Maisha yamenichapa haswa

Kuhusu hiyo simu ya laki 3 una mshauri afanye nini?
Laki 3,

Tafuta Machinjio ya MBUZI, fanya yafuatayo :-
1. Nunua vichwa vya mbuzi kwa 2500 - 3000/- kila kichwa
2. Andaa sehemu ya kupikia, ( Karibu na grocery/bar au sehemu yenye mkusanyiko)

3. Andaa Vifaa kama vile, sufuria kubwa, jiko, visu, bakuli, sahani.

4. Mahitaji, unga, chumvi, pili pili, nyanya, vitunguu, kiberiti, mkaa,

Maandalizi
Chukua kichwa cha mbuzi, kiandae ukiwa bado upo nyumbani ( koka moto wa kuni, choma vichwa hakikisha manyoya yote yanaungua, baada ya hapo tafuta sufuria kubwa vichemshe mpaka vinaiva kisawa sawa, ( kazi hii ifanyike asubuhi ikifika mchana kila kitu kiwe tayari,)

. Mida ya saa nane andaa sufuria ndogo ndogo kwa ajili ya ku roast vichwa vya mbuzi, ( nyanya, kitunguu, chumvi, pilipili ni mhimu, ) ( usiuze kichwa kama kilivyo unakiponda ponda kama ulojo fulani vile, Wataalam wa haya mambo waananielewa ninacho maanisha)

. Kichwa kimoja fanya elfu 6000 - 7000/- nusu kichwa fanya elfu 3000 - 4000/- plus ugali 4000 - 8000/-,

. Vichwa 5 × 2500 = 11500/-( gulioni)
. Baada ya kuuza 6000 × 5 = 30000/-
. Ugali 1000 matonge 10 =?

. NB: kwenye kila mteja atakaye kuja kuorder iwe nusu au Kichwa kizima hakikisha unapunguza nyama 2 au 3, mpaka unapata kichwa kingine cha ziada, ( hii utalipia nauli, kuni, chumvi na kitunguu), but Tamaa ni mbaya, ukigundulika wataje watahama wote.

. Mwisho Acha ubishoo na kupenda uliko zaliwa/toka..

. Mapambano mema Kijana 🙏🙏🙏.
 
Usikate tamaa mkuu, kama vipi tembelea wagonjwa ICU utapata majibu ya maisha yako.
 
Mkuu Ila mi naweza kuendesha bajaji na bajaji mpya ni hela nyingi Ila watu wanakopesha shida kianzio

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Idea nzuri. Kama hachagui kazi inaweza kumsaidia
 
Duh huyu jamaa akauze nyanya sio bishoo huyu kweli?
 
Bonge ya idea mkuu, tatizo sie mabishoo sijui inakuaje?

Evelyn Salt mchongo huu hapa wa 2024
 
Mkuu Ila mi naweza kuendesha bajaji na bajaji mpya ni hela nyingi Ila watu wanakopesha shida kianzio

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
. Ni kweli mkuu, ila unaona kikwazo ulicho nacho, bado tunaludi pale kwenye umaskini 😥,

. Siyo kwamba watu hawana hela, tatizo uaminifu,( hili limekua changamoto sana katika maisha ya sasa),

. Kwa sasa unacho hitaji ni msingi kwanza ambao unaweza kuaminiwa na mtu yeyote.
1. Anza na dayworker ya Bajaj vijiweni
2. Fahamiana na madereva wenzio, weka ukaribu nao.
3. Onesha nia ya Kazi yako, Rafiki zako watakupa connection za Maboss walipo.

NB: Kama una mwanini mungu mtangulize katika mahangaiko yako, mtoto wa kiume marufuku kukata Tamaa 🤝🤝
 
Je mkuu nikiuza flat,kitanda na simu yangu humu ntakosa mtu wa kunipa milioni moja ili nikawape wale watu wanikopeshe bajaji mpya?

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
 
Je mkuu nikiuza flat,kitanda na simu yangu humu ntakosa mtu wa kunipa milioni moja ili nikawape wale watu wanikopeshe bajaji mpya?

Sent from my Pixel 3a XL using JamiiForums mobile app
. Bajaj ya mkopo ni bei gani?

. Kwa Nini uuze vitu vyote hivyo ukachue bajaji ya mkopo?

. Najua ndoto yako ni kuendesha/kumiliki bajaji ( labda marafiki/Rafiki yako anayo 😐 na wewe unatamani iwe hivyo), ndiyo waweza ukawa upo sahihi kabisa, lakini kuiga biashara ya mtu utapotea)

. Kaka/Mdogo wangu masuala ya mikopo achana nayo, najua kabisa hiyo Bajaj utafanya kazi ya kulipia/kuludisha mkopo wa bajaji ndani ya miaka 3 - 4,, ( hii siyo kabisa)


. Million 8 ÷ 365½ = 21917 kila siku . Kwa hiyo ukikomaa na biashara ndogo ndogo na ukaheshimu hela, kwa mwaka mmoja na nusu hiyo M8, unaipata bila shida. ( hapa utakua ume save mda)

. Siyo lazima uazae na bajaji mpya, Unaweza anza hata bajaji used, ambayo bei ni chee kabisa.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…