Maisha ya sasa ya msanii Saida Karoli

Maisha ya sasa ya msanii Saida Karoli

kinshwi

Member
Joined
Aug 22, 2016
Posts
48
Reaction score
173
Nimerejea Bukoba kwa likizo baada ya miaka kadhaa, na kwa masikitiko makubwa nilikumbana na hali iliyonishtua sana. Nilimkuta msanii nguli wa muziki wa asili, Saida Karoli aliyewahi kutoa nyimbo zilizopata umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hadi kuvuka mipaka ya Tanzania akiishi maisha ya dhiki yasiyoendana kabisa na hadhi na mchango wake mkubwa katika sanaa na utamaduni wa taifa.

Kwa sasa, Saida Karoli anaishi katika nyumba ya kupanga ya vyumba viwili, katika mazingira yasiyofurahisha, hali ambayo haistahili hata kidogo kwa msanii aliyewahi kuiwakilisha nchi yetu kimataifa kwa heshima kubwa. Hali hii inanifanya nijiulize maswali mazito kuhusu mfumo wetu wa kulinda wasanii, hasa wale waliotoa mchango mkubwa kabla ya enzi ya mifumo ya sasa ya kidijitali.

Kwa wajuzi wa masuala ya commercial entertainment, je, hakuna njia ya kusaidia wasanii kama Saida Karoli kufaidika na royalties za kazi zao walizofanya miaka ya nyuma? Je, sheria na taasisi zetu za hakimiliki zinawafikia kwa vitendo, au zipo tu kwenye maandishi?

Zaidi ya hapo, tukio hili linapaswa kuwa funzo kwa wasanii wanaong’ara kwa sasa. Umaarufu ni wa muda, lakini maisha ni ya kudumu. Ni muhimu kwa wasanii wa kizazi cha sasa kupambania sera imara za kulinda kazi zao, kudai haki zao za kisheria, kusaini mikataba yenye kuwanufaisha hadi baadaye

Kwa kweli, hali niliyoikuta imenihuzunisha sana.
 
Lakini wasanii wenzake walijaribu kumnyanyua mwaka 2017, 2018 kuna wasananii walimshirikisha kwenye nyimbo kadhaa na kutumia nyimbo zake za zamani.

Maisha siyo tu kupewa pesa, tatizo ni akili zetu wenyewe. Ukifikiria kwa pesa hata kidogo alizopata kwenye muziki asngeweza kufanya biashara au kilimo akajikwamua kiuchumi?

Hapaswi kulaumiwa yeyote kwa maisha ya mtu binafsi, ni hali ambazo mhusika mwenyewe huzisababisha.

Maisha haya dahh!
 
Nimerejea Bukoba kwa likizo baada ya miaka kadhaa, na kwa masikitiko makubwa nilikumbana na hali iliyonishtua sana. Nilimkuta msanii nguli wa muziki wa asili, Saida Karoli aliyewahi kutoa nyimbo zilizopata umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hadi kuvuka mipaka ya Tanzania akiishi maisha ya dhiki yasiyoendana kabisa na hadhi na mchango wake mkubwa katika sanaa na utamaduni wa taifa.

Kwa sasa, Saida Karoli anaishi katika nyumba ya kupanga ya vyumba viwili, katika mazingira yasiyofurahisha, hali ambayo haistahili hata kidogo kwa msanii aliyewahi kuiwakilisha nchi yetu kimataifa kwa heshima kubwa. Hali hii inanifanya nijiulize maswali mazito kuhusu mfumo wetu wa kulinda wasanii, hasa wale waliotoa mchango mkubwa kabla ya enzi ya mifumo ya sasa ya kidijitali.

Kwa wajuzi wa masuala ya commercial entertainment, je, hakuna njia ya kusaidia wasanii kama Saida Karoli kufaidika na royalties za kazi zao walizofanya miaka ya nyuma? Je, sheria na taasisi zetu za hakimiliki zinawafikia kwa vitendo, au zipo tu kwenye maandishi?

Zaidi ya hapo, tukio hili linapaswa kuwa funzo kwa wasanii wanaong’ara kwa sasa. Umaarufu ni wa muda, lakini maisha ni ya kudumu. Ni muhimu kwa wasanii wa kizazi cha sasa kupambania sera imara za kulinda kazi zao, kudai haki zao za kisheria, kusaini mikataba yenye kuwanufaisha hadi baadaye

Kwa kweli, hali niliyoikuta imenihuzunisha sana.
Acha ateseke!!!
 
ingawaje simjui kibinafsi na siwezi kumhukumu lkn kuna magonjwa ya akili pia na siyo kila failure ni makosa ya wengine labda ni matatizo yake yeye mwenyewe binafsi pia, kwangu kabla ya kutaka kusaidia mtu kama huyo wasaidiwe kwanza watoto yatima, walemavu au hata wazee wasio na msaada wowote, halafu kiasi kitakachobakia kama hata kikibakia ndio aangaliwe yeye &co. labda …
 
Nimerejea Bukoba kwa likizo baada ya miaka kadhaa, na kwa masikitiko makubwa nilikumbana na hali iliyonishtua sana. Nilimkuta msanii nguli wa muziki wa asili, Saida Karoli aliyewahi kutoa nyimbo zilizopata umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi, hadi kuvuka mipaka ya Tanzania akiishi maisha ya dhiki yasiyoendana kabisa na hadhi na mchango wake mkubwa katika sanaa na utamaduni wa taifa.

