biashara hata robo ya post za MMU haifiki.

Unganisha dots hapo

hapo kazi ipo mkuu hakika kizazi kinaangamia
 
-sheshe la wajanja
-hofu ya vizito(wadada watatu walikua majambazi hatari kwenye hadithi hii)
-ghadhabu (humu utakutana na mzee ole, zumo, obi, linda, mamvi ya ng'ombe nk)

mkuu umetisha,nakumbuka enzi hizo ikifika mwisho wa mwezi unakuwa na mshawasha kweli wa kupata nakala yako.mzee Ole alikuwa nouma kweliii....hakika nayamic sana majarida yale.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom