Majadiliano: Wapalestina kupelekwa Sudan Kusini

Majadiliano: Wapalestina kupelekwa Sudan Kusini

Umkonto

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2018
Posts
3,115
Reaction score
5,365
Ikiwa ni kweli; Je, viongozi wa Sudan Kusini watajifunza kutokana na historia au watatanguliza njaa zao? Kipindi kile Janjaweed wanawaua Wasudan weusi, wanahistoria wakasema kuwa, Wasudan weusi ndiyo walikuwa wenyeji wa Sudan na ndiyo waliwakaribisha Waarabu lakini mwisho wa siku Waarabu wakawa tabaka tawala na kuanza kuwanyanyasa Weusi. Na Weusi wakaanzisha uasi na kupata uhuru mwaka 2011.

Habari kamili;
Sudan Kusini na Israel zinadaiwa kujadili mpango wa kuwapa makazi Wapalestina wa Gaza katika nchi hiyo ya Afrika inayokabiliwa na migogoro. Haya ni kulingana na vyanzo vitatu vilivyoliarifu shirika la habari la Reuters.

Vyanzo hivyo vyenye ufahamu wa suala hilo lakini vilivyozungumza kwa sharti la kutotambulishwa, vimesema hakuna makubaliano yaliyofikiwa lakini mazungumzo kati ya Sudan Kusini na Israel yanaendelea.

Vyanzo hivyo vitatu vimesema matarajio ya kuwapa Wapalestina hao makazi Sudan Kusini yaliibuliwa wakati wa mikutano kati ya maafisa wa Israel na waziri wa mambo ya nje wa Sudan Kusini Monday Semaya Kumba, alipofanya ziara nchini humo mwezi uliopita.

Hata hivyo maelezo ya vyanzo hivyo yanaonekana kutofautiana na wizara ya mambo ya nje ya Sudan kusini ambayo siku ya Jumatano ilipuuzilia mbali ripoti za awali kuhusu mpango huo na kuzitaja kutokuwa na msingi.

Wizara hiyo haikuweza kufikiwa kujibu madai hayo yaliotolewa jana na vyanzo hivyo.

DW Swahili.
 
Uzi tayari
 

Attachments

  • Screenshot_20250816-163507_Facebook.jpg
    Screenshot_20250816-163507_Facebook.jpg
    121.8 KB · Views: 16
South Sudan ni member wa EA Community. Soon, mafilisti tutawaona kwenye vikao na mikutano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. 50 yrs ahead there will be complete change in this region.
 
Back
Top Bottom