Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,392
- 39,493
Kuna majaji ambao nina uhakika amewateua ndani ya miaka yake hii miwili ambao wananchi hawana budi kuwaangalia kwa ukaribu. Hofu yangu ni kuwa tunaanza kuona yale yanayotokea Marekani ambapo Marais wanashindana kujaza Majaji kwenye mahakama za federali wakitarajia kwamba endapo kesi fulani fulani zikifika huko mbeleni basi majaji hao wanaweza wakaamua kwa njia fulani.
Hii mara nyingi inafuatana na judicial philosophy ya jaji husika na rekodi yake hiyo. Hivyo Marais wa Demokrati watachagua majaji wanaoona kuwa Katiba ni "living document" ambayo inaweza kutafsiriwa kwa kufuata muda na situation na ambao wamepitia "litmus test" ya kama majaji hao wanahistoria haki ya utoaji mimba, mashoga, n.k Upande wa Repablikani wao wateuzi wao huangalia Katiba kama historical text ambapo waanzilishi wa Taifa walichotaka kusema kuhusu nchi kimeshasemwa na hivyo hawaoni "uhai" wa Katiba. Hawa wanatetea haki ya mtoto hata kabla ya kuzaliwa, wanapinga ndoa za mashoga n.k
Hofu yangu katika swali hili ni je yawezekana Rais Kikwete inawezekana ameanza kuweka watu kwenye nafasi ya Ujaji akiangalia huko mbeleni mahakama itakuwa na watu wake? Je, kesi ya Mkapa (kama iko) au ya Tangold, Meremeta, na Mwananchi zikifika itakuwaje pale ambapo Jaji mmoja (tunayefahamu) alikuwa ni wakili wa mojawapo ya makampuni? Je, anapomteua Masha mmoja wa mawakili katika kampuni ya IMMA ambayo imepokea fedha nyingi zisizoeleweka kutoka Tangold (wakati Masha akiwa wakili huko) na kumpa Uwaziri wa Jeshi la Polisi na Magereza anajaribu kuangalia mbeleni-just in case?
Je majaji wake wengine aliowateua wametoka wapi, na je huko nyuma waliwahi kuwa na uhusiano wowote na kashfa zinazoendelea?