'Maisha ya Jela Matamu Sana' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Maisha ya Jela Matamu Sana'

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by MziziMkavu, Sep 16, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Thursday, September 16, 2010 12:57 AM
  Mwanaume mmoja wa nchini Ujerumani alienda kwenye kituo cha polisi nchini humo akiomba arudishwe tena jela kwakuwa hakuna maisha matamu aliyowahi kuishi duniani kama maisha ya jela. Mwanaume huyo ambaye polisi hawakumtaja jina lake alienda kwenye kituo cha polisi katika mji Saarbruecken magharibi mwa Ujerumani na kuanza kuwabembeleza polisi wamrudishe tena jela.

  Mwanaume huyo alisema kuwa hajawahi kuwa na maisha matamu duniani kama wakati ambao alikuwa jela kwenye miaka ya 1980.

  Mwanaume huyo baada ya kuona polisi hawana mpango wa kumtupa jela aliwauliza polisi ni kosa gani afanye ambalo litapelekea atupwe jela.

  Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 47, aliwaonyesha polisi hati zake za kuachiwa huru kutoka jela ambako alitumikia kifungo kwenye miaka ya 1980.

  Huku akiongea kwa upole katika hali ya kubembeleza, aliwaambia polisi kuwa itakuwa furaha kubwa sana kwake iwapo atafanya kosa ambalo litapelekea atupwe jela muda mrefu.

  Polisi walifanya naye mahojiano kwa muda mrefu wakimshauri aache kufikiria hivyo na wamemuandalia semina ya ushauri nasaha juu ya maisha ya uraiani.
   
 2. D

  Dick JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Feb 10, 2010
  Messages: 477
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni abnomality aliyokuwa nayo. Vitu (abnomalities) kama hivyo vinatokea kwa chochote na kwa lolote!
   
 3. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #3
  Sep 17, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,901
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Matatizo kwao mbagaraaaaaaaaaaa ,Hapa nyumba mbere jararaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
   
Loading...