Kwa sasa, Saida Karoli anaishi katika nyumba ya kupanga ya vyumba viwili, katika mazingira yasiyofurahisha, hali ambayo haistahili hata kidogo kwa msanii aliyewahi kuiwakilisha nchi yetu kimataifa kwa heshima kubwa. Hali hii inanifanya nijiulize maswali mazito kuhusu mfumo wetu wa kulinda wasanii, hasa wale waliotoa mchango mkubwa kabla ya enzi ya mifumo ya sasa ya kidijitali.

Kwa wajuzi wa masuala ya commercial entertainment, je, hakuna njia ya kusaidia wasanii kama Saida Karoli kufaidika na royalties za kazi zao walizofanya miaka ya nyuma? Je, sheria na taasisi zetu za hakimiliki zinawafikia kwa vitendo, au zipo tu kwenye maandishi?

Zaidi ya hapo, tukio hili linapaswa kuwa funzo kwa wasanii wanaong’ara kwa sasa. Umaarufu ni wa muda, lakini maisha ni ya kudumu. Ni muhimu kwa wasanii wa kizazi cha sasa kupambania sera imara za kulinda kazi zao, kudai haki zao za kisheria, kusaini mikataba yenye kuwanufaisha hadi baadaye

Kwa kweli, hali niliyoikuta imenihuzunisha sana.
Saida karoli na wasanii wengine kama Q chief walikubali kuuza haki zao zooote za muzikikwa maharamia.

Huyu Saida nadhani alimuuzia Felician Mutta(fm studios)

Q chilla aliuza kwa chief kiumbe haki zoote.

Hata diamond almanusura anase kwenye mitego hiyo, sema yeye alivyojitoa akaambiwa arudishe gari alilopewa
 
Wapo bize na kampeni za mbogamboga
 
Wasanii na wanamichezo wengi hupigika sana muda wao wa kutamba ukipita. Tatizo kubwa ni kutokuwa na akili za uwekezaji. Pia mfumo wa ujamaa ni kirusi kwenye maisha ya wengi ambao sio GenZ. Yaani utakuta akiwa kwenye ubora wake Saida alikuwa kimbilio la ndugu, jamaa na marafiki kumsaidia kutafuna pesa zake.

Cha muhimu akubaliane na hali yake na akomae tu na maisha kupitia shughuli yoyote ya halali.
 
Saida karoli na wasanii wengine kama Q chief walikubali kuuza haki zao zooote za muzikikwa maharamia.

Huyu Saida nadhani alimuuzia Felician Mutta(fm studios)

Q chilla aliuza kwa chief kiumbe haki zoote.

Hata diamond almanusura anase kwenye mitego hiyo, sema yeye alivyojitoa akaambiwa arudishe gari alilopewa
TMK walimpa haki zote P Funk. Huyu P Funk alikiri kuwa Prof Jay alikuwa mjanja kwa kumlipa yeye pesa na hatimaye kubaki na kazi zake. Ila kina Nature na wenzake walishapoteza haki.
 
Biashara hiyo inahitaji nidhamu, maana kujua kuimba pekee haitoshi kunifikisha Msanii nchi ya ahadi mpaka uwe na watu wa kueleweka.

Kwa mfano Juma Nature na wenzake walikataa kusimamiwa na Saidi Fella wakidhani kuwa na meneja ni mzigo kwao, kwamba wana uwezo wa kufanya kila kitu wenyewe.

Lakini tayari leo Nature na wenzake pamoja na vipaji vyao wamepotea ili hali Fella anamsaidia Diamond kulishika soko la muziki.
 
Ukiwa na uhakika kupata pato la hata laki sita plus au hata chn yake kutegemeana na mazingira unayoishi nakushauri yafuatayo hususani kama hujatoka royal family:

1. Epuka maisha ya anasa yasiyokuwa na maana/ achana na zile kauli za kusema "ponda maisha" wakati hujui hcho kipato kitaishaje?

2. Achana na ulaghai wa wana siasa uchwara, jitahidi kila mwezi uwe unapeleka hata elfu 40 au 50 pale NSSF angalau kwa muda wa miaka 15 mfulululizo, hautajutia..

3. jitahidi sana kujifunza kuhusu fixed account hususani kwa mabenki yanayotoa interest rate kubwa

4. achana na mambo ya AMIS UTT kama pato lako ni la chini ya milion 50.

5. jitahidi kwenda maeneo ya wilaya ambazo hazijachangamka hususani zilizo bush, nunua ardhi (huko gharama bado ni vitonga)

6. jitahd kujenga hata kama ni chumba na sebule ya kwako
-acha kujifanya eti unataka uwe na milion 30 ndo uje ujenge (kama huwez kujenga chumba na sebule, basi kipato kikisha utakuja kupanga chumba na sebule)
 
Back
Top Bottom