Maiti afufuliwa huko mkuranga pwani.... Milioni 15 zahitajika kwa mganga wa kienyeji ili kumrudisha

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,318
33,125
MAITI AFUFULIWA HUKO MKURANGA PWANI.... MILIONI 15 ZAHITAJIKA KWA MGANGA WA KIENYEJI ILI KUMRUDISHA KATIKA HALI YA KAWAIDA



BINTI aitwaye Nuru Omari anayedaiwa kufariki dunia mwaka 2010 ameibuliwa hivi karibuni wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani na mganga akiwa hai kwenye banda kuukuu.

Binti Nuru Omari aliyeibuliwa.
Tukio hilo limetokea kwenye Kijiji cha Kalole, Tarafa ya Kisiju, walayani humo.




Kwa mujibu wa baba wa binti huyo, Omari Salum, mwaka 2010 ndugu wa mkewe aitwaye Nyasenene aliyekuwa akiishi Charambe Mbagala, jijini Dar alifika nyumbani kwake na kuwaomba wampe mtoto wao kwa ajili ya kwenda kufanya kazi za ndani ‘hausigeli'.


Kijumba alimokuwa Nuru.
Baada ya binti huyo kufanya kazi kwa muda mfupi aliugua malaria, baba mtu akapewa taarifa na kufika Dar kwa ajili ya kumuona mwanaye aliyekuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar.


Mzee huyo amesema alikwenda Muhimbili na kufanikiwa kuzungumza machache na mwanaye huyo ambapo alikuwa akilalamikia maumivu ya tumbo.



Ndugu na majirani waliofika kumtazama Nuru.
Mzee huyo alisema ilibidi aondoke licha ya mwanaye kumtaka alale lakini kwa vile yeye ni mwanaume isingewezekana kulala hospitalini hapo.


"Kesho yake nilipewa taarifa kuwa mwanangu amefariki dunia usiku. Tulianza taratibu za mazishi na kumzika kwenye Makaburi ya Kichangani, Mbagala, Dar kutokana na kukosa fedha za kuusafirisha mwili hadi Mkuranga," alisema mzazi huyo




Mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Said Ali Ngaora ‘Dr. Lamba' anayeishi Mbagala Rangi Tatu, Dar alifika katika kijiji hicho cha Kalole mwaka huu na kuwaambia wananchi kuwa kijijini hapo pana mtu anaonekana alikufa na kuzikwa lakini bado yupo hai na amewekwa sehemu na kutaja gharama za kumtoa ni shilingi milioni tatu.



Mganga aliyemuibua Nuru.
Akielezea tukio zima Dr. Lamba alisema wananchi walimruhusu akaanza kazi kwa kushirikiana na wataalamu wenzake.


Dr. Lamba na timu yake walifanikiwa kumuibua msichana huyo anayekadiriwa kuwa na miaka 12-15 kwenye mji ambao hakuna mtu anayeishi akiwa ndani ya banda la kuku huku kukiwa na chungu chenye damu, asali na udongo ambavyo vilikuwa ndivyo vyakula vyake akiwa na muonekano wa kutisha kwa kuwa na nywele ndefu na chafu na kucha zikiwa ndefu mithili ya jini.




Baada ya kumtoa alipelekwa katika uwanja wa mpira kijijini hapo na kuogeshwa pamoja na kukatwa kucha kisha akapelekwa katika nyumba aliyofikia mganga huyo, hata hivyo hakuweza kuongea vizuri.




Kwa mujibu wa mashuhuda ulimi wa Nuru ulikuwa mzito na mpaka sasa anazungumza kwa vitendo kama bubu huku chakula ambacho ameanza kula vikiwa ni ugali na kuku, uji na juisi ya embe.


Mbali na shilingi milioni tatu za kutoa, mganga huyo anataka milioni 15 kutokana na dawa anazompa kwa ajili ya matibabu ili arudi katika hali ya kibinadamu .




Hata hivyo, baadhi ya ndugu wanaopinga kuwa Nuru siyo mtoto wao lakini baba mzazi anasema ni mwanaye kutokana na alama zilizopo mgongoni mwake na anafanana sana na mdogo wake.


Makamu Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ali Hassan Ndeko alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mpaka sasa wanakijiji wanaendelea kumiminika kwa ajili ya kumuona mtoto huyo akiwa chini ya uangalizi maalumu wa mganga huyo huku wakijitolea vyakula.

GPL:

MAITI AFUFULIWA HUKO MKURANGA PWANI.... MILIONI 15 ZAHITAJIKA KWA MGANGA WA KIENYEJI ILI KUMRUDISHA KATIKA HALI YA KAWAIDA - MPEKUZI HURU
 
Uchawi unasababisha umaskini na maisha duni. Nawachukia sana waganga wa kienyeji na wachawi. I real hate them in JESUS NAME. Nimeishi mkuranga wananchi wana maisha duni sana. Imani za kishirikina zimetawala no development at all.
 
Uchawi unasababisha umaskini na maisha duni. Nawachukia sana waganga wa kienyeji na wachawi. I real hate them in JESUS NAME. Nimeishi mkuranga wananchi wana maisha duni sana. Imani za kishirikina zimetawala no development at all.
Upo sahihi sana mkuu!
 
Hao watakuwa walimficha mtoto wa watu sasa wamemuibua ili wapate pesa. Wachawi na waganga wa kienyeji wajinga sana.
 
Hii ni network ya matapeli. Inajumuisha waandishi wa habari na waganga wa kienyeji! Watanzania wengi hulizwa na huu utapeli! Watu kama hawa ni kupeleka gerezani na kuwaonyesha shehemu ya kulima!
 
aisee!! Wiki kma 2 zlzopta nlkuwa huko kikaz, mbaya zaid tulcmama mbele ya hyo nyumba ilypgwa picha, mwenyeji wetu alitueleza hzo tetec za kuja mganga kufichua misukule,kumbe kweli! Sasa nmejua kwa nn kule hakuna maendeleo
 
Mh. waziri piga ban watu kama hawa wizarani kwako kwani wanataka umaarufu kwa kuleta utapeli usio na kichwa wala miguu. Kama kuroga karoga yeye ili alipwe hizo pesa.
 
Hivi uchawi/ndumba unafaida gani katika Uislamu? Aliye rogwa ni Muislamu, Mchawi ni Muislamu, Korani anayo tumia kupiga ndumba ni ya waislamu. I bet you, huko waendako nako watatoana roho kama wehu.

Biblia insema kuwa wachawi wote wataenda motoni

Na wakafuata yale waliyo zua mashet'ani kuuzulia ufalme wa Suleiman. Na wala Suleiman hakukufuru. Bali mashet'ani ndio walio kufuru, wakiwafundisha watu uchawi,na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili; Haaruta na Maaruta katika baabil. Wala hao hawakumfundisha yeyote mpaka wamwambie: Hakika sisi ni mtihani; basi usikufuru. Wakajifunza kwa hao wawili yale ya kumfarikisha mtu na mkewe. Wala hawawezi kumdhuru mtu ila kwa kutaka Mwenyezi Mungu. Na wanajifunza yatayowadhuru wala hayawanufaishi. Na hakika wanajua kwamba aliye khiari haya hatakuwa na fungu lolote katika Akhera. Na hakika ni kiovu mno walichojiuzia nafsi zao laiti wangelijua. Qur'an 2:102


Na lau kuwa wangeamini na wakaogopa, bila shaka malipo yatokayo kwa Mwenyezi Mungu yangekuwa bora. Laiti wangelikuwa wanajua! Qur'an 2:103
 
Hivi uchawi/ndumba unafaida gani katika Uislamu? Aliye rogwa ni Muislamu, Mchawi ni Muislamu, Korani anayo tumia kupiga ndumba ni ya waislamu. I bet you, huko waendako nako watatoana roho kama wehu.

Biblia insema kuwa wachawi wote wataenda motoni
Jina sio dini,tunao waganga wengi ni wakristo,wengine wanajiita maji marefu,nakujiita maprofesa,sehemu za bara kuliko na wakristo wengi,kila mara matukio ya uchawi yanatokeo,hivi karibuni kuna mchungaji wa kanisa alizikwa yuko hai,kwa kutuhumiwa amemuu mtu kiuchawi,wacha idadi kubwa ya vikongwe,wanawake wazee wanaouliwa kwa kuhisiwa ni wachawi.
 
Mijitu ya bara ni mijanja sana, wao huuwa na kumchuna binadamu ngozi ili iwe mitajiri ndo maana mijitu ya huko imeendelea sana, teh! teh! teh! teh!
Maeneo mengi ya bara kuna uchawiu wa kutisha,na wengine ni viongozi wa dini,wanazikwa hai.
 
Hivi uchawi/ndumba unafaida gani katika Uislamu? Aliye rogwa ni Muislamu, Mchawi ni Muislamu, Korani anayo tumia kupiga ndumba ni ya waislamu. I bet you, huko waendako nako watatoana roho kama wehu.

Biblia insema kuwa wachawi wote wataenda motoni

Msaidizi wa zamani wa Padri Katekisika,katika Kigago cha kanisa Katoliki kijiji cha Mkwajuni,Florian Mwamosi,70; amekufa baada ya kuzikwa akiwa hai,katka kaburi moja na mtuanayedaiwa kumuua kwa njia ya kishirikina.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya alikiri kutokea kwa tukio hilo.
Chanzo,gazeti la Mwananchi ijumaa june 28;2013
 
Hivi uchawi/ndumba unafaida gani katika Uislamu? Aliye rogwa ni Muislamu, Mchawi ni Muislamu, Korani anayo tumia kupiga ndumba ni ya waislamu. I bet you, huko waendako nako watatoana roho kama wehu.

Biblia insema kuwa wachawi wote wataenda motoni

Mkasa wa baba kumzika mwanawe akiwa hai,umezidi kuibuwa mapya ,baada ya mama mzazi wa marehemu Debora Riziki(3) kusimulia mkasa mzima.
Hii imetokea Mbeya,kijijini KwaleI Ibula kata ya kiwira,wilayani Rungwe.
Chanzo Mbeya yetu.
 
Imani za kishirikina zinashabihiana na umaskini wa kutupwa. Hiyo fedha ya kumfufua wanaitoa wapi kwanza hawa!
 
Rozina Mwadala,60,aliyezikwa akiwa hai,baada ya kutuhumiwa kujihusisha,na imani za kishirikina katika kijiji cha Malaba,Wilaya ya Mbarali,mkoani Mbeya,june 2.
Tukio hilo limekuja baada ya Mganga wa jadi kupiga ramli,kwamba marehemu aliyezikwa hai amesababisha kifo cha Frank Lingo,25;
chanzo chimbuko letu
 
Back
Top Bottom