Uchaguzi 2020 Majaliwa: Hatuendi kwenye Uchaguzi na jazba

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasichague kiongozi kwa sababu ya jazba au hasira.

Ametoa wito huo leo (Jumatatu, Oktoba 26, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nalasi, wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Katani. Mheshimiwa Majaliwa leo amezuru wilaya ya Tunduru akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli.

“Hatuendi kwenye chama kwa jazba wala kwa hasira. Hatari ya kipindi hiki unaweza kujikuta unaenda kwenye chama ambacho hakina sera wala hakieleweki. Chama makini kinapaswa kuwa na viongozi wanaoeleweka,” amesema.

Akitoa mfano, Mheshimiwa Majaliwa alisema leo hii kuna chama viongozi wake wamegombana na wala hakina mgombea urais. “Je ukikichagua chama hiki na ukawa na changamoto inakukabili, utaipeleka wapi? Au utampelekea nani? Na ukimchagua diwani au mbunge wa chama hicho, hayo masuala yako atayawakilisha kwa nani?”

“Ninawasihi, unapochagua viongozi, usichague chama kwa sababu maendeleo hayana chama. Chagueni chama ambacho kina mwelekeo na kinajali kutatua shida za watu. Ukienda kupiga kura, chagua diwani, mbunge na Rais anayetoka Chama cha Mapinduzi. Keshokutwa, tumchague Dkt. Magufuli kwa kura nyingi za ndiyo,” amesisitiza.

Mheshimiwa Majaliwa yuko wilayani Tunduru ambako alienda kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Tunduru Kusini, Bw. Adimu Mpakate na wagombea udiwani wa kata nne za jimbo hilo.

Akiwa njiani kuelekea Tunduru, Mheshimiwa Majaliwa alifanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya stendi ya mabasi ya Mangaka, wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara.

Akizungumza na wakazi wa Mangaka kwenye mkutano huo, aliwasihi Watanzania wasikubali kuandamana kwa kisingizio cha kutokubali matokeo ya uchaguzi kwa sababu huko ni kuvunja sheria.

“Ninawasihi vijana mjihadhari, msikubali kuandamana kwani mtakuwa mnavunja sheria na mtajikuta mnajiingiza matatizoni. Kuna mtu anakuja hapa na anatulazimisha kuandamana, huyo hafai kuwa Rais wa nchi.”

Mheshimiwa Majaliwa alitumia fursa hiyo kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Nanyumbu, Bw. Yahya Muhata na wagombea udiwani wa kata zote za jimbo hilo.
 
Wenye jazba idadi yao ndogo sana ! Kura zao ndogo sana tuwaambie tu ukweli! Kama lowassa alipata kura 6M ni ngumu sana kwa TL kufikia hata nusu ya kura hizo! Huo ndo ukweli mchungu!

Lazima tuwaandae kisaikolojia mapema maana watu matumaini yamewajaa sana ! Kutwa kucha wakikesha huku mitandaoni , wakidhani kuna mgombea wao atashinda !. Sasa kesho ndo siku yenyewe!
 
Nimefurahishwa na ujumbe wa Waziri Mkuu kuwa uchaguzi ni hekima na busara hivyo kutanguliza jazba hailipi badala yake utajikuta unachagua chama kisichokuwa na sera na uongozi thabiti.

Ujumbe huu siyo wa kubeza hata kidogo. Wahenga wanasema ukitaka kufanya jambo jema unapaswa uweke hasira pembeni. Hivyo wananchi tutafakari mambo mema yaliyofanywa na Kiongozi wetu na CCM tufanye maamuzi ya busara na hekima ya kumchagua tena ili aweze kumalizia miradi ambayo bado iko kwenye mchakato.

Natoa wito wote tunaostahili tukapige kura.
Donald Ndagula for CCM
 
We ni meanaume au mke wa mtu?? nakuona umekaa kikusutana sutana ivi. Au umeamkia kuchambwa leo??
Wenye jazba idadi yao ndogo sana ! Kura zao ndogo sana tuwaambie tu ukweli! Kama lowassa alipata kura 6M ni ngumu sana kwa TL kufikia hata nusu ya kura hizo! Huo ndo ukweli mchungu!

Lazima tuwaandae kisaikolojia mapema maana watu matumaini yamewajaa sana ! Kutwa kucha wakikesha huku mitandaoni , wakidhani kuna mgombea wao atashinda !. Sasa kesho ndo siku yenyewe!
 
