Maisha yangu nimeyaharibu mwenyewe

SEHEMU YA TISA (9) Part 2 (in details)

Habari ndugu zangu wanaJF
Nimesoma maoni ya wengi na ntaendelea na story bila kuacha detail zote muhimu

Sasa nitaendelea na sehemu ya yule binti wa kanisani sambamba na yule bwana mdogo ambaye Baba yake alitokea kunikubali sana.

Tuendelee sasa….

Wakati nikiwa najiandaa na mtihani wa NECTA (ilikua imebaki kama miezi miwili hivi) kuna siku niko bwenini simu yangu iliita na ilikua namba ngeni lakini baadae niliitambua sauti kuwa ilikuwa ya yule binti wa kanisani (Tumwite mama mchungaji) hili jina hata shule walikua wakimuita hivyo.

Alipiga simu akimuulizia mdogo wake flan wa O-level kama ntaweza onana nae kesho nimpe simu waongee. Mama mchungaji alikua kashamaliza form four kwa wakati huo ( System ya zamani olevel walikua wanamaliza mwezi wa 10 hivi then advance tulikua tunamaliza mwezi wa 5) naamini wengi mnakumbuka.
So mama mchungaji hakuwepo shule tena ila nilikua nafahamiana nae vizuri tu kama nilivyowaambia nilikua church boy wakati fulani shuleni.

Kwa kunitazama hivi nilikua kijana mstaarabu sana, hii nasikia hadi leo watu huwa wanasema. Sasa mama mchungaji alikua anapenda kunishirikisha sana mambo ya biblia sana na nilikua nikimsikiliza, alikua pia na ushawishi mkubwa sana kwa wanafunzi kutokana na tabia yake njema sana.
Kukazia tu, mama mchungaji alikua mzuri jamani, Mchaga flani aliyekulia Mbeya.

Turudi kwenye simu yake sasa, tuliongea sana siku hiyo na nikamuuliza alitoa wapi namba nae akaniambia aliiomba kwa binti fulani walimaliza nae (nilikua mtu wa totoz so namba zangu wengi walikua nazo). Baada ya maongezi mengi na mama mchungaji basi tulikubaliana tutakua tukiwasiliana.

Mawasiliano yaliendelea na mama mchungaji alionyesha kunielewa na mimi nilikuwa na hisia hizo pia. Nilivutiwa sana na tabia yake. Ni aina ya mwanamke ukiwa nae huwezi kuwa na stress. She is amaizing kwakweli.

Baada ya wiki kadhaa mbele, mimi na mama mchungaji tukawa wapenzi ila ndo kwenye simu sana maana alikua home mimi niko shule. Tulipanga ntakapomaliza mitihani basi kabla sijarudi Dar tutaonana tushinde siku nzima. (Mama mchungaji alikua anakaa Tukuyu mjini). Amelelewa na baba yake mzazi na mama wa kambo. (Mama yake alifariki miaka mingi nyuma). Baba yake ni mchungaji kweli.

Maisha ya shule yaliendelea na wakati huu nilikuwa busy sana na masomo nikiwa na ndoto ya kufika chuo kikuuu. Matokeo ya Mock yalifanya nijitambue na kuanza kukaza buti.

Niwarudishe nyuma kidogo maana kuna mdau aliuliza kama nilikua narudi Bukoba.
Maisha yote ya Advance sikuwahi kurudi Bukoba. Ilikua likizo nakuja Dar na wakati wote huo B.mkubwa alikua anahakikisha nasoma tuition wakati wa likizo.
So nilipokua narudi shule, almost topic zote mi nilikua nishasoma huko likizo. Advance napo sikuwahi teseka kwa kukosa mahitaji ya muhimu, isipokuwa nilikua natumia oesa vibaya kwenye kamali, Disco vumbi na mara chache sana nilikua nikinywa pombe wakati wa disco.
So nilikua nishakua kijana wa Dar na Mbeya

Kula tulipokua tukifunga basi lazima twende Mbeya mjini, tukale maisha club alafu kesho ndo safari kwenda Dar.


