Maisha yanachanganya sana

Maisha yanachanganya sana

Melancholic

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
3,545
Reaction score
6,499
Daaah!! Maisha yanachanganya sana.

Nipo Dar takriban miez 6 sasa nililetwa na ndugu yangu toka mkoani kwa ajili ya mchongo fulani ila kwa bahati mbaya mambo hayakwenda kama tulivyopanga nikawa nimefeli.

Ndugu yangu sio kinyonge ni mtu mwenye maisha yake safi tu sio tajiri ila ana magari kama matatu hv na taasisi yake inayojishughulisha na masuala ya elimu.

Sasa Baada ya ule mchongo kufeli ndugu yangu huyo jana akaniweka chini akaniambia, "Mdogo wangu nishakuleta mjini tayari na mji ushaujua sasa usikae tu home inabidi ujichanganye hata mimi nilianzia maisha duni sana nililala nje lakini leo mambo yangu yamenyooka hivyo na wewe anza kujitafuta mapema, kuhusu kulala nitakusimamia mimi ila vitu vingine inabidi ujitafutie mwenyewe ili akili yako ikae sawa na pia uanze kujitegemea mapema maana ushakuwa mtu mzima, Sifanyi hivi ili nikutese hapana nafanya hivi ili nikusaidie na usiwe tegemezi.

Nikamwambia sawa kaka nimekuelewa wazo lako nitalifanyia kazi.

Sasa ndugu zangu hili suala nimelileta kwenu mnisaidie idea, mawazo yoyote ni vipi nitaweza kusurvive hapa mjini, hata kama kuna viwanda vinavyotoa kazi za kulipwa kwa siku mnielekeze vinapatikana wapi. Maana mimi bado sijawa mwenyeji sana hapa jijini. Kiufupi ni kwamba sichagui kazi yoyote ili mradi tu nisiwe nimevunja sheria za nchi.

Naombeni mawazo yenu ndugu zangu kiukweli napitia nyakati ngumu sana, sijui nianzie wapi kutafuta hata pesa yakula natanguliza shukrani na karibuni kwa mawazo yenu.
 
Miezi yote 6 ulikuwa unachezea remoti ya tv tu sebuleni?

Jifunze pikipiki muombe akufadhili pesa ya driving license, chukuwa pikipiki ya mkataba tafuta kijiwe ingia mtaani.

Mengine utajiongeza changamsha akili.
 
Sina connection na Wala sijawahi kuishi dar ila Nina experience na aina hiyo ya maisha jaribu kufanya haya yafuatayo pengine unaweza pata mwanga ingawa pia Kila mtu ana bahati yake

1. Toka tembea.... Kuna msemo mguu unaotoka ndio hurudi na baraka na wehenda husema riziki ya mbwa iko miguuni mwake...
Riziki haitokukuta umelala ndani au mekaa unatazama tv liziki iko nje Toka ndani tembea nje huko utakutana na hivyo viwanda unavyoviulizia, utakutana na mafundi mwashi wakitaka vibarua, utakutana na wabeba cargo, wapiga debe, nakadhalika.... Huko ndio utajichanganya sasa

2. Ongea na watu vijana au Rika lako
Tafuta marafiki au washkaji Rika lako ambao unaona wanajishughulisha kwa shughuli kama hizo nlizoorodhesha.. ongea nao fatana nao Wala usijifanye we wakishua na usiwaeleze habari za mafanikio ya Kaka yako... Changamana nao kama mtu asiye na mzazi au mlezi. NOTE Kuwa makini na tabia zao pia maana wengine hawana tabia njema

3. Waza kufanya zaidi ya hilo tandiko alilokupa
Amekupa malazi ko usibweteke ukasema natafutia tumbo langu tu waza kuwa atakutoa hata kwenye hilo tandiko ko unakazi ya kutafuta sehemu ya kulala pia. Namaanisha weka akiba hata kama ni kidogo ili ukiweza upate kamtaji ka kuuza hata maji dar.

Kwangu ni hayo tu na wengine watakuja kuongezea
 
Kama upo fizikali fiti nenda Buguruni pale kiwanda cha Bakhresa huwa wanachukua vibarua kila siku asubuhi, Ila narudia tena KAMA UPO FIZIKALI FITI. Kila la kheri.
Nipo fizikali fiti kaka na malipo yao huwa yapoje
 
