Maisha yana surprises nyingi sana

Maisha yana surprises nyingi sana

Nikiwa kijana mkubwa wa secondary,kama unavyojua kuna kipindi kinafika unaona kabisa hapa wazazi inabidi wasiendelee kuzaa sasa,kwanza kutokana na umri wao lakini pili ile kuona inakuwaje bimkubwa na umri huu anabeba mimba

Ilikuwa inanipa shida kidogo,lakini sikujua kwamba Mwenyezi Mungu anasababu kubwa sana ya kumleta yule dogo akiwa kama last born pale nyumbani

Miaka kadhaa baadae, huku ukubwani dogo huyo ndio kawa nguzo ya familia kwa kiasi kikubwa sana,yeye ndio kajaliwa uchumi mzuri sana na anaisadia familia kwa kiasi kikubwa sana

Hakika kuna mambo Mwenyezi Mungu pekee ndio anajua,nimejifunza kitu kimoja kikubwa kwamba,kila kitu hutokea kwa sababu

Kwahiyo si kazi yako kujaji mambo ambayo huwa yanatokea hapa duniani just wait and see,utashangazwa na hekima ya Mwenyezi Mungu.

Silent king
Kweli kabisa. Mara nyingi tunahukumu jambo kwa tunachokiona leo, kumbe Mungu anaiona kesho yake. Wakati mwingine tunachokiona kama “mshangao” leo, kesho kinakuwa baraka kubwa. Tusihukumu haraka, muda utaeleza kila kitu.
 
Huwezi kusema ni makusudio ya Mungu kuwafanya wawe wakorofi na kusumbua wazazi

Lakini hatuwezi kuweka kila kitu kwenye kapu moja,hapa nazungumzia uwezo wa Mungu kuinua baadhi ya familia kupitia viumbe wake au kupitia wanafamilia wengine
Hizo ni siasa tu za watu walioshindwa kupambana na maisha yao
 
Kama mungu ndio anawajibika kuinua watu kwa ajili ya kutumikia familia zao basi pia ndiye anawajibika kwa wale watu waliokuwa mizigo na mateso kwenye hizo familia. Mfano rahisi ni kama vile kiongozi akijenga barabara anasifiwa na asipojenga anapaswa kulaumiwa na kuwajibishwa.
Hapa naona kuna mambo mawili au matatu

Kuna kuwajibika kwa mtu binafsi na uwajibikaji wa familia

Kwanza mtu binafsi kama mwenyewe amejiingiza kwenye mtindo wa maisha ambao unaathiri maisha yake binafsi hapo yeye ndio wa kulaumiwa,mfano kutowajibika,mihadarati na ujinga mwingine,hapo kijana ameijiharibia mwenyewe,Mungu hayupo hapo

Lakini kwa upande wa wazazi kama hawakumjenga huyu mtoto kwenye misingi bora ya kielimu na makuzi,hapo shida ya wazazi na sio Mungu

Kwahiyo hata huyu kijana akiwa bado amepeta misingi bora mwa nyanja zote bado sio ndio uwakika wa kutoboa maisha,kuna rehema ya Mungu wake,yeye ndio mgawa riziki, yupi humpa kwa kipimo kikubwa na yupi kidogo

Mfano Bakhressa,anasema akianza kushona viatu baadae mdogo mdogo huyo mpaka tunamjua habari yake

Je,kuna fundi viatu wangapi wapo kama bakhressa?

Maana yake ni kwamba mapitio na mafaniko ya mtu tayari yalitayarishwa Tila zamani sana,huyu atakuwa juu huyu atakuwa chini
 
Hakuna kitu kama hicho. HIYO INATOKEA NI KWA TANZANIA TU. MTU UNAJITUMA SANA KTK KAZI ZAKO IWE KILIMO AU BIASHARA ZAKO. LAKINI UNACHOAMBULIA NI HAMNA KITU UKILINGANISHA NA NGUVU ULIYOTUMIA. HAYO NDIO MATOKEO YA SIASA MBOVU ZA CCM.

Mfano unafanya biashara kwa kutumia mtaji wako. Lakini zinakuja kodi nyingi, makusanyo ya TRA hata kabla ya kupata faida inatakiwa ulipe. Hawajali utapata faida au la. Hawana muda wa kuwekeza kwenye kukufundisha kupata faida. Wanawekeza kwenye kukusanya tu bila kujali faida umepata au una hasara.

Ukija kwenye kilimo unaweza kulima lakini soko lake ni la chini kabisa,kwa hiyo nguvu uliyotumia ni bure kabisa.

Kazini fikiria waalimu wana kazi ngumu sana kuliko wabunge. Linganisha mishahara na malupulupu yao. Mwalimu ni kama yupo yupo tu,mshahara wake hata hautoshi kuishi mpaka mwisho wa mwezi. Ili-hali wabunge wanaogelea kwenye mamilioni kwa kazi bure kabisa.

