Maiti yageuka ng'ombe Tanzania

Mfano Mofu...Kwa akina Lumbanga mmmmmh hata ukinjenga nyumba ukimaliza tu kifo ukichelewa kuzikwa unageuka mnyama.....Pia sehemu za Mahenge pia hipo hiyo mdau wa Kilombero.
 
NYAMBO NGALI,ni Mwanga ata mimi nimeamini.

Leonard,

mwanga according to Kamusi ya Kiswahili sanifu , Taasisi ya uchunguzi wa Kiswahili Oxford University Press, Dar Es Salaam,2002 means

1. mtu afanyaye mazingaombwe ya uchawi usiku
2. mtu anayetembea usiku badala ya kulala
3. mtu anayecheza ngoma ya mahepe

Mimi niko kwenye kundi gani na kwa sababu zipi unaniweka kundi hilo
 
Ushirikina Upo tuu, hata huko Lindi kuna mtu aliwahi kugeuka simba na bado yupo mpaka sasa, ni simba asiye na madhara kwa watu wema.
 

Bila shaka unazungumzia gamboshi, au sio?
 

nimebakia nacheka peke yangu ...
 
kunani bunda
juzi kati mama kajifungua jiwe
nkasikia mtu kazaa kitimoto
leo kuna maiti imegeuka ng'ombe whats going on there?



 
khaaa nyie waongo na hivyo vya sukari vinatoka wapi?
mtageuka paka kwa uongo we haya wee


sawa sawa_yaani mpaka uende dukani kununua sukari ndio upate kipande ulicofungiwa sukari then ukisome...hebu wekeni hii habari hapa wakuu
 
Babu wa Loriondo anaweza kuwa na ufafanuzi kwa vile yeye huwa anaoteshwa... hakuna member wa JF jirani huko amuulize? Maana magazeti yameshajua kuwa akili zetu zimechoka kufikiri nazinapokea na kukubari chochote basi wanaleta chochote wanachoona watafanya biashara.
 
Atakuwa aliiba ng'ombe wa mnyantuzu huyo. Hao wanyantuzu huwa hawaoni taabu kukugeuza pusi, ngo'ombe au mbusi. Ni noma sana hao jamaa lakini pia ni wema na wakarimu sana.
 
Kweli nimeamini mtu akisoma saaaaaana badae anakuwa mjinga katika makabila yenu hakuna mila na desturi? Mambo kama haya yalikuwa yanafanyika au ni adhabu alikuwa anaadhibiwa mtu kutokana na kile alichokitenda kilichokuwa kinafanyika kinyume na jamii inayomzunguka na hilo tukio hufanyika ili iwe fundisho kwa waliobaki wasirudie tabia kama hiyo alokuwa anaifanya marehemu.Tusijidai kusoooma sana tukazisahau mila zetu. Mbona mtu huwa anapigwa kipapai mnaletewa huko hospitali na hayo maPHD na sayansi zenu mnagwaya???????
 
Acha bwana,mi nilienda kijiji fulani cha kabila la wanyamwanga huko mbozi,nikapewa onyo nikimuona simba kijijini mida ya jioni nisishtuke,huyo ni marehemu Sinkala,alifufuka akawa simba,ila huwa hana madhara yoyote.Wenyewe wakimuona wanampa vikuku na bata,akisha kula wanamwambia aondoke na anaondoka.
 
Tunaficha nini mkuu,ni hawa ndugu zetu wandamba.Kama umeshawahi kukaa na wandamba,maumbo yao juu ni wapana chini wembamba hali inayowafanya wafanane na simba.
 
Mioyo isiyo na imani na Mungu na iliyokata tamaa na maisha ni uwanja mpana sana wa kupandikiza imani za ushirikina.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…