Majaji aliowateua Kikwete: Pre-emptive strike?

millioni 35

Dawa ya huyu mtu ni kuachana naye kabisa. Angekuwa ni mtu anayetoa maoni yake lazima hoja zingine angekuwa upande huu na mwingine huu, sasa huyu mtu yuko upande mmoja kila hoja mnaangaika naye kwa nini? tufanye kama tulivyofanya kwa mwali
 
Inaonesha sheria zinakupiga chenga, lakini si kitu sitarajii kuwa upo that bright kutokana na nnavoziona post zako zinavyomuandama mtu mmoja.

Hoja nyingine zinafurahisha kweli.Yaani unapima u"bright" wangu kwa kuangalia idadi ya ninaowaandama? Hivyo nikiongeza niwaandamao ndio utaniona bright.. duh!


Si uweke hapa, utatowa hoja na ushahidi unao halafu uniambie mimi nikukumbushe, unanshangaza sana na hata mantiki siioni. Hata mahakamani anaeshitaki ndie hutakiwa ku-proof. Kama nilivyosema sitegemei kama hata dogo kama hili linaweza likakupitikia kwa sababu niliyoitoa hapu ju.

Unajitahidi kusema kitu lakini husemi, next time sema unachotakakusema.

Polisi na magereza hawana uhusiano wowote na mahakama. Hata hao mapolisi na magereza wakifanya kosa hupelekwa huko huko kuhukumiwa, iwe ni mahakama ya kijeshi au kiraia. (unakumbuka Zombe?).

Kwa maneno yako mwenye umethibitisha kuwa kuna uhusiano! Labda nianze kukufundisha logic kidogo. Ni kama jamaa yenu Mwanyika jana alipojaribu kusema kitu ambacho hakutaka kukisema lakini kwa maneno yake mwenyewe alijikuta anakisema!
 
Point yako ni nzuri, lakini viongozi wanapochaguliwa na wananchi haina maana wananchi wamekasimisha madaraka yao kwao na hivyo wananchi wakae pembeni kuwaangalia viongozi wanafanya nini.



Tatizo ni kuwa lazima tuishi kwenye Taifa la kushuku, tusiposhuku na kuhisi tunawaachia wafanye wafanyazo. Kuongoza Taifa siyo kama kuongoza familia! Sisi siyo familia za viongozi hivyo tunakaa tukitumaini kama vile baba/mama afanyavyo mambo kwa maslahi ya familia basi na viongozi wa kuchaguliwa nao watafanya hivyo kwa maslahi ya Taifa.

Historia inashuhudia hilo; viongozi wakiachwa bila kufuatiliwa, kuhisiwa, kuulizwa maswali n.k huanza kufanya mambo kwa maslahi yao. Mkapa hatukumhisi kuwa amefanya madudu Ikulu; hatukuhisi Daniel Yona amejigawia Kiwira, hatukuhisi Chenge ni mwanasheria mbovu n.k Ni kutokuhisi kwetu kumetufikisha hapa.

On my part, I'll suspect them until proven otherwise. I trust them, but I demand proof! Sikubali tu ati wakisema "tunafanya mambo kwa uzalendo" basi tupige makofi na kushangilia.




Ndiyo tunafanya hivyo lakini haina maana tukishapiga kura basi tunawaachia nchi wafanye wapendalo. Nilipiga kura 2005, na nitapiga tena 2010. Lakini nikishapiga kura siendi likizo na kusubiri miaka mitano.

Uliwapigia kura CCM?
 
Heshima Mbele,

Kuana jambo moja hapa,Kwani jaji anatoa maaumuzi kabla ya kupata maelezo ya Mashaidi?Mie naona ni sawa kwa wao kupewa madarak ili waweze kuendesha kesi kwa kasi,alafu nachokifahamu kuwa jaji kuna kamati ambayo huwa inapendekezsa na Rais anapewa majina tu.tusiangalie jambo moja tu kwamba mujilizi kapewa ujaji ili khali na inawezekana kuna wapo majaji walipewa kwa upendeleo mkubwa,na inafahamika wazi.

tuangalie nini watafanya kama wakichaguliwa na tusianze kuwasakama kabla hawajanza kazi.tukianza na dhambi hii hata watu wataanza kuhoji uhalali wakuchagua upinzani ili khali kuna baadhi ya viongozi walipitia maisha ya kifuska miaka ya nyuma na inafahamika wazi.

Mie nafikiri jambo la Msingi ni utendaji wa kiongozi kwanza!
 
Yes sir I did kwenye Urais kwenye Ubunge hapana...
Mwanakijiji Bwana,ndio maaana hata wakati unachagua rangi ya JF Pre. member ulichagua ya kijani..Mie ubunge niligawa kwa Upinzani ila niliyempigia alishinda ina nilisikia CCM walimnunua ili akubali matokeo.wakamjengea na nyumba!

2010.Nitapigia CCM,na Ubunge nitavote kwa Mchungaji Mtikila!
 
Mwanakijiji Bwana,ndio maaana hata wakati unachagua rangi ya JF Pre. member ulichagua ya kijani..Mie ubunge niligawa kwa Upinzani ila niliyempigia alishinda ina nilisikia CCM walimnunua ili akubali matokeo.wakamjengea na nyumba!