Lakini nenda nchi zingine nguvu utakayotumia kujitafuta ndio malipo yake yatalingana na nguvu uliyowekeza humo.
Siasa za CCM ndizo zimetufikisha hapa
Village in,

Nakubaliana na wewe kwamba linapokuja swala la kiuchumi kwa nchi kwa ujumla wake na maslahi ya watu wake upo sahih kusema uliyoyasema

Kwasababu ni nchi au Taifa ndio hutengeneza misingi ya mafanikio ya watu wake na jamii yake,hilo halina ubishi kabisa

Kwasababu linatengeneza misingi sahihi kuinua uchumi wa watu wake

Lakini tukija kwa mtu mmoja si sahihi kuchukua nadharia ya maendeleo ya Taifa fulani na ukalinganisha na mafanikio ya mtu binafsi, naweza nisieleweke vizur lakini haya ni maono yangu
 
Kweli kabisa. Mara nyingi tunahukumu jambo kwa tunachokiona leo, kumbe Mungu anaiona kesho yake. Wakati mwingine tunachokiona kama “mshangao” leo, kesho kinakuwa baraka kubwa. Tusihukumu haraka, muda utaeleza kila kitu.
Yani kama tungefahamu haya unayosema na kuyazingatia tungebarikiwa sana

Tunaambiwa tusikufuru bali tushukuru tutazidishiwa,lakini tunaharibu baraka zetu kwa kulalamika na kukufuru
 
Lakini anastahili hayo aliyoyapata, utapata unachostahili, ukitaka kupata unachotaka lazima uwe unastahili...

Sisi huwa tunafanya generalisation lakini kuna small details mwenzako au ndugu yako anazingatia ndio maana anatoboa. Maisha hayaamuliwi na generalisation maana kama ni kazi Kila mtu anafanya, kama ni pesa Kila mtu anapata Kwa kiwango chake nk but kuna vitu Tu vidogo vidogo ndio baadae ukivikusanya probably ndio vitatofautisha Hali zetu za kiuchumi...

Mungu na nature haimpi mtu mafanikio ya kiuchumi ambayo hastahili, haijalishi umeyapata Kwa njia mbaya au nzuri lakini lazima ustahili, hakuna kitu cha bahati mbaya. Ukiona watu wanasema Fulani ana bahati Jua kastahili alichonacho.
 
Yani kama tungefahamu haya unayosema na kuyazingatia tungebarikiwa sana

Tunaambiwa tusikufuru bali tushukuru tutazidishiwa,lakini tunaharibu baraka zetu kwa kulalamika na kukufuru
Kabisa. Mara nyingi tunatamani baraka zaidi huku tunasahau kushukuru tulichonacho tayari. Shukrani huleta utulivu, na kulalamika kunaweza kutufanya tusione thamani ya tulichopewa. Ni ujumbe mzito sana huo.
 
Napenda kutofautiana na wewe kidogo, unaposema kufuata details au taratibu au formula ya mafanikio

Sio kwamba watu hawazifuati,ila naamini mafanikio sio kupambana tu,kwasababu kuna watu wanapambana sana lakini mafaniko yao sio makubwa

Naamini rikizi ni kutoka kwa aliyetuumba,tunazo fanya ni sababau tu
Mafanikio binafsi yanatokana zaidi na bahati inayohusisha genetics, familia uliyozaliwa, mahali ulipozaliwa, connections, black swan events n.k Mfano mmojawapo ni wanozaliwa uswahilini kwenye familia masikini inavyokuwa vigumu sana kwao kufanikiwa na wanaishia kuwa waendesha bodaboda kuliko wanaozaliwa familia Bora/za kishua wanaoishi Mbweni, Msasani n.k
 
Hapa tuna mawazo pishani

Maisha yetu yanategemea ridhaa ya Mwenye Enzi Mungu

Hakuna mwenye uhakika wa nini kitakachomkuta sekunde inayofuata ya maisha yake

Tuendelee kumuomba Mwenye Enzi Mungu atupe ridhiki, afya njema na mwisho mwema
Maisha yetu yanategemea bahati nasibu zaidi kwa asilimia 70%(umezaliwa wapi, wazazi wa aina gani, wakati gani, matukio, afya, umbo, rangi n.k)
 
Napenda kutofautiana na wewe kidogo, unaposema kufuata details au taratibu au formula ya mafanikio

Sio kwamba watu hawazifuati,ila naamini mafanikio sio kupambana tu,kwasababu kuna watu wanapambana sana lakini mafaniko yao sio makubwa

Naamini rikizi ni kutoka kwa aliyetuumba,tunazo fanya ni sababau tu
Stop using riziki kama excuse ya kufeli kwa mifumo ya watu. Kila mtu anapambana, lakini swali la msingi ni are they solving the right problems?

Muumba alituwekea akili ili tugundue codes za maisha, ukizikosa hizo utakwama tu hata upige goti vipi.
 
Stop using riziki kama excuse ya kufeli kwa mifumo ya watu. Kila mtu anapambana, lakini swali la msingi ni are they solving the right problems?

Muumba alituwekea akili ili tugundue codes za maisha, ukizikosa hizo utakwama tu hata upige goti vipi.
Ngoja tukubaliane kutokukubaliana,itakuwa imekaa poa sana
 
Back
Top Bottom