Maisha ya Ingrid mjini Arusha mpaka Dar-es-Salaam

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Ingrid msichana mrembo, alianza kuishi ghetto baada ya kukorofishana na mama yake. Baba yake alifariki Ingrid akiwa bado mdogo. Ghetto waliishi maisha ya fighting for survival. Kitanda kimoja na ilikuwa ni marufuku kurudi na mwanaume.

Siku moja Jumamosi akiwa club alikutana na Damian kijana aliyekwenda likizo Arusha akitokea Dar. Damian alimuelewa sana Ingrid na mwisho wa Disco waliishia katika nyumba ya wageni. Asubuhi waliagana Daniel alitaka kumuacha Ingrid nyumbani kwao ili jioni akamchukue. Ingrid alikataa kabisa kumuonyesha Damian ana poishi. Baada ya mahojiano marefu alifunguka kuwa anaishi ghetto. Damian aliumia sana kumuona mtoto mzuri anapata tabu. Alimuomba Ingrid atafute chumba yeye atagharamia.

ingrid alipata chumba akiwa anaishi guest house na Damian mpaka walipomaliza kununua kitanda, na vitu muhimu kwenye chumba. Walianza maisha kwa wiki chache kabla Damianhajarudi kwao Dar.

Wazazi wa Damian ni wazaliwa wa Arusha na likizo hii Damian alitaka kufahamu maisha ya Arusha. Baada ya likizo kwisha aliondoka akiwa na mambo mengi kichwani na hakuwa na plan za kurudi Arusha kumuona ingrid. Walifurahia maisha na aliweza kuyabadilisha maisha ya Ingrid kwake iliishia hapo.

Mwezi mmoja baada ya kurudi Dar, Damian alipata ujumbe kutoka kwa Ingrid kuwa ni mjamzito. Ingrid alitaka aitoe mimba kwani imeshaweka kiwingu kwenye maisha yake. Damian kwa mara ya kwanza aliomba ushauri kwa mama yake. Mama alimwambia kama ni damu yako inabidi ubebe majukumu.

Damian alihakikisha anamtumia Ingrid matunzo yote na kumsihi asiitoe ile mimba. Ingrid alijifungua salama mtoto wa kiume. Mama Damian alimkaribisha Ingrid na mtoto Dar. Ingrid alitumiwa ticket ya ndege. Alifika Airport na kumkuta Damian anawasubiri. Walifika nyumbani na kulikuwa na shamra shamra kubwa. Mipango ya tohara, ubatizo na mambo mengi. Kustuka miezi Sita ilikuwa imepita na Ingrid akiwa na mimba ya pili ya Damian.

Mama Damian alimuelewa sana Ingrid ni msichana mwenye mawawzo ya maendeleo. Alimshauri asome QT afanye mitihani akiwa anamsaidia ulezi. Ingrid alianza shule baada ya kujifungua mtoto wa pili. Nyumbani alimsaidia mama Damian katika biashara za duka na bar.

Damian alikamatwa na madawa ya kulevya na kufingwa jela miaka mitano. Ingrid alisikitika sana. Ingrid alimaliza mitihani ya kidato cha nne na kujikinga na chuo cha Uhazili Magogoni. Alimaliza Diploma ya Secretarial na kupata kazi kwenye ofisi ya Balozi wa nchi za Ulaya.

Baada ya Damian kutoka jela uhusiano wake na Ingrid ulivunjika. Ingrid alilea watoto wake ingawa walikwenda kwa baba yao kila weekend. Ingrid alikutana na Mnigeria kazini na alifunga nae ndoa. Kila mtu aliishi kwa raha na starehe.

Unaemsaidia si lazima umuoe.

Wengine wanakua changu doa kwa kukosa msaada.
 
Back
Top Bottom