2010.Nitapigia CCM,na Ubunge nitavote kwa Mchungaji Mtikila!

Nyie mnaoendelea kuipigia kura CCM ndivyo mlivyo!!!
 
Nyie mnaoendelea kuipigia kura CCM ndivyo mlivyo!!!


Nilikuwa hivyo, sasa siko hivyo wale ambao ndivyo mlivyo mnauwezekano mkubwa wa kuiendelea kuichagua CCM hadi pale mtakapokataa mawazo ya 'ndivyo tulivyo'. Miye niligundua mapema kuwa nilifanya makosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia!
 
Nyie mnaoendelea kuipigia kura CCM ndivyo mlivyo!!!
sasa unataka nipigie Chama gani wakati hata nisipopiga kinaendelea kushinda.mie nimeamua kujiunga nao ila kuna kipindi nilitoka kuwaamsha watanzania nikaona hawaamshiki na moshi wa mwenge.

kama ukiona wanakushind aungano nao na utuie mbinu ya kutoka kama alivyofanya Odinga.
 
Nilikuwa hivyo, sasa siko hivyo wale ambao ndivyo mlivyo mnauwezekano mkubwa wa kuiendelea kuichagua CCM hadi pale mtakapokataa mawazo ya 'ndivyo tulivyo'. Miye niligundua mapema kuwa nilifanya makosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia!

Ina maana you "voted for IT before you voted against IT" lol
 
exactly just like JFK alivyofanya kuhusu authorization ya vita ya Iraq.. ndiio maana criticism yangu inatokana na kuona usaliti wao!!

Kikwete amelet down watu wengi sana waliokuwa wanamsapoti na waliompigia kura (thanks GOD I am not one of them). Laiti angejua ni jinsi gani alikuwa anaungwa mkono na watanzania mwanzoni mwa uraisi wake na kufanya kila awezacho kukomesha ufisadi.

So far, I think the guy is beyond repair. Kama inafikia kuwa anapata bonge la pass toka kwa Jayson Kidd (Mwakyembe) na bado anashindwa kabisa ku-Vince Carter (kudanki) na kumtoa Chenge basi kuna mengi ya kusema kumhusu!
 
Nilikuwa hivyo, sasa siko hivyo wale ambao ndivyo mlivyo mnauwezekano mkubwa wa kuiendelea kuichagua CCM hadi pale mtakapokataa mawazo ya 'ndivyo tulivyo'. Miye niligundua mapema kuwa nilifanya makosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia!

Mimi sivyo nilivyo maana nilishayastukia mafisadi ya CCM tokea mwaka 95. Sikuyapigia kura mwaka huo na sijawahi kuyapigia kura tokea nianze kupiga kura. I guess now mimi sivyo nilivyo! Lol
 
Yapo mambo mengi katika mifumo ya nchi yetu ambayo yanahitaji mabadiliko makubwa. Mojawapo ya mambo hayo ni huu utaratibu au utamaduni wa kuteuana, si tu katika nafasi za ujaji bali pia hata ukuu wa mkoa, nafasi za wabunge kumi wateule wa Rais na nafasi nyinginezo.
Binadamu wengi kama sio wote, wana hulka ya ubinafsi.Hivyo viongozi wetu nao tunapowapa madaraka ya kuteua, haiyumkini wakatumia hulka ya kuangalia maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma. Ili kudhibiti hilo katika eneo hili la uteuzi, ni ama tuachane kabisa na utaratibu wa kuteua au tuwe na vigezo makini na vinavyothibitika kuhusu nani ateuliwe ngazi gani, akiwa na sifa zipi, kwa malengo gani na kwa muda gani.
Kadiri tutakavyoendelea kuwa na mfumo unaompa madaraka rais wa nchi kuteua watu bila kulazimika kuuambia umma aliowateua wana sifa gani za kuwastahilisha uteuzi huo,wataendelea kuteuliwa washikaji, washirika wa biashara fulani na kadhalika. Ni hadi hapo umma utakapokuwa na mamlaka ya kumtaka rais aeleze vigezo vya uteuzi wake, ndipo tutaondokana na kuteuliwa kwa watu kwa vigezo vya kujuana, kulipana fadhila na kulindana.

Laiti kama uteuzi ungeanza na hatua ya kusudio la kumteua mtu fulani kabla ya uteuzi kuthibitika, ili umma upate nafasi ya kuzipitia CV za wateuliwa watarajiwa, uadilifu wao na uchapakazi wao, na kama kweli hawana uhusiano wa namna yoyote ile na mteuaji.
Vinginevyo tuachane kabisa na uteuzi, watu waajiriwe kwa sifa zao kama ilivyo katika sekta mbali mbali za ajira.
ASOMAYE NA AELEWE
 
kwamba pamoja na maneno yako meeeengi, kumbe na wewe "sivyo ulivyo".. maana ungekuwa "ndivyo ulivyo" ungeipigia kura CCM.. do you agree? LOL

Come on Mwanakijiji...you know better. Hahahahahaaaa....kumbe na mimi maneno meeeeengi eeeehhh...?

On a serious note, we need to wake up the majority of the people to realize that we deserve better than what we have now. I know we can do it.
 
brutus upo wapi kuhusu mtiririko wa thread or arent they supposed kukaa kimya na kusoma or they'll be banned ??
 
Back
Top Bottom