Maisha yananigonga

Maisha yananigonga

Nafikiria hata nijiue au nikimbilie kusikojulikana, nadaiwa kodi mwezi ujao na sijui nitalipa vipi, kazi nafanya haiwezi kulipa madeni yote, au nimefikiri niachane na mke wangu tatizo ana watoto...
Kuanza upya sio ujinga, anza upya kama ndio unatoka chuoni. Rudisha mke kwao au kwenu kwa muda.

Toka hapo unapoishi tafuta sehemu nyingine ya chee anza maisha ya kujibana kama upo Dar amia sehemu zenye ushamba ila zina utulivu wa maisha kama mbezi kimara, kiluvya, bunju, mbagala nk.

Anza upya maisha ni ya ajabu sana inawezekana kuna kitu yanataka ukiachie wewe unakipenda ndio roho yako. Siku ukikiachia ndio utaona mabadiliko.
 
Nafikiria hata nijiue au nikimbilie kusikojulikana, nadaiwa kodi mwezi ujao na sijui nitalipa vipi, kazi nafanya haiwezi kulipa madeni yote, au nimefikiri niachane na mke wangu tatizo ana watoto...
Na wale malaika wako ulosema wapo kichwan.

Maisha hayana lelemama wala mchezo ni kupambana asubui jion hakuna kulaza damu, Hakuna wa kumaliza shida zako zaid ya upambanaji wako.
 
Nafikiria hata nijiue au nikimbilie kusikojulikana, nadaiwa kodi mwezi ujao na sijui nitalipa vipi, kazi nafanya haiwezi kulipa madeni yote, au nimefikiri niachane na mke wangu tatizo ana watoto...
Maisha Yana changamoto kwa kila mtu, hafi mtu, ila cha moto tutakiona.

Jipe muda, kama ulikuwa unapoteza muda na pesa kwa waganga na wanawake, ndio mwanzo wa kubadilika. Fanya kazi kwa bidii, tafuta fursa za ziada kuongeza kipato, ikiwezekana na Mama watoto naye aongeze nguvu, maisha yenu wote.
 
Back
Top Bottom