Maisha ya kijijini yalivyo na furaha

Nakumbuka hata nikiwa na 10000 mfukoni kwa wiki naweza tumia hata 2000 tu.Mboga za majani zipo ndani,chai hakuna,uji wa mabuyu au ukwaju no sugar,Ugali dona safi,mafuta ya kupikia ya ng'ombe au mawese,chumvi ya mawe nyingi,maji ya bure mtoni au bwawani,magunia ya mahindi na mtama mweupe mengi ndani,No perfume/body spray,nguo nzuri 2 tu,kulala saa 2 mpaka 3 na kuamka 12.
Da! life zuri sana
 
Hata mimi laifu la bushi nalielewa sema entertainment kama kununua malaya,kuruka debe, kukutana na watoto wakali inakuwaga shida..................
Bush mambo hizo starehe kibao.....debe la nini ngoma inaanza saa nne asbh hadi saa 12 asbh. Warembo naturally kijana..watoto wakali wa mijini wazazi wao walionwa wakali pia kijijini.
 
Wakati wa mavuno hiyooo balaaaa.....unakuta chungu kimejaa karanga za maganda mahindi mabichi na viazi kibao maganda unamenya wakati wa kula. pembeni jagi la majiii kubwa. storiiiiii kibao
 
Sasa mbona kila siku watu wanakimbilia mijini?!
Inategemea na kijiji ila kwa ujumla wake, vijijini ni sehemu nzuri ya kutembelea haswa kwa mapumziko ila kuishi moja kwa moja ni mtihani na ukitaka kulijua hili waangalie wakazi wake walivyochoka na maisha
 
Hapo nimeelewa maana watu wanaotoka vijijini kwenda mjini ni kubwa kuliko kinyume chake.
 
Ili uyafurahie maisha ya kijijini ni lazima uandae mazingira vizuri. Ukienda kijijini kichwa kichwa lazima upigike mbaya kabisa.
 
Ishi mjini hata kama ni kwa gharama kubwa na usikubali kuishi kijijini hata kama kuna maisha rahisi......!!!!! Mjini kunoga CHAI........na vitabu vya dini vinasema manabii wote waliishi Town vijijini walienda kufanya biashara na kueneza dini tu......Wa umri wako waliopo kijijini wamekuwa WAZEE utawahurumia...........
 
Ili uyafurahie maisha ya kijijini ni lazima uandae mazingira vizuri. Ukienda kijijini kichwa kichwa lazima upigike mbaya kabisa.
Mjini kuona watu wanahesabu fedha ni jambo la kawaida........lakini kijijini thubutuuuuuuuu watu wanajificha kwenye kuhesabu fedha.......
 
Kwenda Kufua na kuchota Maji Siku ya jmos na kuanza kutongozana kisimani, ilikuwa raha sana aisee, na mkichelewa kurudi hizo mboko zake ni za hatari
 
Kwenda Kufua na kuchota Maji Siku ya jmos na kuanza kutongozana kisimani, ilikuwa raha sana aisee, na mkichelewa kurudi hizo mboko zake ni za hatari
 
Back
Top Bottom