Maisha yamenipa funzo kubwa

Nebuchadneza

JF-Expert Member
Oct 6, 2023
415
1,032
Habari zenu ndugu zangu.
Natumaini wote ni wazima wa afya.

Katika kupambana na maisha na kuptia changamoto mbalimbali kumenifanya niwe mtu mpole sana, mkimya na mtu nisiye na makuu.

Katika ukuaji wangu wa ujana enzi zile nikiwa teenager sio siri nilikuwa na akili za kipuuzi sana, maisha niliyaona hayana thamani kwa kuwa niliiona kufa kupo,yanini kupambana ndoto zako na kufa kupo ni Bora kula bata,yalikuwa mawazo ya kipuuzi sana nadiriki kusema hivyo.

Nilikuwa mtundu na mkaaidi kwa jamii ila shule sikuwa chini yan top 5, baada ya umri kusonga kidogo na kuptia lile life la Kitaa, na majanga kibao kunipata kweli maisha yamenipa funzo kubwa sana.
Kama:=
- KUHESHIMU WATU WA RIKA LOLOTE.
  • KUWA MPOLE NA MSIKIVU.
  • KUMUANINI MUNGU NA KUJUA UWEPO WAKE.
  • KUTOMDHARAU MTU YEYOTE.
  • KUFURAHIA MAISHA HAYA..
  • KUPAMBANA BILA KUCHOKA..

Maisha ni mwalimu tosha,asiye na cheti cha chuo kikuu.

Daaah tupambaneni wandugu wa tathania.
 
Mitihani ya maisha ndiyo inayomfanya aweze kuelewa maisha vyema na kutambua anatakiwa kufanya nn .by the way keep learning and bring changes to others.
 
Back
Top Bottom