Majadala wa "Internship" na "starting salary"

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Ameandika jumanne mtambalike on twitter
Mjadala huu unakuaga na mihemko sana mara nyingi sipendi kujihusisha nao. Laakini ni mjadala muhimu sana.

Naomba nitoe busara yangu ndogo.

Baada ya kuangaika sana mwanzoni mwa miaka ya 2010s nikiwa na makaratasi tu bila uzoefu na ujuzi nilipata nafasi ya kibarua bandarini.

Wazoefu wa bandari wanaziita zile kazi "chondoma" na unalipwa kwa kitu kinaitwa "Take On" kati ya shillingi 5000 mpaka 10,000 kwa siku na siku nyingine haulipwi. Chondoma hachagui kazi Kuna siku unafagia mbolea, siku nyingine unapanga mafaili na saa nyingine unamnunulia bosi chai. Ukibahatika unakaa ofisini kama wazee wako wana network. Hakuna mambo ya "career path".

Nashukuru nilifanya kazi, nikaonekana na bosi wangu mmoja akanipa nafasi ya kufanya kazi kama "Data Analyst". Degree yangu ya Computer Science haikusaidia chochote kipindi nafanya chondoma ni ukaribu wangu na watu na utayari wa kujifunza ndio ulionitoa.

... chakusikitisha ilipofika muda wa kutangaza ajira rasmi nilipigwa chini..nikaamua nisogee zangu.. lakini at least nilikua nimepata kitu kwenye CV yangu. Ukishakua kwenye makali ni maumivu tu..utaamua yawe ya kiasi gani..gemu ya maisha ni ngumu.. mama alilia sana.. muda hakupita nilipata fursa sehemu nyingine.. mwenda bure sio mkaa bure..

Kwaground mambo ni tofauti sana. Ukipata fursa ya kutoka mgundini "kijiweni", toka katafute. Mwenda bure sio mkaa bure. Issue sio mshahara, issue ni malengo yako. Unaenda ofisini kufanya nini?

Kama malengo yako ni kukutana na watu, kuongeza ujuzi wako, na kufungua milango yako ya fursa, mambo yakikaa sawa usogee, nenda. Kama nikupata Pesa nyingi, subiri kazi ya hadhi yako itokee.

Mjadala huu ulikuja Baada ya mwandishi wa habari za michezo PRISCA KISHAMBA kupost tangazo la nafasi za kazi ambazo aliweka na mshahara kama ifuatavyo

JOB APPLICATION
KISHAMBA MEDIA is looking for

1. Content Creator
2 yrs Experience
=> Salary 400,000/= (Tshs)

2. Content Creator (Intern)
  • Experience 6 Month - 12Month
  • Any graduate, specified in Journalism

=> Salary 200,000/= (Tshs)

3. Project Coordinator (Intern)
- Experience Any within 1 or 2 companies

- Education: Diploma/Degree in Marketing & PR
=> Salary 200,000/= (Tshs)

SEND YOUR CV with Cover letter with vivid Past work you have done or been, through our email pkishamba@gmail.com

Thank you!

Na hiki ndio kilikuwa chanzo cha mjadala
Screenshot_2023-07-31-07-51-25-787_com.twitter.android.jpg
 
Back
Top Bottom