Turudi kwa mama mchungaji, penzi letu lilikua la moto sana, simu nyingi usiku na sms kibao na nilimpenda yule binti.

Tulifanya mtihani salama na vitu vyangu kama Godoro, Blanketi na vingine vyote nilimwachia yule bwana mdogo ambaue baba yake ananikubali sana.
Yule Baba aliniletea kuku watatu kama asante ya kukaa na mwanae vizuri na pua kama zawadi kutokana na maisha ambayo niliishi na yule mzee ( nilikua weekend nnapoenda mtaani lazima nipite kwake nimsalimie yeye na familia, niaga kuondoka lazima anifungie maparachichi na vitu vingine vya kula) niliipenda sana ile familia sanaaaa. Bwana mdogo yule alikua kijana asiye na mambo mengi, alipenda sana shule na kila nilipokua napata nafasi tulishauriana mengi kuhusu maisha.

Ntatoa code ya shule niliyosoma maana naona wengi washaijua. Nimesoma shule iko ndani ndani sana inaitwa Lufilyo

Niliondoka shule baada ya siku 2 nilipomaliza mtihani wa NECTA, tukaoanda canter kama kawaida safari moja kwa moja tukuyu.

Nilishapanga na mama mchungaji kuwa siku hiyo ntalala tukuyu na ntaondoka kesho kuelekea mbey mjini ili keshi kutwa nirudi Dar.

Nilifika Tukuyu kama saa nne hivi asubuhi na mama mchungaji alikuja pale lodge nilipofikia ila kuingia aligoma. Nilitoka nikaenda kumwona, tuliongea sana na baadaye nikamsindikiza then nikarudi lodge.

Pale lodge sikuwa mwenyewe, nilikua na marafiki zangu kadhaa tushaoanga lazima jioni tukamwagilie moyo.
Yule dreva tax kama mnakumbuka alinipiga nauli day 1 nimefika Tukuyu alishakua mshikaji wangu sana na kila nilikua nikifika Tukuyu yeye ndo anakuwa mwenyeji wetu wa kutuonyesha machimbo.

Saa tisa mama mchungaji alikuja tena na this time nilimwomba aingie ndani. Tuliongea mengi, tulikiss sana na hatimaye aliamua kunitunuku tunda (baada ya mtafutano mwingi)

Mama mchungaji alikua bikra kabisaa kama ilivyokua kwa Clara. Jioni nilimsindikiza home hakua na hali nzuri sana lakini hakukuwa na namna. Tulipeana ahadi nyingi za kuoana mbeleni na kiukweli sikua namdanganya, nilimpenda sana yule binti.

Maisha ya kwao mama mchungaji yalikua na challenge kidogo, hakuwa anatokea familia bora alafu yule mama wake wa kambo alikua akimpiga matukio mengi sana. Hivyo mama mchungaji alikua akiniona kama mfariji wake mkuu, na nilikua nikifanya hivyo. Nilimpenda sana na kumjali sana.

Wakati nikiwa advance nilijiunga na mtandao wa facebook na kiukweli nilijipatia umaarufu mkubwa sana facebook, kipindi kile ukikuta mtu ana friends 5000 huyo ni noma na ndo ilikua limit. Baada ya hapo hata friend request zilikua zinagoma unaambiwa mtu huyu kafikia limit.

So upendo wangu kwa mama mchungaji ukafanya hadi nimpost facebook.
Ilikua kosa maana wale watumishi sasa (wanafunzi waliokuwa wakusali sana na mama mchungaji) wakaanza kumjaza maneno kuwa umekuaje awe na mtu kama mimi, Wale jamaa walikua wanajua code zangu nyingi akiwemo HP (Kiranja mkuu)

Nakumbuka wakati tuko shule HP alishatuita akasema sisi ndo tutaaibisha shule kwenye matokeo ya NECTA sababu ya tabia zetu.
HP pua alikua mwenyekiti wa CASFETA ambapo mama mchungaji alikua akisali hivyo wanajuana vizuri sana maana mama mchungaji alikua kiongozi pia.

