Maiti ikitolewa nje hairudi ndani?

kanali mstaafu

JF-Expert Member
May 17, 2015
4,318
4,098
Kuna tukio limetokea juzi huku mtaani huku mtaani.

Kuna Dada mmoja kafariki sasa imefika mida ya saa 8 maiti ikatolewa kwa ajili ya mazishi.mara baada ya maiti kutolewa nje mvua ikaanza kunyesha ikabidi maiti irudishwe ndani...baada ya mvua kunyesha wakaanza kutoa jeneza ambapo lilibana mlangoni ikabidi mlango upanuliwe wakati mwanzo maiti ilipita bila kukwama,maiti ilipofikishwa nje mvua tena ikaanza wakarudisha tena maiti ndani.

Sasa ikaendelea kila walipokuwa wakitoa maiti nje mvua inaanza na wakirudisha tu ndani maiti basi mvua ilikuwa inakatika, ilipofika saa 1 usiku ikabidi wazike hivyohivyo huku mvua inanyesha na mpaka wanaweka jeneza kaburini kulikuwa na maji ndani ya kaburi yaliyofunika hadi jeneza ambapo waliamua tu kufukia hivyohivyo.

Baada ya mazishi nikasikia wazee wakinong'ona eti maiti ikitolewa ikazikwe haipaswi kurudishwa tena ndani hata kama kuna vikwazo gani inabidi wazike hivyohivyo...

Naomba mchango wenu wana jukwaa juu ya hili lililonenwa na wazee
 
Ni kweli kabisa. Kwa tamaduni zetu za kiafrika ni sawa na kurudisha tatizo ndani
 
Hiyo kitu nilishawahi kuisikia ni sawa na ikishapangwa starehe ya kufunga ndoa haitakiwi kubadirishwa labda Ade mtu wa jaribu sana
 
khaaaah izi mambo bhana ndomana wengine wanaamua kuchoma moto mfu tuu......BTW sasa umeshatoa unairudisha ndani kisa mvua..... labda jeneza lililoa likatanuka mana mbao ile
 
Dead and gone ndicho nichoamini mambo mengine ni mawazo ya binadamu waliobaki how come maiti awe na mbwembwe wakati hawezi hata kuongeza au kupunguza speed ya jeneza.
 
Back
Top Bottom