Maisha ya Nigeria

Artifact Collector

JF-Expert Member
Mar 7, 2019
6,539
10,006
Na Edo kumwembe

Wanigeria wameshindwa kugawana vyema kile kitu kinachoitwa keki ya taifa. Inaonekana ni taifa la watu wajanja ambao kila mmoja anachukua chake mapema na kuwaacha raia wake wakiwa maskini ingawa inatajwa kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi imara Afrika.

Hauwezi kuliona hilo kwa macho. Kwanza kabisa watu ni wengi. Kando ya barabara za Port Harcourt watu ni wengi na maisha ni vurugu. Hii inatokana na ukweli kwamba Nigeria ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani kwa ujumla. Sensa inaonyesha kuna Wanigeria 112 milioni wanaoishi nchini kwao. Vitongoji vya Port Harcourt vinaakisi idadi kubwa ya watu Nigeria. Kila kitu kimechakaa. Watu wamechakaa. Magari yamechakaa. Majengo yamechakaa na barabara pia zimechakaa.

Jiji la Port Harcourt linatajwa kuwa lenye utajiri mkubwa zaidi miongoni mwa majiji ya Nigeria. Hapa kuna utajiri wa mafuta lakini pia kuna bandari. Kinachoshangaza ni kwamba utajiri huo unabakia katika makaratasi au serikalini. Raia wake wamechoka, mitaa yake imechoka, barabara zake zimechoka. Naelezwa kwamba Abuja ndio mji ambao walau una majengo ya kisasa na barabara za kuvutia. Vinginevyo Nigeria imechakaa na ni wazi kwamba hesabu za wachumi Nigeria ni nchi tajiri haziakisi macho pindi utakapotembea vitongoji.

Raia wengi ni maskini na watu wachache ni matajiri. Kutoka katika hoteli ambayo Yanga walikuwa wamefikia ya Swiss Sprit kando yake kwa nyuma tu kuna nyumba zilizochakaa ambazo mabati yamewekewa mawe juu ili yasizolewe na upepo. Watoto wanacheza mpira mbele ya macho ya wazazi wao ambao wanapika chakula nje ya nyumba. Naambiwa hapo ndipo yanapoanzia maisha ya mchezaji wa Kinigeria. Kuondoka Nigeria na kwenda kucheza nje ya nchi kuna maana kubwa kwa mchezaji.

Kwanza mchezaji anaondokana na vurugu za jiji lake au mtaani kwake. Mchezaji yeyote wa Nigeria ambaye ataondoka Nigeria na kwenda kwingineko ghafla atajikuta katika jiji zuri, lisilo na vurugu kama ilivyo mitaa ya kwao. Pua yake itapumua vyema na masikio yataondolewa katika kelele zisizo na msingi.

Mtu yeyote ambaye ataondoka Nigeria atajikuta katika nafasi ya kuongeza kipato. Nigeria hii ina watu lukuki lakini ambao hawana ajira. Wengi kati yao wana elimu kubwa ambayo inawapa uhakika wa ajira mahala kwingine au uhakika wa maarifa ya kuishi.

Kwa wale ambao wamezaliwa na vipaji, soka inabakia kuwa njia kubwa ya kutengeneza maisha. Inawezekana katika umri mdogo wakapelekeshwa na mambo mawili. Kwanza ni kuona maisha ya kifahari ya mastaa wengi wanaocheza nje. Lakini pia msukumo kutoka kwa wazazi. Ni tofauti na nchi yetu ambapo baadhi ya wazazi hawaamini kama vipaji vya michezo na sanaa vinaondoa umaskini. Lakini pia mazingira haya magumu ninayoyaona Nigeria haishangazi kuona linamfanya Mnigeria aweze kuishi Shinyanga akicheza Biashara Shinyanga bila ya shida. Kwanza mji wenyewe Shinyanga kwake unakuwa mzuri tu kuishi tofauti na kelele za Port Harcourt.