Presha ilikua kubwa kwa mama mchungaji kwamba aache kuwa karibu na wahuni (Mimi) kwa ufupi alipokea simu nyingi zikinielezea vibaya

Personality yangu ni kijana flani mpole sana unless ujue mambo yangu kiundani, ila watu wengi ukiwaambia hata nakunywa pombe watabisha.

Mama mchungaji hakuniacha na nilimuhakikishia kwamba wanayosema mengine ni kweli mengine sio na niliahidi kujirekebisha, na yeye hakuwa na shida alikubaliana na mimi.

Matokeo ya form 4 yalishatoka wakati hui na mama mchungaji hakufanya vizuri sana, alipata 4 ya 26 ila combination hazikubalance. So alikua na option ya kwenda kusoma chuo cha ustawi Iringa pale.

Mchakato wa kwenda chuo ulimchosha sana kwani nyumbani kwao uchumi haukua mzuri na mimi sikua na msaada zaidi ya kumpa pole na kumfariji.
Wakati huo wote mi nilikua Dar na maisha yalikua yanaenda vizuri tu nikiwa nasubiri matokeo.

Mama mchungaji alifanikiwa kwenda chuo japo kwa kuunga unga sana na mzee wake alimwona lecture mmoja pale awe anakaa kwake (hakuwa na uwezo wa kulipa Hostel).
Yule lecture alikua ni mwanamke kwakweli alimpa shida sana mama mchungaji, kazi nyingiii na matatizo mengine (mnaelewa ambao mmeishi kwa watu).


Mama mchungaji alikua mvumilivu sana na hakuwahi kusema hata kwa Baba yake, alikua akiniambia mimi tu. Nilikua faraja yake na kwakweli kwa aliyopitia pale, inahitaji ujasiri sana kuendelea kuishi na yule Lecture.

Kwa upande wangu matokea yalitoka na nilifaulu kwenda chuo. Nilichagua course ya Mass communication ingawa home B. Mkubwa hakunielewa kabisaa alisema ntakosa mkopo bora nisome education.
Sikua na wito wa ualimu at all so niliwatafuta kaka zangu wale wa UDSM (mtoto wa aunt wa bukoba) na kaka yangu kabisa wakati huo yeye alikua UDOM anasoma shahada ya kwanza ya Udaktari wa binadamu.
Tulifanikiwa kumshawishi aunt na kwenye kuchagua vyuo education niliweka ya mwisho kabisaa. Nikachagua Mass Comm~SAUT MWANZA then Health system management~Mzumbe na kuendelea

Nilichaguliwa SAUT Mwanza na nilifurahi sana maana nilikua napenda kusoma mambo ya uandishi wa habari.

Mama mchungaji alifurahi sana japo alikua na huzuni kwamba naenda mbali zaidi lakini nilimwambia hakuna shida tupambanie future yetu.

Siku zilisonga na nilitakiwa kwenda chuo sasa, wakati huo nawaza kurudi mwanza nikawa namkumbuka mpenzi wangu wa mwanza Clara.
Nilitakiwa kwenda Bukoba kwanza kufata cheti changu cha o-level (transcript) kwa ajili ya kuapply mkopo.


Safari ya Dar - Bkb ilianza na nilifika salama kesho yake mchana, nilipata cheti changu, aunt wa Bk alifurahi sana kuona naenda chuo lakini kiherehere kikanituma niulize kuhusu Jane na nikaambiwa ana kama wiki 2 amerudi kwao na anakaribia kujifungua mtoto wa 2 (Jane alikua ameolewa na yule jamaa anayefanya kazi dar ila kwao ni Bukoba)

Nilienda kwao na Jane na mdogo wake alinofungulia mlango, nikakaa sebuleni kumsubiri Jane. Alikuja baada kama ya dak 5 na alikua anaonekana kuchoka, mimba yake ilikua kubwa. Hakuwa na hasira na mimi tena, tulipiga story nyingi nikampongeza kwa hatua aliyofikia nae akanipongeza sana aliposikia naenda chuo.
Niliondoka kwao na kurudi home na mambi mengine yaliendelea..