Mnapotuambia maendeleo hamleti tusipoichagua CCM huwa mnatujaza jazba.
Maendeleo yatakuja vyovyote vile. Hata Kilimanjaro ilikokua ngoja ya upinzani wana ajira zaidi ya 3000 toka kwenye kiwanda cha ngozi

Sayansi ya CCM kwenye uchaguzi ni pana sana.kwa upinzani huu wa akina Zito na Mbowe hawawezi toboambele ya CCM.
 
Wenye jazba idadi yao ndogo sana ! Kura zao ndogo sana tuwaambie tu ukweli! Kama lowassa alipata kura 6M ni ngumu sana kwa TL kufikia hata nusu ya kura hizo! Huo ndo ukweli mchungu!

Lazima tuwaandae kisaikolojia mapema maana watu matumaini yamewajaa sana ! Kutwa kucha wakikesha huku mitandaoni , wakidhani kuna mgombea wao atashinda !. Sasa kesho ndo siku yenyewe!
Ukweli mchungu huu. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki CCM.
 
Uniudhi kwa kila njia halafu unipangie namna ya kukuadhibu?
Safari hii hatupangiwi, lazima tutoe adhabu ili heshima yetu itambulike kwa watawala ushwara.
 
Sielewi tena maana ya siasa ya vyama vingi! Kwani kuwa na mbunge na madiwani wanatoka vyama tofauti maana yake ni kukoka maelewano??

Hii dhana ya maendeleo hayana chama iko wapi, au ni unafiki tu???
 
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Kassim Majaliwa amewataka Watanzania wasichague kiongozi kwa sababu ya jazba au hasira.

Ametoa wito huo leo (Jumatatu, Oktoba 26, 2020) wakati akizungumza na wakazi wa kata ya Nalasi, wilayani Tunduru, mkoani Ruvuma katika mkutano uliofanyika kwenye viwanja vya Katani. Mheshimiwa Majaliwa leo amezuru wilaya ya Tunduru akimuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli.

“Hatuendi kwenye chama kwa jazba wala kwa hasira. Hatari ya kipindi hiki unaweza kujikuta unaenda kwenye chama ambacho hakina sera wala hakieleweki. Chama makini kinapaswa kuwa na viongozi wanaoeleweka,” amesema.

Akitoa mfano, Mheshimiwa Majaliwa alisema leo hii kuna chama viongozi wake wamegombana na wala hakina mgombea urais. “Je ukikichagua chama hiki na ukawa na changamoto inakukabili, utaipeleka wapi? Au utampelekea nani? Na ukimchagua diwani au mbunge wa chama hicho, hayo masuala yako atayawakilisha kwa nani?”

“Ninawasihi, unapochagua viongozi, usichague chama kwa sababu maendeleo hayana chama. Chagueni chama ambacho kina mwelekeo na kinajali kutatua shida za watu. Ukienda kupiga kura, chagua diwani, mbunge na Rais anayetoka Chama cha Mapinduzi. Keshokutwa, tumchague Dkt. Magufuli kwa kura nyingi za ndiyo,” amesisitiza.

Mheshimiwa Majaliwa yuko wilayani Tunduru ambako alienda kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Tunduru Kusini, Bw. Adimu Mpakate na wagombea udiwani wa kata nne za jimbo hilo.

Akiwa njiani kuelekea Tunduru, Mheshimiwa Majaliwa alifanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya stendi ya mabasi ya Mangaka, wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara.

Akizungumza na wakazi wa Mangaka kwenye mkutano huo, aliwasihi Watanzania wasikubali kuandamana kwa kisingizio cha kutokubali matokeo ya uchaguzi kwa sababu huko ni kuvunja sheria.

“Ninawasihi vijana mjihadhari, msikubali kuandamana kwani mtakuwa mnavunja sheria na mtajikuta mnajiingiza matatizoni. Kuna mtu anakuja hapa na anatulazimisha kuandamana, huyo hafai kuwa Rais wa nchi.”

Mheshimiwa Majaliwa alitumia fursa hiyo kumuombea kura mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dkt. John Pombe Magufuli, mgombea ubunge wa jimbo la Nanyumbu, Bw. Yahya Muhata na wagombea udiwani wa kata zote za jimbo hilo.

Mimi binafsi kwa Kweli naenda kupiga kura ya jaziba na hii yote ni kutokana na maneno ya kibaguzi ya mara kwa Mara anayotoa mgombea urais kupitia chama Cha ccm kila akipanda jukwaani.
 
Back
Top Bottom