Maisha ya mama Anna Tibaijuka kijijini Muleba

Maisha ya mama Anna Tibaijuka kijijini Muleba

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,719
Screenshot from 2014-12-23 12:27:02.png
Hapa ndipo alipozaliwa na kukulia.

Screenshot from 2014-12-23 12:28:07.png
Hapa akiwa na familia yake Moscow ubalozi wa Tanzania

Screenshot from 2014-12-23 12:33:45.png
Uzio wa shamba lake huko Muleba,kiasili zaidi.

Screenshot from 2014-12-23 12:34:21.png
Geti la kuingia kwenye nyumba yake likiwa limetengenezwa kwa mbao na makuti.

Screenshot from 2014-12-23 12:31:19.png
Upande wa mbele wa mjengo wa Mama Tibaijuka

Screenshot from 2014-12-23 12:32:26.png
Jasiri haachi asili,kwa mbali kahawa zikiwa zimeanikwa ili zikaushwe kwa jua.

Screenshot from 2014-12-23 12:32:59.png
Lango kuu la kuingia ndani ya nyumba

Screenshot from 2014-12-23 12:35:10.png
Mandhari nzuri ya nyumba ikiwa imepambwa kwa migomba yenye ukijani.


Alizaliwa tarehe 12 Oktoba, 1950 kijiji cha Kagabiro, Wilaya ya Muleba, mtoto wa 5 kati ya watoto 11 wa wakulima, Hayati Ta Alexander Kajumulo na Ma Aulelia Teyolekererwa Rwakajuga (yu hai).


Alisoma Shule ya Msingi ya Kaigara, 1958 -1961. Alifaulu akiwa wa kwanza kwenda Shule ya Kati (Middle School) ya Wasichana ya Kashozi – Kamukukubwa, 1962 -1965 (sasa ni Sekondari ya Wasichana, Hekima). Alifaulu tena akiwa wa kwanza kujiunga na shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa, Bukoba, 1966 – 1969.


Alisonga mbele na kujiunga na kidato cha tano Shule Bingwa ya Wasichana ya Marian College (sasa Kilakala), Morogoro. Mwaka 1972 alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, Operesheni Tumaini, Ruvu (akiwa pamoja na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete). Akafaulu tena na kujiunga na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Kitivo cha Kilimo, Morogoro 1972 - 1975.


Alihitimu akiwa ameongoza darasa lake na kupewa nishani ya Mkuu wa Chuo kwa ushindi huo. Aliajiriwa kama Mhadhiri Mzaidizi, Idara ya Uchumi. Mwaka huohuo (1975), alichaguliwa kwenda kusoma masomo ya juu Chuo Kikuu cha Cornell Marekani lakini Desemba 1975 akaamua kufunga ndoa na mchumba wake aliyekuwa amemsubiri siku nyingi amalize masomo, Hayati Balozi Wilson KamuhabwaTibaijuka, aliyekuwa kwa wakati huo Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, Stockholm, Swideni.


Katika ndoa yao walijaliwa watoto wanne, Muganyizi (1976), Kemilembe (1979), Kagemulo (1986) na Kankiza (1991). Waliishi vyema hadi Mungu alipowatenganisha Mei, 2000.
 

Attachments

  • Screenshot from 2014-12-23 12:28:31.png
    Screenshot from 2014-12-23 12:28:31.png
    47.7 KB · Views: 6,689
..mtusi walipa kodi naye amesoma Muleba..mtoto awaombe radhi watanzania kwa kutumia neno nanukuu "*** all"
 
Nasikia hajanunua hata kagari ni mcommunist huyu anaipenda jamii kuliko anavyojipend yeye
 
bandiko limekaa kihuruma kweli....natamani kulia.mama wewee uwiiiii mama anna tibaijuka....
 
Muleba hapo Nshamba. Bukoba kuna mandhari nzuri sana
 
lizaliwa tarehe 12 Oktoba, 1950 kijiji cha Kagabiro, Wilaya ya Muleba, mtoto wa 5 kati ya watoto 11 wa wakulima, Hayati Ta Alexander Kajumulo na Ma Aulelia Teyolekererwa Rwakajuga (yu hai).


Alisoma Shule ya Msingi ya Kaigara, 1958 -1961. Alifaulu akiwa wa kwanza kwenda Shule ya Kati (Middle School) ya Wasichana ya Kashozi – Kamukukubwa, 1962 -1965 (sasa ni Sekondari ya Wasichana, Hekima). Alifaulu tena akiwa wa kwanza kujiunga na shule ya Sekondari ya Wasichana ya Rugambwa, Bukoba, 1966 – 1969.


Alisonga mbele na kujiunga na kidato cha tano Shule Bingwa ya Wasichana ya Marian College (sasa Kilakala), Morogoro. Mwaka 1972 alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa, Operesheni Tumaini, Ruvu (akiwa pamoja na Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete). Akafaulu tena na kujiunga na Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Kitivo cha Kilimo, Morogoro 1972 - 1975.


Alihitimu akiwa ameongoza darasa lake na kupewa nishani ya Mkuu wa Chuo kwa ushindi huo. Aliajiriwa kama Mhadhiri Mzaidizi, Idara ya Uchumi. Mwaka huohuo (1975), alichaguliwa kwenda kusoma masomo ya juu Chuo Kikuu cha Cornell Marekani lakini Desemba 1975 akaamua kufunga ndoa na mchumba wake aliyekuwa amemsubiri siku nyingi amalize masomo, Hayati Balozi Wilson KamuhabwaTibaijuka, aliyekuwa kwa wakati huo Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, Stockholm, Swideni.


Katika ndoa yao walijaliwa watoto wanne, Muganyizi (1976), Kemilembe (1979), Kagemulo (1986) na K


Sasa nimeelewa ni kwanini Kikwete alikuwa na wakati mgumu kumtimua huyu MwanaMama.
 
Huyu mama anaonekana ni kichwa sana na very hard working sidhani kama ni fisadi. ila kitu kidogo sana kimemcost kwenye escrow scandal ni baada ya kupokea hela ya magumashi kwa jina lake, imemcost haswaa.
 
mume wake alikuwa balozi, yeye mwenyewe prof...ningeshangaa kama asingeishi hivi, big up sana kwake....wako wapi wale wanaosema eti wahaya hawajengi kwao?

Nawashangaa wanaomkandia mama, Tibaijuka pesa anayo kitambo hata kabla ya kuwa mbunge.
 
Back
Top Bottom