Nilifanikiwa kurudi dar salama na nikaendelea na mchakato wa kuapply mkopo. Siku zikasonga hatimaye nikaenda chuo. Ada ya kuanzia na matumizi yoote alinipa b.mkubwa hela (majibu ya mkopo kwa kipindi hiki yalikua yanatoka wakati watu washaanza kureport vyuoni)

Safari to Mwanza ikaanza na nilifikia kwa mzee pale Mwanza, kesho yake nikaenda chuo kufanya reg na utaratibu mwingine.
Nilitafuta hostel za nje (SAUT MWANZA ni miongoni mwa vyo vyenye hostel za nje nzuri kuliko vyuo karibia vyote Tz) hapa watu waliosoma SAUT watadhibitisha hili.

Kuna rafiki yangu mmoja nilisoma nae advance nae alichaguliwa Mass comm ila alikua hajafika chuo. Tulikubaliana kukaa wote na pesa ya awali nililipa mimi then yeye atakuja amalizie.

Nilikamilisha taratibu za malipo yote chuoni, hostel na kila kitu kilikua poa na nilikua tayari sasa kuanza maisha mapya ya chuo.
Mzee alinipa pesa kidogo pia.


TUTAENDELEA…

Maoni yako ni muhimu na nasoma yote ili niweze kuendelea na story yangu
Hii Haiba yako unayozungumzia umenikumbusha mimi wakati nasoma haiba yangu ilikuwa ya upole mnoo ikitokea kosa nikiwemo ndani Mwalimu anaweza wasamehee wote akiamini ni bahati mbaya
Ila ukweli mimi ndo nilikuwa kiongozi wa magenge yote ya kihuni shuleni,kutoroka kwenda night club,kufanya biashara ya kuuza Mandazi,samaki ndani ya shule(ilikuwa tunaenda nunua mtaani mandazi sh 50 nakuja uza 100)ulevi mixer mjani

Ila hadi nahitimu sikuwa shikwa kwa kosa lolote la utovu wa nidhamu na Crew yetu walikuwa wanadakwa na kupewa suspension karibu kila mara

Ilifika mahali washakji wakahisi natumia labda uchawiimaana haikuwa kawaida kuna muda hadi mimi nilikuwa najishangaa nawezaje kufanya yote yale bila kudakwa,nawezaje toka shule na kupanda bus hadi mjini siku ya ijumaa tunaenda club tunalala huko huko tuanrudi jmosi jioni bila kudakwa ajabu zaidi siku ambayo sitatoroka wakatoroka wengine ndo siku itapita Rollcall kalii sana na wanabainika,,,nilikuwa na machale ambayo siwezi yaelezea

Siku ambayo hadi mimi mwenyewe nilijikubali na wanafunzi watukutu walikubali nina machale sana hadi ikapelekea wakitaka toka mimi ndo naongoza msafara ilikuwa siku ya Sokoo tukapanga twendeni jioni baada ya masomo kama kawaida inafika ule muda nikawaambia washkaji leo tusitoroke na nguo za Home tuvae Uniform alafu kama ilivozoeleka wengi wakitoroka mnapita njia za chocho nikawaambia tupiteni Main Road jamaa wengine wakagoma ila mmoja akakubali tukaambiana tukutane sokoni sisi hao Main road na nguo zetu jamaa wakala chocho tunafika sokoni hatuwaoni tukala supu chapati,mixer kitimoto(wakati ule kg 1= 2,400) tukanunua mavitu ya kurudi nayo shule kuuza mara kidogo tunamaliza maliza shoping mwalimu huyu hapa akatuuliza vipi tukamwambia tumepewa Pass akaendelea na yake sisi hao tukarudi shule kwa Main road kukaribia fensi ilikuwa ya Seng'enge tukapenya kama kawa hao bwenini kufika tunasikia story jamaa wamepitishwa wamefungwa mashati kumbe huko chocho walikutana na Headmaster muda huo wapo staff wanachezea Fimbo toka siku ile nilionekana kama mchawi au nabii

