Maisha yanachanganya sana

Ahsante sana mkuu nitafuata ushauri wako ubarikiwe sana kwa kuwa na mawazo mema
 
We acha tu ndugu yangu kuna watu wana mioyo ya ajabu sana
 
Mtaji wa masikini ni nguvu zake mwenyewe, Anza kutafuta Cha kwako usisuburi ndugu yako akupe mtaji,ushauri wa ndugu yako ni mzuri anataka ujue uchungu wa kutafuta maisha, kwani yeye alivyofanikiwa alipewa mtaji, unakula na kulala na wala hulipi bili yoyote. Asee chakarika
 
1.unakunywa pombe?,isije kuwa ukishika 30000 unashtua double kick kuweka akili sawa?
2.nakushauri tafuta wasanii wa uchoraji, culture ujifunze

.sekta ya utalii inaenda kukua.ANZA SASA UTAKUJA KUNISHUKURU BAADAE
 
Ndio hataki kumpa sasa na kamwambia ajiongeze .. anafanyaje
Lakini pia inategemeana na aina ya ndugu na ukaribu uliopo Kati yake na ndugu yake kasema ni Kaka ko hajatuambia ni Kaka kivipi inawezekana anamuita Kaka kwa Kuwa wametoka Kijiji kimoja or mtoto wa shangazi aliyezaliwa na Bibi waliyeshea baba hahahahaaaaa.... Hizi ni kawaida Sana Kaka. Kikubwa ye ajiongeze mwenyewe na asimame kwa miguu yake..
Ashasema ana magari matatu kwa kwa nini asimtafutie hata leseni awe dereva wake
 
Umeomba jambo jema. Angekuwa mwingine angekuja kulalama
 
1.unakunywa pombe?,isije kuwa ukishika 30000 unashtua double kick kuweka akili sawa?
2.nakushauri tafuta wasanii wa uchoraji, culture ujifunze

.sekta ya utalii inaenda kukua.ANZA SASA UTAKUJA KUNISHUKURU BAADAE
SitumiI kilevi chochote ndugu yangu nipo very smart hata ndugu yangu analijua hilo
 
Ni kaka yangu tumbo moja namaanisha ni baba na mama mmoja na ana gari tatu za school bus na noah moja ya kutembelea na hizo school bus zote kaajili watu lakini mimi ndugu yake nipo mtaani naangaika
 
Yaani ujitafutie bila mwongozo wake anazingua huyo kaka yako


Mambo sahiv sio rahisi kama zamani
Ndio sasa kashaamua mi nitafanyaje na jamaa ni mtu mwenye taasisi kubwa ya kielimu kwa watu wanaofaham kuwa ni kaka yangu wananiita boss, wakishua ila hawajui ugumu wa maisha naopitia. Kifupi sijawahi kupewa hata elfu 10 tu ya kununua suruali toka nifike hapa dar, kuhusu mavazi yote najitegemea na pesa ya kula huwa naachiwa kiduchu sana na kingine huyo kaka yangu bado ajaoa tunaisho wawili tu mimi na yeye. Najiskia vibaya sana maana mtaani watu wanajua nina hela nyingi kumbe sina hata shilingi sometime naona hata aibu kujichanganya hapa mtaani kupiga vibarua coz cv ya brother inatisha na itafanya jamii ishangae kuona mafanya kazi vibarua wakati ndugu yangu yupo njema.
Kingine pamoja nayeye kumiliki idadi yote hiyo ya magari ajawahi kuniruhusu hata kujifunza kuendesha gari mpaka watu huwa wanamwambia kwanini usimuachie dogo mashine nae avimbe mtaani siku moja moja anaishia kucheka tu.
 
Ni kaka yangu tumbo moja namaanisha ni baba na mama mmoja na ana gari tatu za school bus na noah moja ya kutembelea na hizo school bus zote kaajili watu lakini mimi ndugu yake nipo mtaani naangaika
Fanya nilichokushauri, kama unajuwa kuendesha gari na pikipiki ingia mtaani utanikumbuka.

Bodaboda sasa hivi ndio wanaotesa mtaani, wana quick money za kuhonga kina Mwajuma nchokonowe.

Ukiwa driver ni rahisi kupata mishe za driving project kila siku zipo zinahitaji madereva.

Cha msingi sasa hivi upate take off kianzio kwanza.

Halafu ninayekushauri mwenzako ni jobless nina mke na watoto wanasoma English medium, kuna bill ya Dawasa, luku, Dstv, takataka, ulinzi shirikishi na daily nourishment.

Bongo ya sasa usiwaze kuajiliwa, ajira itakufuata ukiwa tayari upo golini kwako maisha yanasonga.
 
Inasikitisha sana, labda anakupima uvumilivu wako, akili na upambanaji wakati anakuandalia kitu kikubwa cha kukutoa coz naamini damu nzito kuliko maji.
 
1.unakunywa pombe?,isije kuwa ukishika 30000 unashtua double kick kuweka akili sawa?
2.nakushauri tafuta wasanii wa uchoraji, culture ujifunze

.sekta ya utalii inaenda kukua.ANZA SASA UTAKUJA KUNISHUKURU BAADAE
Nimepiga industry ya utalii kwa miaka mingi sana.

Hapa Dar hakuna duka lolote la Arts kulishinda duka la All African Arts la mwenge.


Nimefanya nao biashara pia hawa jamaa Waitaliano lakini ndio wazungu wa kwanza kushindwa kunilipa deni la pesa mbuzi tu mpaka nimeamuwa kusamehe hilo deni, maana mzigo niliowapa ulikwenda duka lao la Mlimani city na biashara imekuwa ngumu wamefunga duka wamerudisha fremu.

Kwahiyo nakielewa vizuri unachomshauri uhalisia haupo hivyo, nenda pale Tingatinga Haile selassie road karibu na mambo club waulize wale jamaa wa Arts wakueleze mambo yalivyo magumu mpaka wengine wamebadiri fani.
 
Kaka kuhusu udereva wa gari bado sijafanikiwa kujifnza ila piki piki naifahamu atleast lakini ni kazi ambayo huwa siipendi kutokana na changamoto zake kwanza ilishamuuwa jamaa yangu wa karibu juzi kati pia kuna mwanangu alikodiwa kwenda buguruni kumbe ni wezi kufika huko jamaa ile kupaki tu akaona makundi ya watu yanaibuka na mapanga, ile jamaa kutaka kuchomoka yule aliempakia akamuwahi akampiga bapa la mgongo ajakaa sawa akapigwa bapa la kichwa akazimia jamaa wakachukua chombo navyokwambia mshikaji saiz yupo polisi boss wake kamuweka ndani akiamini kwamba yeye ndio kacheza mchongo. Binafsi hiyo kazI ya boda boda huwa siitaji kufanya
 
Hakuna Jiji hatari Africa na huenda duniani kwa ujumla kama City of Johannesburg, lakini watu ili wasurvive maisha nimeona pale wageni wengi tu wanachangamkia kazi za security ambayo ni most dangerous job katika mji ule maana wakija huwa wanauwa tu.

Successful is for risk takers.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…