Sina connection na Wala sijawahi kuishi dar ila Nina experience na aina hiyo ya maisha jaribu kufanya haya yafuatayo pengine unaweza pata mwanga ingawa pia Kila mtu ana bahati yake
1. Toka tembea.... Kuna msemo mguu unaotoka ndio hurudi na baraka na wehenda husema riziki ya mbwa iko miguuni mwake...
Riziki haitokukuta umelala ndani au mekaa unatazama tv liziki iko nje Toka ndani tembea nje huko utakutana na hivyo viwanda unavyoviulizia, utakutana na mafundi mwashi wakitaka vibarua, utakutana na wabeba cargo, wapiga debe, nakadhalika.... Huko ndio utajichanganya sasa
2. Ongea na watu vijana au Rika lako
Tafuta marafiki au washkaji Rika lako ambao unaona wanajishughulisha kwa shughuli kama hizo nlizoorodhesha.. ongea nao fatana nao Wala usijifanye we wakishua na usiwaeleze habari za mafanikio ya Kaka yako... Changamana nao kama mtu asiye na mzazi au mlezi. NOTE Kuwa makini na tabia zao pia maana wengine hawana tabia njema
3. Waza kufanya zaidi ya hilo tandiko alilokupa
Amekupa malazi ko usibweteke ukasema natafutia tumbo langu tu waza kuwa atakutoa hata kwenye hilo tandiko ko unakazi ya kutafuta sehemu ya kulala pia. Namaanisha weka akiba hata kama ni kidogo ili ukiweza upate kamtaji ka kuuza hata maji dar.
Kwangu ni hayo tu na wengine watakuja kuongezea
Ahsante ndugu wazo lako ni zuri ntalifanyia kazi na nashukuru sana kwa mchango wako
 
Yupo ndugu mmoja alinipigia kwamba ameingia mjini baada ya mishe za kijijini kumkataa . Alifikia kwa dadake single maza.....tukapatana tutaftane j2 flan ajue kwangu.

Siku ya miadi napiga simu weee haikupokelewa hadi leo. Ukute mishe zimemnogea kauza hadi cm
 
Yupo ndugu mmoja alinipigia kwamba ameingia mjini baada ya mishe za kijijini kumkataa . Alifikia kwa dadake single maza.....tukapatana tutaftane j2 flan ajue kwangu...
Siku ya miadi napiga simu weee haikupokelewa hadi leo. Ukute mishe zimemnogea kauza hadi cm
mdada, mtu anauza simu akinogewa na maisha au akipigika?!
 
Mkuu kuna sehemu inaitwa Kisenvule,ipo Mkoa wa Pwani wilaya ya Mkuranga ni kilometre chache kutoka Mbagala Rangi tatu.

Una weza kwenda na kurudi kwani Magali yanapatikana k/koo pale na nauli yake kwasasa 850 mpaka huko.
Kisenvule ni Mji wa Viwanda,kuna viwanda vingi sana.%kubwa ya wakazi wake ni wafanyakazi wa viwandani,
Fika asubuhi na mapema utakuta Umati wa Watanzania wanaelekea viwandani waulize hao kazi zinaendaje watakujuza.

Kuhusu malipo inategemea na kuwinda ila malipo ya chini ni 5000 per day
 
Ukibahatika kupata chochote cha kufanya kumbuka kumnunulia hata zawadi na usave ili utoke hapo haraka. Ndigu yako amekupa makavu mapema bila kukuigizia.

Na huo ndio utaratibu wetu siku hizi haya maisha ya mjini. Ukija kwa ndugu kutafuta maisha nakupanga mapema, kama kukusaidia nitakusaidia ukapate sehemu ya kazi. Chakula na sehemu ya kulala lazima nikusapoti.

Ila ujitahidi upate pahala pa kuishi na uanze maisha yako haraka sana.
 
Sina connection na Wala sijawahi kuishi dar ila Nina experience na aina hiyo ya maisha jaribu kufanya haya yafuatayo pengine unaweza pata mwanga ingawa pia Kila mtu ana bahati yake
1. Toka tembea.... Kuna msemo mguu unaotoka ndio hurudi na baraka na wehenda husema riziki ya mbwa iko miguuni mwake...
Riziki haitokukuta umelala ndani au mekaa unatazama tv liziki iko nje Toka ndani tembea nje huko utakutana na hivyo viwanda unavyoviulizia, utakutana na mafundi mwashi wakitaka vibarua, utakutana na wabeba cargo, wapiga debe, nakadhalika.... Huko ndio utajichanganya sasa
2. Ongea na watu vijana au Rika lako
Tafuta marafiki au washkaji Rika lako ambao unaona wanajishughulisha kwa shughuli kama hizo nlizoorodhesha.. ongea nao fatana nao Wala usijifanye we wakishua na usiwaeleze habari za mafanikio ya Kaka yako... Changamana nao kama mtu asiye na mzazi au mlezi. NOTE Kuwa makini na tabia zao pia maana wengine hawana tabia njema
3. Waza kufanya zaidi ya hilo tandiko alilokupa
Amekupa malazi ko usibweteke ukasema natafutia tumbo langu tu waza kuwa atakutoa hata kwenye hilo tandiko ko unakazi ya kutafuta sehemu ya kulala pia. Namaanisha weka akiba hata kama ni kidogo ili ukiweza upate kamtaji ka kuuza hata maji dar.
Kwangu ni hayo tu na wengine watakuja kuongezea
Mwana akifuata huu ushauri bila Shaka atatusua.
 
Back
Top Bottom