Majaribu yanapotokea katika maisha

Majaribu yanapotokea katika maisha

Texas Tom.

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2013
Posts
510
Reaction score
273
attachment.php

Pichani ni gari lillilopatwa na mkasa wa ajali nzito na habari yake inaanza kama ifuatavyo.

Kijana Joseph ambaye sasa ni marehemu enzi za uhai wake alibahatika kuwa na kazi nzuri kabla ya kuoa.

Baada ya kuoa miaka mitano ya kwanza akabahatika kuwa na watoto mapacha wa kike na wa kiume na mke wake aliishi kwa furaha akifurahia baraka ambazo Mungu aliwapa familia ile.

Mke hakuwa na kazi na mme akaona ni vyema amsaidie kwa kumsajilia kampuni na mama yule akawa na kampuni ya mitindo na ikafana sana na kupata umaarufu katika eneo lile.

Miaka michache baadae baadae mme akapatwa na matatizo kazini na kusimamiswa kazi na kwa kuwa alikuwa daktari basi na leseni yake ya udaktari ikafungiwa na hakutakiwa kufanya kazi yoyote.

Mpango huo ulisukwa na wenzake pale kazini kwa kuwa alisifiwa sana kwa utendaji wa kazi zake na kupinga vitendo vya rushwa.

Maisha yakazidi kuwa mabaya pale nyumbani kwani miaka ilivyosogea hakupata tena wala kuliona lile penzi la mkewe, kwani mke akawa ni mtu wa kumchukia mmewe mara mme akihitaji fedha apewe kwa masimango na mbaya zaidi hata watoto wakaanza kufundishwa na mama yao kumchukia baba yao.

Hali ile ilimpa mzee yule wakati mgumu na ikafikia kipindi akaanza kudhohofika mwili kwa mawazo ingawa akajitahidi sana kutoyaonhesha hayo machoni pa matu na majirani.

Baada ya muda akapatwa na homa na akawa akijiuguza lakini baada ya muda akashauriwa aende akapimwe na kugundulika kuwa alikuwa na tatizo katika moyo wake lililosababishwa na msongamano wa mawazo.

Akamfuata mkeweofisini kwake na kumwambia anatyatizo la moyo na ilihitajika apate msaada wa fedha kiasi cha laki tano (500,000) kwa thamani ya fedha za kitanzania ili afanyiwe upasuaji wa haraka na kujiokoa katika hali hiyo hatarishi kwa maisha yake.

Mke alimjibu, " Sidhani kama nina hela ya kuchezea kwa kukupa mwanaume usiye na faida kwa familia yako... yaani mpaka chupi nikununulie mimi?Wanaume wenzako wanfanya kazi na sio kama wewe ulivyo sasa"

Baba alinyanyuka na kuufuata mlango bila ya kusema nen machozi yakimtoka na akikumbuka jinsi alivyoijenga familia yake kwa upendo na amani akiwapa mahitaji yote na jinsi alivyotumia mpaka tone lake la mwisho la fedha, muda na hata jasho kuinyanyua biashara ya mkewe ambayo ni kwa ajili ya familia.

Akawasha gari na kuondoka kuelekea nyumbani akiwa na mawazo huku akiona jinsi mtu umpendaye anayoweza kubadilika kiasi cha kukuombea ufe kwa kuwa ni kero kisa huna kazi na kumfananisha na wale wote.

Huku nyuma mke akaingiwa na roho ya ubinadamu na na kujilaumu kwa kauli ile na kuanza kuumia kisha akajaribu kumpigia simu mzee ikawa haipokelewi na kumka kuliwasha gari na kuanza kumfuata mzee

Kilomita chache mbele akaona kuna mkusanyiko mkubwa wa watu akapaki gari na kuuliza kuna nini? wakamwambia kuna ajali ya gari kuna mzee alikuwa anataka kuingia upande wa kushoto bila kuona kama kuna gari.

Kusogea pale hakuamini kuona mwili wa mme wake ukiwa umefunikwa alinianza kutokwa na machozi kabla ya kuingia kwenye gari na kuona kuna kadi nzuri ikiwa kwenye bahasha akaifungua na kuisoma.

Kilio kikubwa kilimtoka baada ya kugundua kuwa siku hiyo ilikuwa ni siku za kuzaliwa ya baba huyo na hakuna aliyekumbuka zaidi ya yeye mzee kununua kadi iliyoandkiwa " NAKUSHUKURU MUNGU KWA KUNIFIKISHA MWAKA HUU MPYA PAMOJA NA CHANGAMOTO NINAZOZIPITIA NAAMINI KUNA SOMO WATAKA KUIPA JAMII KUPITIA MIMI. UHIMIDIWE BWANA.. HAPPY BIRTH DAY TO ME"

Mama yule aliomboleza na mpaka sasa anazidi kuomboleza na hana amani tena hata faida ya ile biashara haioni tena na hajui nani atamsamehe.

Je unapitia mapito gani sasa katika mahusiano yako?

Je unayamudu vipi matatizo ya mahusiano yako?

Je unafikiria nini kama siku ukiamka na kuona wewe ndio chanzo cha kifo, kilema au chanzo msongamano wa mawazo kwa mwenza wako kutokana na tabia zako za ubinafsi?

Ndugu una kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kukupa mwenza huyo na kuamini kuwa katika kila mnalolipitia ni jaribu la kuwafanya muwe na sababu ya kuonyeshana upendo vyema zaidi ya ule wa mwanzo;

Nimeumia sana mpaka nimefikiria sana mahusiano yangu na watu wanaonizunguka nikajiona nina kila sababu ya kusema R.I.P Joseph ni kupitia wewe umenipa somo la upendo na uvumilivu na kuzishinda stress za dunia hii.
 

Attachments

  • 1902888_588096084609238_1371003741_n.jpg
    1902888_588096084609238_1371003741_n.jpg
    34.4 KB · Views: 1,513
so sad siku zote thamani ya kitu inajulikana pale kinapopotea
 
Ila wahenga walisema 'thamani ya mshumaa utaijua pale giza linapoingia' huyu mke aliona pesa ndo kila kitu bila kukumbuka kuwa ni kwa upendo wa mume wake kumfungulia hiyo biashara ikamfikisha hapo, ni wangapi wenye waume wenye pesa na hawafunguliwi biashara? Kama ni matumizi wanapata ila shughuli ya muhimu ya kufanya kama biashara hawana? Na siku zote yule unayempenda kwa dhati na kumthamini huwa hathamini pendo lako, huthamini pendo la ulaghai lisilo la kudumu. Maandiko matakatifu yanasema hata ukitoa mali yote ukawapa masikini kama huna upendo ni kazi bure. Mungu utusaidie.
 
so touching and sad story, you never know what you got till its gone.
 
Ni ngumu sana kujua mioyo ya binadamu, you get a person whom yo can lean on, kumbe he/she is there for something else... too bad.... Rest in Peace Mr.
 
Biblia inasema ishini na wanawake zenu kwa akili. Pumzika kwa Amani Joseph, jifunze mbinu za wazee wa kiafrika huwa wana aaccount bank za akiba mabazo hata mkewe hajui. Mambo yakienda vibaya ndio unaitumia kuku boost.
 
inauma sana jamani..kweli nimeamini mwanamke mjinga atavunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe....huyo mama atajutia maisha yake yote...
 
akyanani machozi yamenilengalenga.... Sasa kama yule alidhani amani inapatikana kwa hela pekee, ndo atajua sasa. Wapo wengo sana wa hivyo

Kweli kabisa, Shukrani mkuu..
cc: sokwe
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom