Maisha yana surprises nyingi sana

Maisha yana surprises nyingi sana

Silent King

Senior Member
Joined
Jul 17, 2026
Posts
163
Reaction score
361
Nikiwa kijana mkubwa wa secondary,kama unavyojua kuna kipindi kinafika unaona kabisa hapa wazazi inabidi wasiendelee kuzaa sasa,kwanza kutokana na umri wao lakini pili ile kuona inakuwaje bimkubwa na umri huu anabeba mimba

Ilikuwa inanipa shida kidogo,lakini sikujua kwamba Mwenyezi Mungu anasababu kubwa sana ya kumleta yule dogo akiwa kama last born pale nyumbani

Miaka kadhaa baadae, huku ukubwani dogo huyo ndio kawa nguzo ya familia kwa kiasi kikubwa sana,yeye ndio kajaliwa uchumi mzuri sana na anaisadia familia kwa kiasi kikubwa sana

Hakika kuna mambo Mwenyezi Mungu pekee ndio anajua,nimejifunza kitu kimoja kikubwa kwamba,kila kitu hutokea kwa sababu

Kwahiyo si kazi yako kujaji mambo ambayo huwa yanatokea hapa duniani just wait and see,utashangazwa na hekima ya Mwenyezi Mungu.

Silent king
 
No bro,

Maisha hayana surprises.

Kila hatua ya maisha ya mtu yoyote yule ni matokeo ya factors ndogo ndogo zenye kuleta matokeo unayoyaona sasa hivi.

Marcostilone au nimekosea ndugu?
Hujakosea hata chembe ndugu yangu. Hizo wanazoita surprises ni uvivu tu wa watu kutofuatilia details. Kila mtu anavuna alichopanda, hakuna cha ziada. Ni hesabu fupi sana ya logic versus wishful thinking.
 
Napenda kutofautiana na wewe kidogo, unaposema kufuata details au taratibu au formula ya mafanikio

Sio kwamba watu hawazifuati,ila naamini mafanikio sio kupambana tu,kwasababu kuna watu wanapambana sana lakini mafaniko yao sio makubwa

Naamini rikizi ni kutoka kwa aliyetuumba,tunazo fanya ni sababau tu
 
Nikiwa kijana mkubwa wa secondary,kama unavyojua kuna kipindi kinafika unaona kabisa hapa wazazi inabidi wasiendelee kuzaa sasa,kwanza kutokana na umri wao lakini pili ile kuona inakuwaje bimkubwa na umri huu anabeba mimba

Ilikuwa inanipa shida kidogo,lakini sikujua kwamba Mwenyezi Mungu anasababu kubwa sana ya kumleta yule dogo akiwa kama last born pale nyumbani

Miaka kadhaa baadae, huku ukubwani dogo huyo ndio kawa nguzo ya familia kwa kiasi kikubwa sana,yeye ndio kajaliwa uchumi mzuri sana na anaisadia familia kwa kiasi kikubwa sana

Hakika kuna mambo Mwenyezi Mungu pekee ndio anajua,nimejifunza kitu kimoja kikubwa kwamba,kila kitu hutokea kwa sababu

Kwahiyo si kazi yako kujaji mambo ambayo huwa yanatokea hapa duniani just wait and see,utashangazwa na hekima ya Mwenyezi Mungu.

Silent king
Vipi kuhusu ma last born waliogeuka kuwa mizigo na mateso makubwa kwa familia zao? Hayo nayo ndio yalikuwa makusudi ya mungu kwa hizo familia kutokana hao lastborn kuzaliwa?
 
Vipi kuhusu ma last born waliogeuka kuwa mizigo na mateso makubwa kwa familia zao? Hayo nayo ndio yalikuwa makusudi ya mungu kwa hizo familia kutokana hao lastborn kuzaliwa?
Huwezi kusema ni makusudio ya Mungu kuwafanya wawe wakorofi na kusumbua wazazi

Lakini hatuwezi kuweka kila kitu kwenye kapu moja,hapa nazungumzia uwezo wa Mungu kuinua baadhi ya familia kupitia viumbe wake au kupitia wanafamilia wengine
 
Kama mungu ndio anawajibika kuinua watu kwa ajili ya kutumikia familia zao basi pia ndiye anawajibika kwa wale watu waliokuwa mizigo na mateso kwenye hizo familia. Mfano rahisi ni kama vile kiongozi akijenga barabara anasifiwa na asipojenga anapaswa kulaumiwa na kuwajibishwa.
 
Mkuu binadamu ni viumbe wajinga sana..

Wanahisi wanaweza ku control maisha yao

Only God is the answer
Watu wajinga ni wanaofikiri hawana wajibu katika ku control maisha yao. Maendeleo unayoona Japan, Marekani, Europe, Canada, Australia, Singapore, Israel, China, Korea Kusini na kwingine kwingi yametokana na binadamu wa hizo nchi kuamini wana nafasi kubwa ya wao wenyewe ku control maisha yao wenyewe.
 
Napenda kutofautiana na wewe kidogo, unaposema kufuata details au taratibu au formula ya mafanikio

Sio kwamba watu hawazifuati,ila naamini mafanikio sio kupambana tu,kwasababu kuna watu wanapambana sana lakini mafaniko yao sio makubwa

Naamini rikizi ni kutoka kwa aliyetuumba,tunazo fanya ni sababau tu
Hakuna kitu kama hicho. HIYO INATOKEA NI KWA TANZANIA TU. MTU UNAJITUMA SANA KTK KAZI ZAKO IWE KILIMO AU BIASHARA ZAKO. LAKINI UNACHOAMBULIA NI HAMNA KITU UKILINGANISHA NA NGUVU ULIYOTUMIA. HAYO NDIO MATOKEO YA SIASA MBOVU ZA CCM.

Mfano unafanya biashara kwa kutumia mtaji wako. Lakini zinakuja kodi nyingi, makusanyo ya TRA hata kabla ya kupata faida inatakiwa ulipe. Hawajali utapata faida au la. Hawana muda wa kuwekeza kwenye kukufundisha kupata faida. Wanawekeza kwenye kukusanya tu bila kujali faida umepata au una hasara.

Ukija kwenye kilimo unaweza kulima lakini soko lake ni la chini kabisa,kwa hiyo nguvu uliyotumia ni bure kabisa.

Kazini fikiria waalimu wana kazi ngumu sana kuliko wabunge. Linganisha mishahara na malupulupu yao. Mwalimu ni kama yupo yupo tu,mshahara wake hata hautoshi kuishi mpaka mwisho wa mwezi. Ili-hali wabunge wanaogelea kwenye mamilioni kwa kazi bure kabisa.

Lakini nenda nchi zingine nguvu utakayotumia kujitafuta ndio malipo yake yatalingana na nguvu uliyowekeza humo.
Siasa za CCM ndizo zimetufikisha hapa
 
Hapa tuna mawazo pishani

Maisha yetu yanategemea ridhaa ya Mwenye Enzi Mungu

Hakuna mwenye uhakika wa nini kitakachomkuta sekunde inayofuata ya maisha yake

Tuendelee kumuomba Mwenye Enzi Mungu atupe ridhiki, afya njema na mwisho mwema
 
Back
Top Bottom