Maisha ya ubachela ni vituko

Kuna tofauti kati ya kuwa MCHAFU na kuwa bachelor. Mambo yote uliyoyasema hapo juu ni dalili ya mtu mchafu sana na asiyejielewa na kama hayo ndio maisha yako my brother sio sifa nzuri hata kidogo.
na ukisha balehe ukashindwa kuwa tofauti na kabla kwenye suala la usafi bas wewe utakuwa mchafu milele. hata kama ulikuwa msafi baada ya balehe usafi huongezeka
 
Kweli dogo mtata huyu namfuatilia toka 2013..

Hafu sinaga nguo za vitambaa ni jinzi tu yaani hua na2aza sana nikitaka kufua
hahaaa duuhh hapo nimwendo wakuzifuta tu..wakati unapotaka kuzivaa


1more wind on ur SOFA
 
Hahaahaaa...
Very true.
 
Kuna tofauti kati ya kuwa MCHAFU na kuwa bachelor. Mambo yote uliyoyasema hapo juu ni dalili ya mtu mchafu sana na asiyejielewa na kama hayo ndio maisha yako my brother sio sifa nzuri hata kidogo.
Hakika.
 
Ni kwel ila kwa upande wang npo tofauti kdg mkuu..
 
Mimi aisee katika maisha ya kibachela masuala magumu ni kupika na kuosha vyombo tu. Hata hivyo uvivu wa kuosha vyombo haunisababishii kuwa mchafu kiasi hicho!

Shida ni kwamba nikiosha vyombo nakuwa mgumu kuvitumia kwa uhuru, ...nikitumia kijiko kuchotea sukari nakimbia kukisuuza....,, nikinywa chai lazima kikombe na vyombo vingine nilivyotumia nivioshe....,, zamani nilijikuta na kitabia cha kulia kwenye sufuria ili tu nisichafue vyombo vingi
na sufuria lazima niioshe ndo niendelee na mengine...

Binafsi ni kijana msafi sana, si usafi ule wa magumashi kuvaa nguo za nje safi halafu za ndani chafu! Ama kusafisha geto pale tu anapokuja manzi, no! Nina usafi wa uhakika ambao napenda nione na kuamini mwenyewe kwamba ni usafi, kuliko kupendelea zaidi kuonekana kwa watu. Mabinti wa hostel walikuwa wanaogopa kuingia ovyo geto kwangu kwa hofu ya kuchafua duh!

Shida ya vijana wengi uchafu ni tabia, kiasi kwamba walishazoea eti maisha ya uchafu ni UANAUME! Kumbe uvivu tu. Wengine wanaleta hata humu nyuzi zao wakisema mwanaume lazima uoge kwa ku-beep, unuke kikwapa, na blah blah kibao.

I can say 96% ya vijana nilio/ninaokutana na kuishi nao ni wachafu completely, hata akijitahidi namna gani kuficha uchafu ataonekana tu! 3.8% ndo wale wanaobabaisha usafi wao, angalau wanajitahidi kidogo. Then 0.2% ndo tuna usafi asilia, si wa kubahatisha!

Mleta mada umedadavua maisha ya mchafu, si ya bachelor.
 
hadi sururia
 
Mimi kufua ilikuwa sio tatizo kwangu. Niliacha kupika kwa sababu ya usumbufu wa kuosha sufuria.
 
na ukisha balehe ukashindwa kuwa tofauti na kabla kwenye suala la usafi bas wewe utakuwa mchafu milele. hata kama ulikuwa msafi baada ya balehe usafi huongezeka
Kweli kabisa, tatizo ni kuwa tulivokuwa kwenye mikono ya wazazi/ walezi tulifanya kazi chini ya usimamizi na usipofanya utaadhibiwa. kwa mfano utalazimika kufua nguo zako otherwise utachapwa sasa tukianza kujitegemea na hakuna mtu wa kutusimamia tena ndo mambo kama ayo sufuria ya ugali inalowekwa wiki nzima.
 
Kweli kabisa 100%. Kwangu mimi jambo ambalo sijafaulu hadi sasa ni kupika ugali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…