Lakini, hapohapo Mnigeria hataki kutazama nyuma. Kwa nilichokiona hapa ni ngumu kwa Mnigeria kutazama nyuma kimaisha. Sawa nyumbani ni nyumbani, lakini nyumbani kunakuwa kutamu zaidi kama unaweza kurudi ukaishi kwa utulivu. Kwa nilivyoitazama Nigeria, nyumbani kunaweza kuwa kutamu kwa watu kama kina Jay Jay Okocha. Hawa wana majumba ya kifahari hapa na wana magari ya kifahari. Wanaishi kifahari. Nigeria hapawezi kuwa kutamu kwa raia wa kawaida ambaye hajafanikiwa nje ya nchi. Na haishangazi kuona hawarudi nyuma. Maisha ya Nigeria yana ushindani mwingi. Hakuna kazi ya mwanaume wala mwanamke. Nadhani idadi yao kubwa inasababisha watafute mkate katika ardhi nyingine nje ya nyumbani. Ni kama ilivyo kwa Wachina, Wahindi au Wabrazil. Mkate wa ardhi yao pekee hautoshi.
 
kwa hiyo chambua ya edo inatuonyesha kuibuka kwa makundi kama boko haramu ni halali kupingana na ujinga wa serikali unaofanya watu kuchoka na uchakavu wa nchi yao.

ni kweli hata kongo ndio maana vikundi vya waasi ni vingi kwa sababu ya kukosa keki ya taifa kwa wanaanchi
 
Mchambuzi Mzuri hawezi kuandika hivi:

Nigeria ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani kwa ujumla. Sensa inaonyesha kuna Wanigeria 112 milioni wanaoishi nchini kwao.

Duniani kwa Ujumla???? WTF ameshindwa hata Ku Google.
 
Hujaelewa. Ni 'moja' ya nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani.

It means kwenye top populated countries in Africa ipo. Pia 'inawezekana' hata duniani kwa ujumla ni miongoni mwa nchi zenye watu wengi. Top 20 naamini Nigeria haikosekani duniani. Hajasema ni ya kwanza.

Soma uelewe Kiswahili sio unakurupuka mkuu.
 
Pop.png
 
Amekosea wapi? Nimegoogle nimeona nigeria ni nchi namba 6 kwa idadi kubwa ya watu duniani.

Screenshot_20210922-071348_Firefox.jpg
 
Pisi zao tu mi hoi wana macho flani hivi akikutizama genyr lazima ipande na shape sasa
 
Huwezi kutumia neno 'Kama sio Duniani' wakati Nigeria inashikiria nafasi ya 6. Ukitumia neno hilo unajaribu kutupa maana kwamba Nigeria Kama sio nchi ya Kwanza kwa kuwa na Idadi kubwa ya watu basi ni nchi ya Pili.

Ameweka neno miongoni.. maana ya neno miongoni ni nini?

Nigeria ni miongoni mwa nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani kwa ujumla. Sensa inaonyesha kuna Wanigeria 112 milioni wanaoishi nchini kwao.
 
Hujaelewa. Ni 'moja' ya nchi zenye idadi kubwa ya watu Afrika kama sio duniani.

It means kwenye top populated countries in Africa ipo. Pia 'inawezekana' hata duniani kwa ujumla ni miongoni mwa nchi zenye watu wengi. Top 20 naamini Nigeria haikosekani duniani. Hajasema ni ya kwanza.

Soma uelewe Kiswahili sio unakurupuka mkuu.
Sasa ukiwa kwenye Top 20 ndo utumie neno 'Kama sio Duniani? Ni sawa na kusema Phil Knight ni mtu tajiri America kama sio duniani kwa sababu tu yupo kwenye Top 20. Wakati dunia ina Matajiri kibao kumzidi.
 
acha kupindisha hapo, ili ishabihiane na statement ya kumwembe sema hivi

“Pil Knight ni miongoni mwa watu matajiri America kama sio duniani”

akimaanisha marekani kuna matajiri wengi ambapo phil knight ni mmoja wao (haijalishi wa kwanza au wa ngapi ila ni mmoja wa matajiri).

Then pil knight kuna uwezekano akawa miongoni mwa matajiri duniani (haijalishi anashika namba ngapi ila ni mmoja wa matajiri)

Tusipende kuhukumu kwa kutoelewa lugha vizuri
 
Back
Top Bottom