Shule ilikuwa naishi kitajiri sana sababu ya faida kubwa ya biashara ya mandazi,,chapati,,samaki na kitimoto
 
Hii Haiba yako unayozungumzia umenikumbusha mimi wakati nasoma haiba yangu ilikuwa ya upole mnoo ikitokea kosa nikiwemo ndani Mwalimu anaweza wasamehee wote akiamini ni bahati mbaya
Ila ukweli mimi ndo nilikuwa kiongozi wa magenge yote ya kihuni shuleni,kutoroka kwenda night club,kufanya biashara ya kuuza Mandazi,samaki ndani ya shule(ilikuwa tunaenda nunua mtaani mandazi sh 50 nakuja uza 100)ulevi mixer mjani

Ila hadi nahitimu sikuwa shikwa kwa kosa lolote la utovu wa nidhamu na Crew yetu walikuwa wanadakwa na kupewa suspension karibu kila mara

Ilifika mahali washakji wakahisi natumia labda uchawiimaana haikuwa kawaida kuna muda hadi mimi nilikuwa najishangaa nawezaje kufanya yote yale bila kudakwa,nawezaje toka shule na kupanda bus hadi mjini siku ya ijumaa tunaenda club tunalala huko huko tuanrudi jmosi jioni bila kudakwa ajabu zaidi siku ambayo sitatoroka wakatoroka wengine ndo siku itapita Rollcall kalii sana na wanabainika,,,nilikuwa na machale ambayo siwezi yaelezea

Siku ambayo hadi mimi mwenyewe nilijikubali na wanafunzi watukutu walikubali nina machale sana hadi ikapelekea wakitaka toka mimi ndo naongoza msafara ilikuwa siku ya Sokoo tukapanga twendeni jioni baada ya masomo kama kawaida inafika ule muda nikawaambia washkaji leo tusitoroke na nguo za Home tuvae Uniform alafu kama ilivozoeleka wengi wakitoroka mnapita njia za chocho nikawaambia tupiteni Main Road jamaa wengine wakagoma ila mmoja akakubali tukaambiana tukutane sokoni sisi hao Main road na nguo zetu jamaa wakala chocho tunafika sokoni hatuwaoni tukala supu chapati,mixer kitimoto(wakati ule kg 1= 2,400) tukanunua mavitu ya kurudi nayo shule kuuza mara kidogo tunamaliza maliza shoping mwalimu huyu hapa akatuuliza vipi tukamwambia tumepewa Pass akaendelea na yake sisi hao tukarudi shule kwa Main road kukaribia fensi ilikuwa ya Seng'enge tukapenya kama kawa hao bwenini kufika tunasikia story jamaa wamepitishwa wamefungwa mashati kumbe huko chocho walikutana na Headmaster muda huo wapo staff wanachezea Fimbo toka siku ile nilionekana kama mchawi au nabii

Shule ilikuwa naishi kitajiri sana sababu ya faida kubwa ya biashara ya mandazi,,chapati,,samaki na kitimoto
Ulikuwa legend kweli mzee
 
Nakupa elimu ndogo kabisa, Ni baba yenu ndie alikuwa anatafuta hela za kuwalipia ada shuleni, nguo, chakula, n.k. mama yenu alikuwa anapewa ila mkimuona anavyowalipia / kuwapa mnadhani ni zake.

Nani kama mama ni misemo ya watoto / vijana ambao bado hawana familia zao kujua mfumo kamili wa jinsi mambo yanavyokwenda
Kwa mujibu wa muendelezo wa hii story inaonyesha ni kweli baba yao hakuwa na mchango mkubwa maana alishindwa kuilea familia baada ya mke wa kufa ikatawanyikia kwa mashangazi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom